Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni

Ndugu Rejao huwa sipendi hoja zako lakini hii imenikuna na nilipoiona hii picha kwa mara ya kwanza kule MICHUZI nilijiuliza maswali mengi sana..nadhani mwenyekiti inatakiwa atoe ufafanuzi hapa..
idumu Tanzania..mungu Ibariki chadema yetu!
 
wewe kimeo hizi ndizo sheria mbaya za matumizi serikali ya ccm na wake zao cuf walijitungia ili kulihujumu taifa.Mbowe alipolikataa hili gari aliambiwa kuwa anavunja sheria.
kwa hiyo ndiyo maana tunakuambia chadema ni chama makini ndiyo maana wakaweka katiba mpya kwenye ilani yao sii hilo tu kuna wabunge viti maalum,chaguzi ndogo ,mikopo kwa wabunge,posho,kiti cha spika,ccm kufanyia vikao vyake ikulu nk.

Ringo,

Hebu naomba tujuze sheria inasemaje mazee? kuna mambo mangapi ambayo Chadema wameyapenga mazito sembuse hili dogo la kukataa gari!

Sidhani kama kuna swala la kisheria hapo, hamna ulazima wa yeye kutumia hiyo gari na akikataa sidhani kama sheria itasema kwamba anavuliwa ubunge, sasa nashangaa kwanini hafanyi maamuzi magumu?
 
Siku nyingine fahamu nchi inaendeshwa kwa protokali,haiendeshwi kama familia yako unavyotaka kuiendesha..alichokuwa anataka kupinga ni protokali ambazo hazina mashiko kwa watanzania kwa sasa..ila jiulize,hata akilikataa ilihali limeshanunuliwa kuna mantiki hapo?bora litumike,next time pengine serekali itakuwa imejifunza jambo

Kama Mbowe alikuwa anayojua yote hayo kwa nini aliwatanganzia Wananchi kuwa anarudisha gari la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni...halafu hajarudisha.
 
We rejeo mbona umekimbia kwenye post ya wasira kuzomewa waambie na gamba wenzako mrudi kwanza kule
 
Mi ningependa kwanza tukumbushane yaliyojiri wakati ule...hoja ilikuwa kubadilisha magari yanayotumika hivi sasa na kuanza kutumia ya gharama nafuu...la kuuliza kwanza ni kuwa ameshaletewa la gharama nafuu akaligomea na kuendelea kutumia v8? kama jibu ni bado akiendelea kutumia la kwake lenye gharama nafuu, sheria itamruhusu kufidiwa gharama mbalimbali kama vile mafuta,service,driver na mengineyo?..
 
View attachment 54426
Kwa taarifa tulizonazo na wanachi wengi wanavyofahamu, tayari hili gari V8 limekwisharudishwa na Mh. Freeman Mbowe. Lakini cha kushangaza bado huyu mkuu analitumia.

Nashindwa kuwaelewa hawa CDM, kelele zote wanazopiga ni kutuhadaa tu wananchi? Kama kwa hili dogo huyu Mh. kashindwa kulitekeleza, je hayo anayoyahubiri kila siku majukwaani ataweza kuyatekeleza?

Hii inanifanya nikose imani na wapinzani, yapo mengi tu wanayoyazungumza mbayo ukijaribu kuyaangalia utekelezaji wake ni kitu kisichowezekana. Cha muhimu hawa viongozi wetu wasiwe ni watu wa kutudanganya ili kujipatia umaarufu. Kama ukiamua kufanya kitu, fanya kweli!!

Ebu liangalie swala hili kwa mapana kidogo ninaamini wewe si mtoto mdogo wakufikiri hivyo, Mboe anapigania mfumo mzima wa ununuzi wa magari ya bei juu ambao unatekelezwa serikalini nzima na kulisababishia taifa hasara kubwa za mabilioni ya fedha na tena mpaka ku ya maintain hayo magari ni gharama kubwa yaani spare na service kwa ujumla, sasa kukataa gari ambalo limekwishanunuliwa kunamnufaisha nani? jaribu kuliangalia hili na usitangulize chuki tujaribu kuwa wakweli na kauli hii ya Mboe ndio imefanya serikali kuangalia upya mfumo mzima wa uagizaji magari ya watumishi wake na tayari wameanza kuufanyia kazi.
 
