Kiongozi anayehamasisha vurugu hatufai

Status
Not open for further replies.
watanzania tuwe macho na viongozi ambao wapo tayari kuingia ikulu kwa kukanyaga damu zetu, viongozi wanaochochea vurugu ili tu wapate kutimiza malengo yao ya kisiasa tuwaepuke viongozi wa namna ni hatari kwa taifa letu, amani ikitoweka wao huondoka na familia zao nje ya nchi na kutuachia vurugu, tunataka mabadiliko kwa njia ya Amani. Mpenda Amani.

Unacho ongea ni sahihi kabisa kwako kwa vile uko thoughtlessness,ndio maana unaona kuhoji wizi wa kodi yako unaofanywa mchana kweupe na watu wachache kwa maslahi ya familia zao wakati wewe na nduguzo mmepigika kimaisha mpaka kifikra,au kupaza sauti ili huduma za kijamihi kama elimu,afya,barabara,kuheshimu haki za raia,kuhoji uadilifu uliopotea kwenye vyombo vyetu vya dola kwako wewe ndio unaona ni uchochezi,its a shame kwa kua watu wenye iq kama yako ndio mnaofurahiwa na ili genge la wahuni na matapeli wa rasilimali zetu walio chini ya kimvuli cha uongozi!haya maneno yako wewe si wa kwanza kuyatoa,walishayatoa watu wenye dhamana na chama chao na wenye kufahamika nchi nzima kama Wassira,Nnauye nk lakini wamekuja kujigundua Watanzania wamewapuuza kwa vile vichwa vyao vimefunguka siku hz,hawako tena katika dimbwi la ujinga wa kudanganywa kwa hoja za kitoto eti machafuko,udini,ukabila etc!cream ya watu wenye mawazo kama yako kwa Tanzania ya leo ndio inaelekea ukingoni,watu wanakimbilia kujikomboa kifikra na kimaisha mkuu,na hawataki kubaki tena kwenye ignorance siku hizi!
 
Mtoa maada Gamba kubwa wewe tena bahati yako sikujui. Mbona hukumkataa JK na alisema siko tayar Gamba linifie kuna nn pale Ikulu?
 
Mkuu umekuja vibaya, hapa ni Home of Great Thinkers mkuu, siyo kwa wajinga wajinga ambao wanazidi kuchakaa kwa sababu ya kusikiliza maneno maneno kama hayo toka kwa viongozi wao. Hayo maneno hapa si mahali pake hata kidogo, na wewe wafahamu hilo, japo ume-post kwa kuwa umetumwa au uko kwenye system. You dont care about others.

mkuu kamchina kangu hakawezi kugonga LIKE tu.

Umetisha sana mkuu
 
Hakuwez kuwa na aman wkt wananch wana njaa ma2mbon mwao alaf viongoz wana kula national cake na wake na matoto yao
 
Unaweza kumtaja kiongozi yeyote ambae ametoa kauli ya kuchochea vurugu..? Ambae amelazimisha wananchi wapigane ili waingie ikulu..?
Ninachoona mie ni Viongozi wenye busara wanaowasihi wananchi kutulia pamoja na kuona kwamba haki yao inaporwa.. Rasilimali ya taifa ikitafunwa na wajanja wachache..
Nakumbuka uongozi wa serikali pale Mbeya ulipotumia nguvu dhidi ya wamachinga.. Matokeo yake kukalipuka mapambano na polisi kushindwa kuyazuia.. Ni Mh. Joseph Mbilinyi aliekwenda na kutumia dakika mbili kumaliza fujo..
Nakumbuka maneno ya Mh. Mbowe pale Arusha.. Alipokuwa akiwasihi wananchi watulie pale walipokuwa wameshikwa na jazba baada ya kuona haki yao ya ubunge imenyang'anywa.. Na kweli wananchi wakatulia..
Nakumbuka maneno ya Mh. Dr. Slaa pale alipomshauri JK avunje baraza lake la mawaziri kutokana na kuwa ni mzigo na wezi wa mali ya umma.. Ushauri ambao JK aliupuuza na mwisho wa siku tunaona matokeo yake.. Wananchi wana hasira.. Wamedanganywa..
So ni vizuri ukawashauri wenzio hao ya kuwa itafika wakati wananchi watachoka.. Na hawatamcikiliza Mh. Mbowe wala Dr. Slaa..! Wataingia mitaani wao wenyewe na kwa kuongozwa na uchungu wa nchi yao.. Hilo likitokea hata risasi haitaweza kuwazuia..
 
'Lakini amani peke yake haina maana katika maisha ya mwanadamu kama amani yenyewe maana yake ni kutokuwako mapigano. Maana amani ya namna hiyo inaweza ikawa kisingizio tu cha kudumisha dhuluma inayowapokonya binadamu wengi sana haki ya utu wao.' J. K. Nyerere-kwa mabalozi wa nchi za nje walioko Tanzania. Januari 1, 1968.

Wataje hao viongozi!!

you have made my day,thanks a lot bravo.
 
watanzania tuwe macho na viongozi ambao wapo tayari kuingia ikulu kwa kukanyaga damu zetu, viongozi wanaochochea vurugu ili tu wapate kutimiza malengo yao ya kisiasa tuwaepuke viongozi wa namna ni hatari kwa taifa letu, amani ikitoweka wao huondoka na familia zao nje ya nchi na kutuachia vurugu, tunataka mabadiliko kwa njia ya Amani. Mpenda Amani.

Unatushauri tuwakumbatie Viongozi wanaouza viumbe hai ili watuuze na sisi watanzania kisha wao wabaki peke yao? niambie nani anaeleta vurugu hapa au kuhamasisha
Comrade kama kuuzwa uuzwe peke yako,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom