Kinywaji cha Mo Extra: Ni mimi tu au na wengine...?

Habari waungwana, jana nilinunua kinywaji cha MO EXTRA nikanywa.. Baada ya muda fulan nikaanza kujisikia tofauti...

Maumivu kiasi upande wa moyo kisha yakapotea...

Maumivu ya abnomial hasa upande wa kulia kupanda juu hado katikati ya kiuno na ubavu wa mwisho.... Usawa wa figo

Uvivu katika kufikiri ilhali najisikia uchangamfu kiasi....

Kuna aliyewahi kujisikia hali hii baada ya kutumia hiki kinywaji?

Wajuvi wa afya mna maoni gani juu ya kilichonisibu?.. View attachment 1145914
Kamuone daktari wa figo utanishukuru baadae.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Ushauri wangu kwako ndugu Achana na vinywaji vya Aina iyo jizoeshe kunywa maziwa na maji kwa wingi ujiondoe kwa unywaji wa macaffein
 
Amewatengenezea wajinga



Wewe hujui serikali ya wanyonge hapo inapata kodi kutoka kwa wanyonge kwa vifo vya wanyonge kwa faida ya wanyonge.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mumpe hata akiwa kaburini.😁😁
 
Afya yako mgogoro unasingizia kinywaji cha watu.Kila mtu na mwili wake,sasa kama wewe kimekushinda acha sio kuuliza kila mtu vinginevyo una lako jingine.Kumbuka hakuna ambacho hakina madhara dunia ya leo.
 
Energy Drinks sio nzuri kuzitumia kama haujajua status ya afya yako:-Hazifai kwa watu wenye shida ya:-
-Kisukari
-Pressure
-Magonjwa ya Moyo,Ini,Figo etc

Pia hazifai kutumiwa na Wamama Wajawazito,Dhumuni la Energy drinks lilikuwa kukupa exra energy na relaxation kwenye brain hasa kwa wanajeshi wakiwa vitani ila kwa sasa hata mtu tu katulia masaa 24 hafanyi shughuli yeyote anakunywa hayo "MATAKATAKA" hata chupa tatu kwa siku.
 
Kama kahawa ingekuwa na shida unayojaribu kueleza basi wengi wangeshaacha... Wewe mwili wako kushindwa kuhimili kahawa si kwa wote..
Angalia tafiti
Kunywa tu kahawa ndugu sijatoa sheria bali ni maoni yangu tu mkuu...
 
Back
Top Bottom