Nawashangaa sana nyie mnaokazana kusema CDM ni chama cha kauli na hawazitekelezi hao magamba wameshawahi kukutekelezeeni mangapi? Barabara, umeme, maji, elimu, afya,maisha bora kwa kila mtanzania lipi kati ya hayo kwako limefanikiwa? Wachani kwa washabiki wakinafiki ulitaka hata akitumia gari yake binafsi asitumie hiyo plate number ya KUB?
 
Rejao,

Huo ndio ukisikia unafik na kukurupuka kwa viongozi wa CHADEMA. Huwa wanarukia hoja zisizo na mshiko na Watanzania wanaowashabikia hawa jamaa nao huwa kama misukule au kondoo waliopotea, hawana fikra wala mawazo wanaswagwa kupelekwa wanapotaka hao wachungaji wao na wenyewe wanaenda vichwa chini.
 
Rejao,
Huyu ni Mbunge na anapewa mkopo kwa ajili ya kununua gari pia ,isije ikawa hiyo plate number imewekwa katika gari yake lakini isiyo kuwa ile aliyopewa kama KUB...ni vyema kujiridhisha kabla ya kumtolea mtu uamuzi..!
 
Mkuu ritz, Hicho ndicho kinachosababisha watu wengi wanaojua kuchambua mambo wakose imani na wapinzani.
Kama waliamua kukakataa kitu, wangebaki na msimamo wao huo huo.
BTW, CHADEMA ni kama gari bovu lisilo na uelekeo maalumu. hawana common goal, kila mtu anajiamulia anvyojua. Leo kiongozi wa BAVICHA atasema hivi, kesho makamu wake atasema hivi, Slaa naye atakuja na lake, Mbowe naye...

Rejao unajaribu kuhitimisha kitu gani kwenye hii thread? Ni muhimu tukubaliane kuwa nchi hii imedorora sana kiuchumi, kidira, kimaadili na nyanja zingine kutokana na kuwa na sera mbovu za CCM na watawala wasiojali maendeleo ya nchi. Sera mbadara zinahitajika sasa ili kubadili mwelekeo wengi. Ni wazi kuwa sera za CDM zimeanza kuleta mwelekeo mpya. Je hili wewe hulioni?

Hebu fikiria rushwa zinavyoturudisha nyuma. Wanyama hai wanasafirishwa jua la saa nane, mchanga wetu unasafirishwa bila ya wananchi kuwekwa wazi. Je mikataba ya madini inafichwa kwa manufaa ya nani? Hatutaki nchi hii iwe shamba la bibi.
 
Rejao,
Huyu ni Mbunge na anapewa mkopo kwa ajili ya kununua gari pia ,isije ikawa hiyo plate number imewekwa katika gari yake lakini isiyo kuwa ile aliyopewa kama KUB...ni vyema kujiridhisha kabla ya kumtolea mtu uamuzi..!

Hiki ni kitu kisichowezekana,
 
Rejao unajaribu kuhitimisha kitu gani kwenye hii thread? Ni muhimu tukubaliane kuwa nchi hii imedorora sana kiuchumi, kidira, kimaadili na nyanja zingine kutokana na kuwa na sera mbovu za CCM na watawala wasiojali maendeleo ya nchi. Sera mbadara zinahitajika sasa ili kubadili mwelekeo wengi. Ni wazi kuwa sera za CDM zimeanza kuleta mwelekeo mpya. Je hili wewe hulioni?

