Kingunge Retires!

Wote ni wabunge, lakini wanapokuwa ndani ya bunge hawa wa rais na viti maalum, huitwa wabunge wa kupendelewa huwa hawana heshima kabisa mbele ya wabunge wa kuchaguliwa bungeni, na hata mawaziri,

Kama nikujiuzulu uwaziri kwa Kingunge, ni mpaka aseme kuwa anajiuzulu na ubunge pia, otherwise bado anaendelea mpaka mwisho wa 5 years term.

Mzee hilo ni dongo zito kweli na ni ukweli uliouchi, personaly sioni kama ni jambo la busara mtu asiye na mandate ya wananchi kuingia kwenye bunge. Kwa sababu huko bungeni hatakuwa na la msingi kwa maslahi ya wananchi zaidi ya maslahi ya aliyemteua au chama kilichompa nafasi ya upendeleo. Hii system ya kutoa upendeleo naona wazi kabisa kuwa inalemaza watu, hasa kwa wabunge wanawake wanaoingia kwa upendeleo naona hii ni aibu kubwa sana kwao, ingawa kuna baadhi ya watu wanajaribu kuidefend kwa kuiita affirmativie action, lakini ni matusi na dharau. Kwa wanaume ndio dharau kabisa, afadhari hata kina mama wanaweza kujustfy hii kwa historia mbaya ya ubaguzi kutokana na mila na desturi. Kama inavyojulikana Paka huwa hali panya aliyeletewa, anapaenda na anaweza kumsaka mwenyewe na kumla, huyo ndio paka kweli, ukiona Panya anakula mizoga basi huyo ana tatizo, na anaweza kuliwa na paka wenzie.
Wanawake sasa hivi wanaweza mpambano uwanjani,ingawa kuna sababu ndogondogo zinawakosesha. Sina hakika ni wangapi wameshinda kwenye majimbo ya uchaguzi lakini for sure they can, wanaokuwa wa kuteuliwa na kupewa uwaziri matokeo yake ni kama Meghji, anasema anaonewa kwa kuwa yeye ni mwanamke, lakini hasemi kuwa lipewa ubunge kwa kuwa yeye ni mwanamke.
Nachotaka kusema kujiuzulu uwaziri kwa Babu kunakubalika, regardless ya kuteuliwa na Muungwana kuwa waziri au hapana, amejiona kuwa sasa yeye ni useless, na amekuwa mteteaji wa ufisadi badala ya kuwa mteteaji haki na wa maadili ya chama. Kwa hiyo kujiuzulu kwake ni ombi kuwa Muungwana na Pinda wasimfikirie kwenye cabinet mpya, naona ni jambo zuri! LInaweza kuwa limewapunguzia lawama wanaomsaidia JK kupanga safu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom