Kingunge amgeuka Kikwete: Ashambulia wazee wanaoshabikia mfumo wa serikali tatu; amponda Mwandosya!

MWANASIASA mkongwe aliyewahi kuwa swahiba na mshauri mkuu wa Rais Jakaya Kikwete, Kingunge Ngombale Mwiru, ametoa kauli nzito inayoonyesha hakubaliani na msimamo wa Rais Kikwete na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kingunge akimkejeli Rais na chama chake, ambacho yeye ni mmoja wa waasisi, alisema walikurupuka kukubali na kuanzisha mchakato wa Katiba mpya.

Kwa mujibu wa Kingunge, kabla ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza na kuanzisha mchakato wa Katiba mpya, CCM haijawahi kufanya kikao na kuamua kuhusu suala hilo, kama walivyofanya kabla ya mchakato wa kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1991.

Mbali na kumshangaa Kikwete na chama chake, vile vile Kingunge aliwashambulia wazee wenzake wanaounga mkono mapendekezo ya rasimu ya Katiba mpya kuhusu muungano wa serikali tatu.

Katika hali isiyo ya kawaida, Kingunge alisema wazee hao ni “sawa na watu waliochanganyikiwa”.

Anasema msimamo wake unatokana na ukweli kuwa CCM haijawahi kuwa na ajenda ya kuandika Katiba mpya na kwamba ndiyo maana suala hilo halikuwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.

Alisema hoja ya Katiba mpya ni ya wapinzani, hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kingunge alisema kimsingi aliyeafikiana na hoja ya wapinzani kuhusu Katiba mpya ni Rais, si CCM.

Kuhusu wazee hao ambao alisema “wamechanganyikiwa” Kingunge alisema anashangaa kuona wazee ni miongoni mwa wanaopendekeza muundo wa serikali tatu, kwani baadhi yao walishiriki katika kuunda mfumo huu uliopo ambao umedumu tangu mwaka 1964.

Alisema muungano wa serikali mbili umeleta mafanikio kwa kujenga udugu na umoja wa kitaifa na kwamba kwa sababu hiyo ungeachwa uendelee badala ya kupiga kelele kwamba ufutwe, ziletwe serikali tatu.

Alisema baadhi ya viongozi wameshindwa kuthamini mafanikio ya muungano na sasa mawazo yao yote yamekuwa yakielekezwa kwenye vyeo vyenye marupurupu.

Aidha alipinga kauli za baadhi ya viongozi wanaosema kuwa kuwepo kwa serikali tatu kutasaidia kuimarisha muungano. Alisema serikali tatu zitaua muungano.

Kingunge aliongeza kuwa kama serikali mbili ni sababu za kufa muungano huo, basi usingeweza kudumu kwa miaka 50 sasa.

“Huu ni mpango wa wakubwa kutaka kujiwekea mazingira ya vyeo, kwani wapo ambao tayari wamekwishajiandaa kuwania urais wa Tanganyika.

“Nilishangaa sana hata huko bungeni watu wanapeana sifa za kuwa fulani anastahili kuwa Rais. Huu ni upotoshaji mkubwa kwa taifa,” alisema, akirejea kauli iliyotolewa juzi na Waziri asiyekuwa na wizara maalumu, Profesa Mark Mwandosya, aliyemfagilia Spika wa Bunge, Anna Makinda, kwamba anafaa kuwa Rais.

Kingunge aliongeza kuwa kwa maoni yake lazima Katiba mpya iweke mipango ya maendeleo ambayo itashirikisha wananchi wa ngazi zote.

Kingunge alisema isiwe mipango hiyo inapangwa na viongozi kutoka juu na kuishusha chini bila kujua wanahitaji nini kabla.

Alisema Katiba inayotakiwa ni ile itakayosimamia na kupatikana kwa maendeleo yanayofanana kati katika jamii.

Kuhusu uraia wa nchi mbili, Kingunge alisema suala hilo lilikuwa linasemwa pembeni lakini sasa wanataka suala liingizwe kwenye Katiba.

“Mwanzo nilijua ni utani lakini nilishangaa suala hili kubwa kuliona limeingizwa kwenye kijitabu kilichotolewa na chama changu na kupendekeza hivyo,” alisema.

Alisema suala la uraia ni la nchi, hivyo chama kilipaswa kutoa nafasi kwa wananchi kujadili kwa kina jambo hilo na sio viongozi kujiamulia wenyewe.

“Kwa mfano nchi yetu ilipovamiwa na Nduli Idd Amini kama kungekuwa na vijana wenye uraia wa nchi mbili wangejiweka upande gani, hii ni mipango ya watu wanaopenda kunogewa na maisha kwenye nchi za watu,” alisema.

Alisema amekuwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kwa muda mrefu lakini hakuwahi kusikia hata siku moja kujadiliwa suala hilo ambalo ameliita kuwa la hatari.

Ni mzee wetu na uzee una kawaida zake.
 
mkuu ben, hivi tunavyoongea takataka zenu mlizopeleka tayari zimepigwa kiberiti maana zimeonekana ni uchafu. poleni sana kwa kupoteza muda na raslimali kwa kazi isiyo na faida

Kama kawaida yako na ubongo wako kama wa KITIMOTO! tehe tehe tehe!
 
