Kioja kikuu Bungeni leo!!

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,027
Dah yule mbunge(CCM)ni mtu mzima kwelikweli...

Kasema mshahara wake wa kwanza 1970's ulikuwa 1200, alinunua kitanda, radio na sofa kwa ajili ya kumkaribisha GF(girlfriend) wake!!
Huyu ndie kamtetea Wassira akilala asipigwe picha!!kisa katoka mbali, na Mrema alipigwa picha denda linamtoka kalala bungeni. Kamwaga pumba hata point zake kwa taifa sijaziona!!

Dah magamba kazi ipo!!
 
hao mpwa ndio mwisho wa akili zao na mawazo yao umefikia hapo we twende tukaangalie simba akifungwa tu
 
Dah yule mbunge(CCM)ni mtu mzima kwelikweli...

Kasema mshahara wake wa kwanza 1970's ulikuwa 1200, alinunua kitanda, radio na sofa kwa ajili ya kumkaribisha GF(girlfriend) wake!!
Huyu ndie kamtetea Wassira akilala asipigwe picha!!kisa katoka mbali, na Mrema alipigwa picha denda linamtoka kalala bungeni. Kamwaga pumba hata point zake kwa taifa sijaziona!!

Dah magamba kazi ipo!!

Hao wabunge wa ccmagamba mbona wengi wako kwenye kipindi gani kile? .....wamerudi kuwa watoto,ni hadithi hadithi kwenda mbele na sasa saa yakwenda kwetu tutaonana keshooooooo!

Hilo tu ndilo walilokalia bungeni akili zimechoka hawawezi kusoma hata alama.
 
kwani amelidanganya bunge? shilingi ilikuwa na thamani kubwa kipindi kile, hilo la girlfriend mi simo.
 
Yaani kazaliwa mkoa mmoja na Tundu Lisu AKA Wabunge wa CCM 100? Ama kweli watu hutofautiana.... Nilidhani brain inaweza kuambukiza angalau akawa na akili kidogo.
 
Bwahahahahahahahahahahahahaaaaaa
Siamini kama mwakilishi wa watu timamu anaweza kumwaga shuzi kama hilo mjengoni
 
Hivi ngoja niulize...wabunge wengi(wote) CCM wanaikubali bajeti za wizara 100%, lakini hoja zao zinatoa kasoro nyingi hoja wanazozikubali asilimia mia!! hii mbona siielewi?? Huyo Maji Marefu kamwaga pumba kuisifia wizara ya utumishi wa umma badae anatoa kashfa na kudai ndio uongozi gani huu??sasa hii mi siielewi, nahiso kama hawajielewi wanapoongea!!
 
Bwahahahahahahahahahahahahaaaaaa
Siamini kama mwakilishi wa watu timamu anaweza kumwaga shuzi kama hilo mjengoni

Mkuu hayo ndiyo magamba, wamefika ukomo wa kufikiri, mawazo yooooooooooooote kwenye posho tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu.
 
anaumwa yule! na inaelekea wabunge wa ccm kazi yao ni kuongea pumba ili kusogea muda mbele ili muda uishe tu hawana kipya hawa
 
kwani amelidanganya bunge? shilingi ilikuwa na thamani kubwa kipindi kile, hilo la girlfriend mi simo.

Sasa kama huyo gf wake sio yule mke wake wa ndoa nahisi chumbani patachimbika sana akirudi!!
 
mimi nafikiri wapiga kura nao waache kuchagua wabunge ambao akili zao zimeisha choka, mtu aliye kuwepo 1970 nafikiro kwa sasa hafai kuwepo kwenye utawala, labda wachache tu ambao wamejipambanua tofauti na hao,
 
Mimi aliyenishangaza leo ni yule aliyesema kutoa pesa ndogo (kama elfu mbili au kumi) sio rushwa ni kama kutoa msaada kwa mtu anayekusaidia kazi aitoe vizuri....

Eti kama Doctor hana umeme kwanini usimpe 10,000 ili anunue Generator ili akusaidie vizuri?
 
Kuna haja ya Spika kupewa mwongozo ili ahakikishe wabunge wajenge hoja zinazojikita katika mambo yanayojadiliwa. Kama kuna haja ya mbunge kusema mambo mengine apewe dakika chache kiasi kwamba hapotezi muda wa hoja za msingi. Ushauri wangu ni kama ifuatavyo:1. Kama kuna sababu ya lazima kwa mbunge kuzungumza mambo mengine kama kuwashukuru wapiga kura wake, chama chake,rais, waziri, mchumba, rafiki yake(kike au kiume) nk. basi atumie 10% ya muda wake. Haina maana kama mbunge atatumia 30% ya muda mwingi kuwashukuru watu mbalimbali katika kachangia hoja ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu wakati mjadala hauna uhusiano wa moja kwa moja na shukrani hizo atakazotoa.2. Mbunge atumie 90% ya muda uliobaki katika hoja husika. Mfano: Mbunge anayetaka kuzungumzia kero katika eneo lake ahakikishe kero hiyo inahusiana na mjadala husika. Muda aliopewa ndiyo autumie vizuri hapo na siyo kuchanganya maelezo yanayohusika katika maeneo mengine.Imekuwa desturi kwa mfano mbunge anazungumzia kero ya mambo yahusuyo kilimo wakati hoja inayojadiliwa inahusu utawala bora.
 
Mimi aliyenishangaza leo ni yule aliyesema kutoa pesa ndogo (kama elfu mbili au kumi) sio rushwa ni kama kutoa msaada kwa mtu anayekusaidia kazi aitoe vizuri....

Eti kama Doctor hana umeme kwanini usimpe 10,000 ili anunue Generator ili akusaidie vizuri?

Yule ni Viti maalum(CHADEMA) hata mimi nilikuwa simwelewi, anaongea kwa mapozi kama kanywa mvinyo vile....!!
 
Yule ni Viti maalum(CHADEMA) hata mimi nilikuwa simwelewi, anaongea kwa mapozi kama kanywa mvinyo vile....!!

Chadema eee....kisha Kitila aseme model yake ya uchaguzi ilikuwa bora wakati waliochaguliwa ni hopeless
 
Back
Top Bottom