Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,894
Mbunge kuwasilisha hoja kupinga mijadala ya dini
Exuper Kachenje na Fred Azzah
MBUNGE wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu (CCM), jana ametangaza rasmi kuwa atatimiza ahadi yake ya kuwasilisha bungeni hoja binafsi ya kulitaka Bunge kupiga marufuku mijadala yote inayohusu masuala ya imani za dini ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria wakati wa mkutano wa 17.
Nyalandu alitangaza hatua hiyo katika mkutano na waandishi wa habari aliouitisha kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam akieleza kuwa tayari amepata wabunge wengi wanaomuunga mkono. Mkutano wa 17 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano utafanyika mwezi Oktoba.
Mbunge huyo pia alivitahadharisha vyama vya siasa kuwa makini katika kutunga sera na kuepuka kuingiza kwenye ilani za vyama vyao, mambo yanayoweza kusababisha mgawanyiko na utengano kwa wananchi.
Mbunge huyo kijana alidai kuwa tayari hoja yake imeungwa mkono na zaidi ya wabunge 100 kutokana na imani tofauti na vyama vyote vyenye wabunge, huku akijinadi kuwa anaamini kwamba hoja yake pia inaungwa mkono na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru.
Alidai kuwa idadi ya wabunge waliotia saini kuunga mkono hoja yake ni kubwa ikilinganishwa na sheria inavyosema kuwa ili hoja ikubalike, ni lazima iwe imesainiwa na wabunge watano.
Alibainisha kuwa kwa mujibu wa hoja yake, mijadala itakayoruhusiwa ni ile itakayokuwa na hoja mahususi inayohusu suala la dini, linalotishia usalama wa taifa na kuwa hilo lifanyike baada ya kujadiliwa na kuidhinishwa na kamati ya uongozi ya Bunge.
Alisema hatua hiyo ifikiwe baada ya kamati hiyo kujiridhisha kwamba hoja husika haikiuki masharti ya misingi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Hoja yangu ni kulitaka Bunge la Tanzania kupiga marufuku mijadala yote inayohusu masuala ya imani za dini ndani ya Bunge, isipokuwa endapo kutakuwa na hoja mahususi inayohusu suala la dini linalotishia usalama wa taifa," alisema na kuongeza:
"Hoja hiyo yaweza kujadiliwa tu baada ya kuidhinishwa na Kamati ya Uongozi ya Bunge na kujiridhisha kwamba ni mahususi na haikiuki masharti ya misingi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema Nyalandu.
Kuhusu vyama vya siasa, Nyalandu alisema:" Nadhani itakuwa vyema vyama kuepuka masuala ya dini na ukabila. Vyama vinapaswa kuwa makini katika ilani zake visilete mijadala inayoweza kuwagawa wananchi."
Alifafanua kuwa kimsingi hoja yake ameiandaa kwa kushirikisha wanasheria mbalimbali wakiwemo wa serikali na Bunge na kwamba, inalenga kupinga masuala ya imani za dini kujadiliwa ndani ya bunge kwa kuwa kufanya hivyo ni uvunjaji wa masharti na misingi ya katiba ya nchi ambayo serikali yake haina dini na hivyo kuwa ni hatari kwa amani ya nchi.
"Msukumo wa kuleta hoja, hii umechangiwa kwa kiasi kikubwa na tabia iliyojitokeza hivi karibuni ya baadhi ya wabunge kujadili na kuitaka serikali kukubali kutungwa kwa sheria itakayowezesha kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi pamoja na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kujiunga na Jumiya ya nchi za Kiisilamu (OIC)," alisema Nyalandu.
"Ni jambo la wazi kuwa zipo nchi ambazo zimejikuta kwenye migogoro mikubwa ya kisiasa na kijamii hadi kusababisha kuvunjika kwa amani na wakati mwingine hata vita kutokea... na ukifuatilia chanzo cha matatizo hayo, pamoja na mambo mengine, ni mijadala mbalimbali inayohusu masuala ya dini."
Alisema mijadala ya dini imekuwa mikali na huchangiwa kwa hisia za imani za dini na hivyo kufanya bunge kuacha masuala yenye manufaa kwa nchi na mustakabali wake.
Nyalandu alisema kuendeleza mijadala hiyo bungeni ni kukiuka masharti ya Katiba ya Tanzania inayotamka bayana kwamba Tanzania sio nchi ya kidini.
Alisema kwa maana hiyo si vizuri kwa Bunge kubariki uvunjwaji huo wa katiba.
Nyalandu alimuomba spika wa Bunge, Samuel Sitta na ofisi yake kuidhinisha hoja hiyo ili iwasilishwe katika mkutano wa 17 wa Bunge na kuwasihi wabunge kumuunga mkono.
Alisema kama Bunge halitapiga marufuku mijadala ya kidini bungeni, kunauwezekano siku zijazo hoja binafsi ya kutaka serikali ianzishe mahakama ya Kikristo ikawasilishwa bungeni na serikali kutakiwa kugharamia uanzishwaji wake.
Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyotolewa na Waziri Bernard Membe kwenye mkutano wa 16 wa Bunge mjini Dodoma Julai 18 mwaka huu, Nyalandu aliahidi kuwasilisha hoja binafsi kwenye mkutano wa 17, kulitaka Bunge kupitisha azimio la kutoruhusu kabisa kujadili masuala ya imani za dini ndani ya Bunge.