Kingunge amgeuka Kikwete: Ashambulia wazee wanaoshabikia mfumo wa serikali tatu; amponda Mwandosya!

Unafiki ulioko ccm muda mrefu unamfanya kingunge ajishangae mwenyewe, kwani nchi hii ni ya wananchi sio ya chama cha siasa asituvuruge na ukongwe wake. kwani muungano wa serikali mbili sio msahafu, ulikuwa wa Nyerere na karume, yeye alibaki anashabikia tu hadi leo, atuache wananchi tujadili katiba yetu, mbona hajishangai wakati ule alikuwa kijana leo ni kikongwe, angekataa abaki na ujana wake milele, kwani mpaka sasa tunapigania uhuru tena tubaki na katiba ile ile waliyoandika wachache? kingunge weeeeee!
 
Hii ni hoja ya KITOTO kuliko zote zilizotolewa tangu mchakato wa Katiba uanza.

Yaani Slaa anadhani siku ya kuabudu sio siku ya kazi. Hajui kuwa kuna dini ambazo kila siku ni siku ya kuabudu.

By the way, dini mpya zinaibuka kila siku na zina ratiba tofauti za ibada.

siyo maoni ya Slaa;
ni ya Watanzania!
 
Unahitaji degree kujua ni siku gani sio ya kuabudu?
sijaona wametaja jumapili
kwa kawadia huwa tuna ijumaa-waislamu, jumamosi -wasabato na jumapili wakristo wote.

Alitaja hoja ya kumi kuwa ni siku ya kupiga kura isiwe ni siku ya kuabudu ya imani ya dini yoyote ile, bali iwe siku ya kazi ambayo itapaswa kutangazwa kama siku ya mapumziko.
jitahidi basi kuelewa hata jambo lililo wazi.

Kwahiyo ijumaa sio siku ya kufanya kazi? Au kwenye mapendezo kuna sehemu wanapendekeza Ijumaa isiwe siku ya kazi?
 
Kwa kushirikiana na
kamanda Benson Mramba,Nikiwa kama mratibu wa maoni ya mabaraza ya
CHADEMA kwa njia ya mitandao,kwa niaba ya CHADEMA tunawashukuru kwa
maoni na ushirikiano wa kipekee mliotupatia katika zoezi la ukusanyaji
wa maoni ya mabaraza ya katiba.

Maoni yenu yametosha,yamehesabiwa na tena yametosha na kuwasilisilishwa.

Leo CHADEMA tumewasilisha maoni ya mabaraza yetu kwa tume ya uchaguzi
tukiongozwa na Katibu Mkuu Dr.Wilbroad Slaa.

Tumeweka rekodi ya kipekee kwa kukusanya maoni Millioni 3,462,805 .CCM
kupitia katibu mkuu wao Kinana walijivunia kukusanya maoni takribani
milioni 2 tu.

Pamoja na tume kutoandaa utaratibu mzuri wa kupokea maoni hayo lakini
tumewatendea haki watanzania.CHADEMA tumewasilisha maoni hayo yakiwa
"well packed" .

Tulitumia gari za M4C na Tume wameonyeshwa kushangazwa na kiasi hicho
kikubwa cha maoni na uwazi ambao CHADEamA kimeonyesha.

Tunatoa changamoto kwa CCM,nao waweke wazi maoni yao na yahesabiwe.

Asanteni sana kwa wale wote mlioshiriki zoezi hili,Sukrani za pekee kwa
ndugu Maxence Melo na timu nzima ya JAMIIFORUMS kwa kukubali kutumia
jukwaa lao kama sehemu ya kukusanyia maoni ya baraza letu la katiba.

Mwenyezi Mungu awabariki kwa uzalendo wenu huu

mkuu ben, hivi tunavyoongea takataka zenu mlizopeleka tayari zimepigwa kiberiti maana zimeonekana ni uchafu. poleni sana kwa kupoteza muda na raslimali kwa kazi isiyo na faida
 
Chadema walikuwa
wanawahutubia wanainchi hayo maoni wameyatoa wapi? Hili changa la macho
Hilo!!!!!!!!!!!!!!

mkuu, chadema wamewalaghai tu watanzania, hayo waliyotoa ni maoni yao na si maoni ya wananchi. ushahidi tunao na uko wazi
 
Huo ndio uwazi tunaoutaka watz!Ccm wamezoea kuburuta wananchi,hiyo 2m ni wana masaki,msasani,upanga,mikocheni na mbezi beach sio ya watanzania!CDM big up!!!
 
Namba 10,ni hoja nzuri ambayo dini zote wanaipigia kelele kuwa uchaguz usifanyike siku za ibada,Viva Chadema
 
Yaani watanzania wana maoni 11 tu?

Dr Slaa na chama chake wamechanganyikiwa kweli na hakika imedhihirisha athari ya akili ndogo kutawala akili kubwa. halafu huo muda wa kuchambua hayo maoni waliupata wapi. hakuna chombo chochote kiliketi kuchambua maoni hayo ya wananchi
 
Sikubaliani na yoote aliyozungumza Mzee Kingunge...ISIPOKUWA lifuatalo......

......“Nilishangaa sana hata huko bungeni watu wanapeana sifa za kuwa fulani anastahili kuwa Rais. Huu ni upotoshaji mkubwa kwa taifa,” alisema, akirejea kauli iliyotolewa juzi na Waziri asiyekuwa na wizara maalumu, Profesa Mark Mwandosya, aliyemfagilia Spika wa Bunge, Anna Makinda, kwamba anafaa kuwa Rais.

Kingunge aliongeza kuwa kwa maoni yake lazima Katiba mpya iweke mipango ya maendeleo ambayo itashirikisha wananchi wa ngazi zote.

Kingunge alisema isiwe mipango hiyo inapangwa na viongozi kutoka juu na kuishusha chini bila kujua wanahitaji nini kabla.

Alisema Katiba inayotakiwa ni ile itakayosimamia na kupatikana kwa maendeleo yanayofanana kati katika jamii.

........

Kusema ukweli Profesa Mwandosya.....alichemsha sana.....Siasa zimemfanya awe kama hajielewi anachozungumza siku hizi.....
 
Baada ya kukaa kimya muda mrefu, mwanasiasa mkongwe nchini, Kingune Ngombale-Mwiru, ameibuka na kuwatupia lawama viongozi wa CCM, kwa kutaka kupenyeza suala la uraia wa nchi mbili ndani ya Katiba Mpya. Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam jana, Kingunge alisema baadhi ya ‘wakubwa’ ndani ya chama hicho wanataka kuliingiza suala la uraia wa nchi mbili kwenye Katiba Mpya kwa masilahi yao binafsi, bila kuwashirikisha wanachama.

Alisema anashaanga namna ambavyo suala hilo limeingizwa kwenye kitabu kiitwacho ‘Ufafanuzi wa rasimu ya Katiba Mpya’ kilichoandikwa na chama hicho, kwa kuwa halikuwahi kujadiliwa katika mikutano ya wanachama.

“Lipo jambo limenikera sana, napenda niliseme na lieleweke vizuri linahusu uraia. Nimearifiwa kuwa kwenye kikao cha Kamati Kuu walikuwa wakijadiliana, mimi nastaajabu kweli kwa chama changu kuliingiza suala hili,” alisema Kingunge.

Alisema yeye analipinga kwa sababu lingekuwa kubwa lingejadiliwa na wanachama ambao ni wenye nchi.” Alisema anapinga pendekezo la Watanzania kuruhusiwa kuwa na uraia wa nchi mbili kwa sababu hoja zilizotolewa, hazina nguvu.

“Tunaambiwa eti Watanzania wengi wako Marekani na Ulaya na huko wana fursa nyingi, eti wakipata uraia wa pili watafaidi vizuri fursa hizo. Wanaosema hivyo wana matatizo kidogo, wanataka uraia wa nchi yao na uraia wa nchi nyingine,” alisema.

Akizungumzia rasimu ya Katiba Mpya, Kingunge alisema mapendekezo ya kuwa na Serikali tatu yanaleta mkanganyiko kwa wananchi na kwamba hilo ni tishio tu la kutaka kutoka kwenye Muungano sahihi
 
MWANASIASA mkongwe aliyewahi kuwa swahiba na mshauri mkuu wa Rais Jakaya Kikwete, Kingunge Ngombale Mwiru, ametoa kauli nzito inayoonyesha hakubaliani na msimamo wa Rais Kikwete na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kingunge akimkejeli Rais na chama chake, ambacho yeye ni mmoja wa waasisi, alisema walikurupuka kukubali na kuanzisha mchakato wa Katiba mpya.

Kwa mujibu wa Kingunge, kabla ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza na kuanzisha mchakato wa Katiba mpya, CCM haijawahi kufanya kikao na kuamua kuhusu suala hilo, kama walivyofanya kabla ya mchakato wa kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1991.

Mbali na kumshangaa Kikwete na chama chake, vile vile Kingunge aliwashambulia wazee wenzake wanaounga mkono mapendekezo ya rasimu ya Katiba mpya kuhusu muungano wa serikali tatu.

Katika hali isiyo ya kawaida, Kingunge alisema wazee hao ni “sawa na watu waliochanganyikiwa”.

Anasema msimamo wake unatokana na ukweli kuwa CCM haijawahi kuwa na ajenda ya kuandika Katiba mpya na kwamba ndiyo maana suala hilo halikuwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.

Alisema hoja ya Katiba mpya ni ya wapinzani, hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kingunge alisema kimsingi aliyeafikiana na hoja ya wapinzani kuhusu Katiba mpya ni Rais, si CCM.

Kuhusu wazee hao ambao alisema “wamechanganyikiwa” Kingunge alisema anashangaa kuona wazee ni miongoni mwa wanaopendekeza muundo wa serikali tatu, kwani baadhi yao walishiriki katika kuunda mfumo huu uliopo ambao umedumu tangu mwaka 1964.

Alisema muungano wa serikali mbili umeleta mafanikio kwa kujenga udugu na umoja wa kitaifa na kwamba kwa sababu hiyo ungeachwa uendelee badala ya kupiga kelele kwamba ufutwe, ziletwe serikali tatu.

Alisema baadhi ya viongozi wameshindwa kuthamini mafanikio ya muungano na sasa mawazo yao yote yamekuwa yakielekezwa kwenye vyeo vyenye marupurupu.

Aidha alipinga kauli za baadhi ya viongozi wanaosema kuwa kuwepo kwa serikali tatu kutasaidia kuimarisha muungano. Alisema serikali tatu zitaua muungano.

Kingunge aliongeza kuwa kama serikali mbili ni sababu za kufa muungano huo, basi usingeweza kudumu kwa miaka 50 sasa.

“Huu ni mpango wa wakubwa kutaka kujiwekea mazingira ya vyeo, kwani wapo ambao tayari wamekwishajiandaa kuwania urais wa Tanganyika.

“Nilishangaa sana hata huko bungeni watu wanapeana sifa za kuwa fulani anastahili kuwa Rais. Huu ni upotoshaji mkubwa kwa taifa,” alisema, akirejea kauli iliyotolewa juzi na Waziri asiyekuwa na wizara maalumu, Profesa Mark Mwandosya, aliyemfagilia Spika wa Bunge, Anna Makinda, kwamba anafaa kuwa Rais.

Kingunge aliongeza kuwa kwa maoni yake lazima Katiba mpya iweke mipango ya maendeleo ambayo itashirikisha wananchi wa ngazi zote.

Kingunge alisema isiwe mipango hiyo inapangwa na viongozi kutoka juu na kuishusha chini bila kujua wanahitaji nini kabla.

Alisema Katiba inayotakiwa ni ile itakayosimamia na kupatikana kwa maendeleo yanayofanana kati katika jamii.

Kuhusu uraia wa nchi mbili, Kingunge alisema suala hilo lilikuwa linasemwa pembeni lakini sasa wanataka suala liingizwe kwenye Katiba.

“Mwanzo nilijua ni utani lakini nilishangaa suala hili kubwa kuliona limeingizwa kwenye kijitabu kilichotolewa na chama changu na kupendekeza hivyo,” alisema.

Alisema suala la uraia ni la nchi, hivyo chama kilipaswa kutoa nafasi kwa wananchi kujadili kwa kina jambo hilo na sio viongozi kujiamulia wenyewe.

“Kwa mfano nchi yetu ilipovamiwa na Nduli Idd Amini kama kungekuwa na vijana wenye uraia wa nchi mbili wangejiweka upande gani, hii ni mipango ya watu wanaopenda kunogewa na maisha kwenye nchi za watu,” alisema.

Alisema amekuwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kwa muda mrefu lakini hakuwahi kusikia hata siku moja kujadiliwa suala hilo ambalo ameliita kuwa la hatari.

Tatizo la huyu mzee ni ile SEMBE kule kwa Prezda Zuma. Ndio maana kakasirika maana naye kanogewa na kaufisadi fulani hivi!!
 
Hivi wale wazee wanaosubiri kufa aliowalenga nape nnauye ktk kauli yaje kingunge hayumo?
 
Huyu mzee ametoka uwanjani na kukaa benchi ndio anaona wenzake wanavyocheza rafu while naye alikuwa anacheza rafu akiwa uwanjani??
 
Back
Top Bottom