Nilitegemea pengine angelinganisha aina za muungano kwa kukumbushia muungano wa serikali moja!Lakini kwa kuwa anaona serikali mbili ndio njia pekee ya yeye na familia yake kuendelea 'kutafuna' bac anatuletea blah blah zake!Time changes,miaka ya 47 sio miaka ya 2000,kwa hiyo atupishe na Tanganyika yetu!
 
Haa Haya mazito..Lakini Kingunge anadhani bado yupo ndani ya Mfumo wa chama kimoja na chama kushika hatamu ?
hajui kwamba katiba ni ya nchi na inahusu watu wote na nchi yao
amejisahau kuwa katiba si mali ya ccm ?
hawa ndio wale wazee waso takamabadiliko....wanao dhani ccm ina mamlaka ya kuwaamulia mustakabal wa raia wa nchii hi na wao hawana haki hio ya kutoa mawazo yao
yupo bado katika zimwi la zidumu fikra za mwenyekiti ( ingawa kwenye pesa na ufisadi fikra za mwalimu hazidumu kwani kampuni yake ya Parking services inakula hela yote ya parking za magari na tenda yenyewe ya kifisadi)
Kikwete anaona mbali anajua suala la katiba ni muhimu baada ya miaka 50 ya uhuru
wana nchi wanahitaji katiba mpya itayo tokana na matakwa yao
suala la muungano ni suala la muungano wa nchi mbili na inavo elekea sasa zanzibar hawataki tena kuendelea na mfumo uliopo
na kwa nini wazanzibari wamefikia hali hio .ni kutokna na watu kama kingunge kuwa na mawazo kuwa kwao wamei tawala zanzibar na sio equal partner wa muungano...wao ndio chanzo cha watu kudai muungano tofauti
kama kungekua na nia njema ya muungano huu basi hata hizi mbili isingekua tatizo lakini hakuna nia njema kutoka na watu kama kingunge

bora anyamaze kimya ajenge heshima yake ya uzeeni kuliko kuanza kupinga mchakato wa katiba ....hili si suala la kurudi nyuma vijana wengi wana lifatilia kwa nguvu zote
 
ndugu yangu una elimu ya kidato cha ngapi?
wamesema vema isiwe ni siku ya kuabudu. kwa hivo ukiacha siku nilizozitaja kuna jumatatu hadi alhamisi.
unabishana kitu cha kitoto kabisa,hujalipw ahiyo buku saba hadi sasa?

Kwahiyo ijumaa sio siku ya kufanya kazi? Au kwenye mapendezo kuna sehemu wanapendekeza Ijumaa isiwe siku ya kazi?
 
MZEE KINGUNGE, HAYA NI MANENO YA KIBIBLIA AMBAYO WEWE ULIAMUA KUIKANA " HUWEZI KUWEKA MVINYO MPYA KATIKA KIRIBA KIKUUKUU'' Mzee Kingunge wakati wako wa kufikiri umepita, Kwa yaliyopo sasa hivi kichwa chako hakiwezi kuya accomodate.Mzee umekwisha, kama Bwana Yesu alivyomwambia Petro ' Rudi nyuma shetwani' ndivyo tunaweza kumkemea shetwani kichwani mwako sasa, maana uyawazayo siyo watanzania wenye nafasi ya kuendelea kuishi na kuleta maendeleo ya nchi wayawazayo.
Napenda kumpongeza Mh. Rais Jakaya Kikwete, anajua nini watanzania wachotaka, yeye ni Rais wa watanzania wote na anajua mahitaji yao. Huwezi kushidana na Ukweli daima na Rais wetu amelijua hilo.

Mzee wewe kaa kimya vijana wachape kazi kulingana na wakati uliopo na ule tunaouendea.
 
Asilimia 90 ya alicho ongea hakina mashiko.. hoja zake zime kaa kienzi ya nyerenyere hivi.. umri wake umeisha kuwa tatizo kwa huyu mzee kupambanua mambo na kwenda na nyakati. Serikali mbili imeisha onesha kupwaya kwasasa nilazima tubadirike, alafu bado anataka maslai ya taifa yaendeshwe kichama kama zamani ilivyo kuwa.. mzee kingunge anashindwa tambua kuwa zamani kalibia wasomi wote walikuwa tanu ( ccm) na ndio maana kila kitu kilikuwa kinapita kwenye chama. Majority walikuwa ignorant nandio maana hii katiba tulio nayo kwa sasa
ilitungwa na watu kama sija kosea hawazidi kumi nambili tu na hao kutoka bara na visiwani. Sasa mzee mpaka leo hii bado anataka kubadilishwa katiba yawe ni maamuzi ya chama na yawe ndani ya ilani.!!??? Umri usababisha akili mgando na hawezi kwenda na wakati wa sasa na ameonesha wazi kuwa bado yupo kule enzi za tanu na sela za mwalimu zilizokuwa zina tija kwa kipindi kile.
 
