Kisusi Mohammed
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 563
- 468
Imekuwa ni kama kasumba kwa watu wengi waliofikia rika la kujitegemea kukosa uchaguzi sahihi wa kuyaendea maisha yao kwa usahihi endelevu utakao mjenga na kumuendeleza katika kuyakabili maisha yake ya kila siku.
Wengi wamekuwa wanashindwa kuamua ni kipi haswaa ni cha kipaumbele katika mambo mengi ya msingi ya kufanya ili maisha yawe bora na yenye furaha.
Kwa Mfano: Kuoa au kuolewa, kuwa na usafiri (gari, pikipiki, baiskeli), kujenga nyumba, kununua shamba, kununua kiwanja, kuwekeza katika hisa, kusafiri nje ya nchi katika kutafuta kipato cha ziada au kufanya lolote lenye muelekeo wa kimaendeleo.
Hivyo basi kwa mtazamo wa haraka haraka nikiwa kama mmoja wa waliopata tabu sana katika kuamua kipaumbele, nikaonelea haitakuwa vibaya faida hii nikaifikisha mikononi mwa wanaJF ili kila mwenye wazo lake na atupe alichonacho ili kesho na keshokutwa kwa watakaopata mawazo haya mazuri wayatumie na wasiishie kuapata tabu kama mimi.
Swali la msingi: NI KIPI CHA KUKIPA KIPAUMBELE KATIKA HAYO MENGI NILIYOYATAJA HAPO JUU?
Natumai nimeeleweka.