Kiongozi ni sifa ila ukikosa sifa moja wapo kati ya hizi haufai kuwa kiongozi na ondoka madarakani

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,556
2,999
Uongozi sio tunu wala sio nguo kwa hisani utapatiwa ila ni nidhamu pamoja ushawishi wa kimamlaka ambapo unatakiwa kuvionesha hata kabla haujafika katika ngazi ya uongozi,leo nitaorodhesha sifa tano ambazo kiongozi unatakiwa kuwa nazo hata kabla hujaomba ridhaa ya kuwa mgombea.

1. Nguvu ya ushawishi, matendo na maneno yako yanatakiwa kurelate kile ambacho kipo ndani ya moyo wako kwa kuangalia mazingira pamoja hali ya wale ambao unataka kuwaongoza au unaowaongoza lakini unaposhindwa kuwa na nguvu ya ushawishi dhamira yako ya kuwa kiongozi ifute kabisa.

2. Uthubutu wa kutenda, zipo nyakati ambazo utakumbana nazo zitakufanya usijue ni uamuzi sahihi wa kuchagua ila unapokuwa ari ya kutekeleza jambo bila kujali situation hapo utaweza kuwa na sifa ya kuwa kiongozi ndiyo maana wengi wenye uthubutu hufanikiwa kuliko yule,mwenye mikwamo mingi.

3. Kusikiliza ushauri,baadhi ya mambo unatakiwa kusikiliza wenzako wanasemaje ila sio kila jambo wanaweza kukushauri vyema hivo unahitajika kuwa na uthubutu wa hali ya juu.

4. Sifa ya Kuunganisha, najua kuna baadhi ya mambo hutokea yanaweza kufarakanisha na hasa karne za sasa kuna mambo mengi yanayohusu interest,kanuni na sheria, itikadi na imani huwa ni zenye kugawa ila unatakiwa kuwa mwenye busara ya kuunganisha ila zikitokea hali za sitonfahamu huna budi kuchukua maaamuzi magumu,binadamu hajakalika na siyo kila jambo ufikirie nadharia moja.

5.Kubali kushindwa,unapoanguka tambua kuwa unaishi katika ulimwengu wa ushindani,mahesabu na kanuni hivyo kuna muda utakosea jaribu kutambua makosa yako na uanze upya au jiweke pembeni kabla ya jambo halijawa baya zaidi.


Mwisho kabisa pendelea kutoa shukrani
 
Back
Top Bottom