Hebu fikiria rushwa zinavyoturudisha nyuma. Wanyama hai wanasafirishwa jua la saa nane, mchanga wetu unasafirishwa bila ya wananchi kuwekwa wazi. Je mikataba ya madini inafichwa kwa manufaa ya nani? Hatutaki nchi hii iwe shamba la bibi.
Lakini sioni wa kumnyooshea mwezake kidole kwa haya yote. Hao wanaojidai wanaweza kuibadili Tanzania na mfumo uliopo, ndio hao hao ambao hawawezi kusimamia wanayoyasema.
 
Nimeshawahi kusema mara chache na sitochoka kusema tena - Ushabiki tumeuweka mbele kiasi tunatumia nguvu kupinga hoja badala ya kutumia hoja zenye nguvu katika kutetea utawala, uongozi, dhamana na uwajibikaji; na kupinga ufisadi, ubadhirifu na kutowajibika.
Tumekuwa tukilinganisha mabaya yetu badala ya mema yetu, kiasi tumefika pahala kila linapokuja suala zito linalomgusa kiongozi yoyote wa chama tunaishia kurudia yale yale:
- wetu hawajibiki kidogo tu, wenu hawajabiki sana,
- wetu ni fisadi kidogo tu, wenu ni fisadi sana,
- wetu anatukana kidogo tu, wenu anatukana sana n.k.

Hoja ya magari ya gharama ilianza na mtoto wa mkulima aliposema atalirudisha, amelirudisha? Kutorudisha gari Pinda hakumhalalishii Mbowe kuling'ang'ania. Vivyo hivyo kwa hoja ya posho. Wengi wamepinga, wangapi wamezikataa? Wengine kutokataa posho, hakuwalalalishii wengine kuzipokea.

Hata hivyo, ikiwa mmoja tu atakataa posho au gari, huyu atakuwa anawapa kauli na hoja wananchi wanaoliliwa vyao. Awe Pinda awe Mbowe, kukubali gari la mamia ya mamilioni ya gari wakati wananchi wananchi wanapelekewa vibajaji vya kuuzia Ice cream kama magari ya kubebea wagonjwa huo ni usaliti kwa wananchi.

Kwenye siasa, heshima ya kiongozi yeyote ni kutumiza ahadi zake, awe wa chama tawala au cha upinzani. Mimi nisingemuoana Mbowe mbaya kwa sababu ni mpinzani wala nisingemuona Pinda ni mwema kwa sababu ni mtawala au kinyume cha yake - WOTE WANWASALITI WANANCHI KWA KAULI ZAO.
 
Ebu liangalie swala hili kwa mapana kidogo ninaamini wewe si mtoto mdogo wakufikiri hivyo, Mboe anapigania mfumo mzima wa ununuzi wa magari ya bei juu ambao unatekelezwa serikalini nzima na kulisababishia taifa hasara kubwa za mabilioni ya fedha na tena mpaka ku ya maintain hayo magari ni gharama kubwa yaani spare na service kwa ujumla, sasa kukataa gari ambalo limekwishanunuliwa kunamnufaisha nani? jaribu kuliangalia hili na usitangulize chuki tujaribu kuwa wakweli na kauli hii ya Mboe ndio imefanya serikali kuangalia upya mfumo mzima wa uagizaji magari ya watumishi wake na tayari wameanza kuufanyia kazi.
Chamuhimu hapa siyo FIXED cost ambayo tayari imeshakuwa sunk cost ya kulinunulia hili gari. issue ipo kwenye maintainance, angekuwa amelikataa kama alivyosema, serikali ingekuwa imesave kiasi kikubwa sana cha fedha. Kuendelea kulitumia ni kuuongezea mzigo serikali.
 
Naomba kujua tarehe siku mwaka uliopiga hiyo picha kwani picha hata ya mwaka 2000 unaweza kuitumia kishabiki

Mh Mbowe anatumia gari alilopewa na Serikali kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni. Wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki mwaka huu niliwahi kumuona akipita nalo likiwa na namba rasmi na bendera ya taifa.
 
Back
Top Bottom