Kingunge Ngombale-Mwiru aka Caetano, is a sheer flop in Tanzania politics. Huyu mzee akiwa na jina la caetano kule kipatimu alijaribu useminari ukamshinda akavua makanzu. Akaenda Urusi kujaribu u-marxist akavuruga nchi kama theorist wa ujamaa ambao umefeli vibaya. Mnamo 1991 akaenda Zanzibar na rhetorics zake akaua Azimio la Arusha na kuanzisha Azimioa la Zanzibar.Baada ya hapo akajaribu ubepari ambao sasa umemnogea kiasi kwamba kachanganyikiwa. Huyu mzee ni mwanasiasa mkongwe ambaye hajawahi kufanikiwa hata katika jambo moja. Miaka ya 1980 alipata kuwa waziri wa ushirika kwa matumaini atatekeleza dhana yake ya USHIRIKA WA UZALISHAJI MALI kama mkakati na mbinu ya kutekeleza ujamaa na kujitegemea, yeye akabaki pale Dodoma anapiga domo kinadharia wizara ikamshinda vibaya. Hivi sasa wanaomfahamu huwa hawamsikilizi kwani hana jipya. Ukisikiliza vizuri alichokuwa anasema utagundua bado anafikiria kichama kimoja kwa misingi Russian Vanguard Party na mkakati wake wa Democratic Centralism amepitwa na wakati akaenda na upepo. Mambo yamebadilika sana inaelekea huyu mzee hajui mabadiliko yaliyo-sweep across Tanzania.
 
Kudumu kwa miaka 50 ya muungano si kigezo cha mafanikio, kero kadhaa na malumbano yasiokwisha mbona yameshindwa kutafutiwa ufumbuzi. wala si hoja kama mzee alieunda muungano wa serikali mbili jana aendelee kudefend kitu hicho hicho hata kama mabadiliko ya dunia na wakati haiendani, kwani hata hapo ccm ilipoleta mchakato wa vyama vingi na wananchi kuukataa wakitaka kuendelea na mfumo wa chama kimoja, mbona ccm ilikubali? akiwemo yeye pia kwanini hakulinda kile alichokiunda na kukiamini na akakubali vyama vingi? Hoja potufu ya idd Amin na vita, kwanza hao wananjeshi wazanzibari hata kama wasingepelekwa wote kungelizidisha au kupunguza nini? mbona hasemi kama Mzee karume aliwazuia wanajeshi wazanzibari kuelekea msumbiji wakati wa mwalimu kwa sababu hakuwafiki hoja za mwalimu za ukombozi wa afrika na muungano ulikuwa ndio huu huu. Kwani huyu rais wa ccm au wanancho wote? hafikiri sababu za kuletwa huu mchakato wa katiba, haikuwa khiari ya ccm bali ni yale mabadiliko ya Zanzibar ya 2010 yalioridhiwa na 60% ya wazanzibari huku ikienda kinyume na katiba ya muungano, hakuwa na njia ya rahis isipokuwa kulirudisha suala la katiba kwa wadau wote. Hawa jamaa wamejawa na giza la ubabe, wakati unawapita, hii sio 64 ..
 
maneno ya huyu mzee utadhani siyo mwanachama wa ccm kumbe wale wale miongoni mwa walioua azimio la arusha na kuja na azimio la zanzibar.
 
Haa Haya mazito..Lakini Kingunge anadhani bado yupo ndani ya Mfumo wa chama kimoja na chama kushika hatamu ?
hajui kwamba katiba ni ya nchi na inahusu watu wote na nchi yao
amejisahau kuwa katiba si mali ya ccm ?
hawa ndio wale wazee waso takamabadiliko....wanao dhani ccm ina mamlaka ya kuwaamulia mustakabal wa raia wa nchii hi na wao hawana haki hio ya kutoa mawazo yao
yupo bado katika zimwi la zidumu fikra za mwenyekiti ( ingawa kwenye pesa na ufisadi fikra za mwalimu hazidumu kwani kampuni yake ya Parking services inakula hela yote ya parking za magari na tenda yenyewe ya kifisadi)
Kikwete anaona mbali anajua suala la katiba ni muhimu baada ya miaka 50 ya uhuru
wana nchi wanahitaji katiba mpya itayo tokana na matakwa yao
suala la muungano ni suala la muungano wa nchi mbili na inavo elekea sasa zanzibar hawataki tena kuendelea na mfumo uliopo
na kwa nini wazanzibari wamefikia hali hio .ni kutokna na watu kama kingunge kuwa na mawazo kuwa kwao wamei tawala zanzibar na sio equal partner wa muungano...wao ndio chanzo cha watu kudai muungano tofauti
kama kungekua na nia njema ya muungano huu basi hata hizi mbili isingekua tatizo lakini hakuna nia njema kutoka na watu kama kingunge

bora anyamaze kimya ajenge heshima yake ya uzeeni kuliko kuanza kupinga mchakato wa katiba ....hili si suala la kurudi nyuma vijana wengi wana lifatilia kwa nguvu zote

Ndo umegundua leo nchi inaendeshwa na cdm? Kunywa ile dawa inayoongeza spidi ya ubongo kufikiri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom