political monger senior
JF-Expert Member
- Nov 26, 2020
- 1,801
- 5,788
βΊβΊ 'ππ½πππ πππ ππ ππΌππΌππ'
Ameandika mchambuzi Jemedari Said
"Nawapongeza Simba SC kwa kutwaa ngao ya jamii, nampongeza kijana wangu, Ally Salim kwa kuzuia penati (3) ni ushujaa mkubwa.
"Zaidi nampongeza Ally Salim kwa mbinu yake ya kutoka hatua moja mbele kabla mpira haujapigwa na kumuibia mpigaji na mwamuzi msaidizi ambaye ndio huwa mwenye shughuli ya kuangalia kama kipa ametoka kabla ya mpira kupigwa.
"Ukiangalia penati zote Ally Salim alikuwa anatangulia kutoka kabla mpira haujapigwa, hata ile moja (Ya Azizi Ki) aliyofungwa ni vile tu mpira ulikuwa na kasi.
"Nampongeza Ally Salim kwa mbinu hii ambayo leo imemsaidia kwa kutokuwa na waamuzi makini pia. Lakini nampa tahadhari, mbinu hii siku hizi ni HARAMU na ikitokea ukaokoa basi penati inarudiwa, hivyo leo penati zote (3) zingerudiwa. Ukibisha angalia video kwa umakini.
"Diarra anaweza kuwa mwalimu mzuri kwa namna alivyookoa penati yake kwa kuhakikisha mguu mmoja unabaki kwenye mstari wakati mpira unapigwa na sio kutokea mbele hatua moja.
"Simba furahieni leo na Ngao mmebeba, ila kwenye mechi zenye waamuzi makini msije mkarusha ngumi tu, kipa anatokea mbele hatua moja kabla mpira kupigwa ambayo ni makosa."
Jemedari Said
Mchambuzi wa Efm Radio
"Ally Salim anastahili pongezi nyingi kwa kile alichokionesha katika mchezo dhidi ya Yanga, kudaka penati (3) dhidi ya wanafainali sio mchezo.
"Lakini kuna jambo ambalo halikuwa sawa kwa upande wa waamuzi ambao ndio wenye jukumu la kusimamia sheria zote uwanjani.
"Ki kawaida golikipa wakati wa kudaka penati hapaswi kutoa miguu yake yote kabla mpigaji hajapiga mpira, lakini kwa Ally Salim ilikuwa tofauti alikuwa anatoka hata kabla mpira haujapigwa.
"Katika penati zote (3) alizocheza zilistahili kurudiwa kwani zilikuwa zinapigwa wakati ambao ameshatoka kwenye mstari.
"Bado tuna safari ndefu sana kuhusu waamuzi wetu na sheria hizi"
Edgar Kibwana
Mchambuzi wa Clouds fm radio