Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinga na tiba ya ugonjwa wa kiharusi

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Oct 9, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 38,335
  Likes Received: 2,410
  Trophy Points: 280
  Kiharusi ni ugonjwa mkali wa mishipa ya damu kwenye ubongo unaohatarisha vibaya afya na maisha ya binadamu. Takwimu husika zimeonesha kuwa, kila mwaka watu milioni 1.5 wanapatwa na ugonjwa huo nchini China, na nusu kati yao wanakufa kutokana na ugonjwa huo, na watu wengi wanaopona wanapoteza uwezo wa kufanya kazi kwa viwango tofauti. Hali hiyo imesababisha mzigo mkubwa kwa familia na jamii.

  Mzee Wang Qinmei mwenye umri wa miaka 65 ana afya njema na hakuwahi kupatwa magonjwa makubwa. siku moja asubuhi katika majira ya mchipuko mwaka huu, alienda sokoni kwa baisikeli kununua chakula kama kawaida, ghafla alijisikia kizunguzungu na akapoteza fahamu. Baada ya muda mfupi, alipata fahamu na kuomba msaada kutoka kwa wapita njia na akapelekwa hospitali.

  Katika chumba cha huduma ya kwanza, daktari alithibitisha haraka ugonjwa uliompata mzee Wang. Daktari wa upasuaji wa mishipa ya damu kwenye ubongo katika hospitali ya 301 ya jeshi la ukombozi wa watu wa China Bw. Wang Jun alisema:

  "baada ya kumfanyia upimaji wa CTA, tuligundua sehemu moja nyembamba katika mishipa mikubwa ya damu iliyoko shingoni, na asilimia 90 ya sehemu hiyo ya mishipa ya damu imezibwa. Hali hiyo ni ya hatari sana."

  Tatizo la wembamba wa mishipa ya damu ya shingoni ni chanzo kikubwa cha ugonjwa wa kiharusi wa aina ya kukosa damu kwenye ubongo. Asilimia 60 ya wagonjwa wa ugonjwa huo wanatokana na tatizo la kuzibwa kwa mishipa ya damu ya shingoni. Pamoja na kuzidi kuziba kwa mishipa ya damu, dalili za ugonjwa huo zinaonekana kidhahiri na wazi zaidi, hatimaye zinasababisha kiharusi kibaya. Kwa kuwa asilimia 90 ya mishipa ya damu ya shingoni inakuwa imeziba, hali hiyo inaufanya ubongo ukose damu na oksijen, na dalili mbalimbali za ugonjwa huo zote zinasababishwa na tatizo hilo.

  Mbali na kiharusi cha kukosa damu kwenye ubongo, aina nyingine ni kiharusi cha kutokwa damu kwenye ubongo. Chanzo kikubwa ni shinikizo kubwa la damu linalosababisha mishipa midogo ya damu kwenye ubongo ivimbe na kupasuka.

  Kwanza, ugonjwa wa kiharusi unahusiana na umri na jinsia. Kwa kawaida, watu wenye umri wa zaidi ya miaka 55 wana hatari kubwa zaidi ya kupatwa na kiharusi, na hatari ya kupatwa ugonjwa huo kwa wanaume ni asilimia 50 zaidi kuliko wanawake. Ya pili, ugonjwa huo ni wa kurithi. Aidha, magonjwa ya shinikizo kubwa la damu, kisukari, tatizo la moyo, tatizo la kuwa na uzito kupita kiasi, kuvuta sigara na kunywa pombe zote zinaweza kusababisha kiharusi.

  Kwa kawaida, kuna dalili kadhaa zinaonekana kabla ya kutokea kwa kiharusi. Mkurugenzi wa idara ya upasuaji wa mishipa ya damu katika hospitali ya 301 ya jeshi la China Bw. Li Baomin alisema:

  "kabla ya kutokea kwa kiharusi, mgonjwa hujisikia kizunguzungu, mwasho kwenye mikono na miguu, na kutoona vizuri. Baada ya muda, hisia hiyo itaisha au itarejea tena. Kama una dalili hizo, ni lazima uchukue tahadhari."

  Bw. Li alisema, kama dalili hizo zinatokea mara kwa mara katika siku moja au mbili, na pia una shinikizo kubwa la damu au ugonjwa wa kisukari au ugonjwa wa kurithi, unapaswa kwenda hospitali mara moja kufanyiwa uchuguzi. Hivi sasa, ugonjwa wa kiharisi unaweza kuthibitishwa mapema na kwa usahihi.

  Basi kama wagonjwa wakipatwa na kiharusi nyumbani au kwenye sehemu za hadhara tutafanyaje? Watalaamu wanaeleza kuwa, kiharusi kinatokea ghafla, wagonjwa wanaweza kupoteza fahamu, kuanguka, kutikisika au kushindwa kuongea. Watu huchanganyikiwa wakati hali hiyo ikitokea, na hata wanakuwa hawajui la kufanya. kwa kawaida, watawaamsha hata kuwatingisha wagonjwa. Vitendo hivyo vinaweza kuwadhuru wagonjwa hao, hata vinafanya hali yao iwe mbaya zaidi.

  Kama mtu akipatwa kiharusi, kwanza jamaa zake wasihangaike, bali wanatakiwa kumtuliza mgonjwa, na ni afadhali wasimwamshe alipo, lakini wanatakiwa kumwita daktari mara moja. na ni bora walegeze nguo za ndani za mgonjwa, hatua hiyo inamsaidia mgonjwa kupumua bila tatizo. Kama mgonjwa akitikisika, hali hiyo ni mbaya, ni lazima wamshtue. Kwa kuwa wakati huo, mgonjwa anaweza kujiuma ulimi, hivyo ni afadhari wazibe mdomo wa mgonjwa kwa nguo. Wagonjwa wengi wa kiharusi wanatapika, ili kuzuia wagonjwa kama hao wasijizibie koo, ni bora kuwalaza shingo upande. Kama matapishi yakibaki mdomoni, ni lazima yatolewe mdomoni kwa vijiti, na kama mgonjwa huyo ana meno bandia, inapaswa kuyatoa ili yasije yakaingia kooni.

  Zamani ugonjwa wa kiharusi ulikuwa unatibiwa kwa upasuaji, hivi sasa unatibiwa kwa matibabu yenye usalama, ufanisi na rahisi zaidi. Matibabu hayo ni kuingiza mrija mdogo kwenye mshipa mkubwa wa damu wa pajani na kuifikisha kwenye sehemu yenye tatizo mwilini na kutibu. Kwa kuwa kipenyo cha mshipa mkubwa wa damu ni milimita 15 hivi, na kipenyo cha mirija ni milimita 2 tu, hivyo mrija huo unaweza kupita kwenye mishipa ya damu bila tatizo. Mbali na hayo, kutokana na kuwa hakuna nevu za hisia ndani ya mishipa ya damu, basi wagonjwa hawasikii maumivu.

  Mzee Wang Qinmei alitibiwa kwa matibabu hayo. Daktari aliweka chombo maalum cha kupanua mshipa wa damu ndani ya sehemu ya mshipa mkubwa wa damu wa shingoni kwake iliyozibwa kwa kutumia mirija. Mzee Wang alisema:

  "Baada ya kuwekewa chombo cha kupanua mshipa wa damu, nilisikia damu inapita vizuri, ghafla hisia ya kizunguzungu iliondoka mara moja."

  Matibabu hayo hayahitaji kuwapa wagonjwa nusukaputi ya mwili mzima. Wagonjwa wanaweza kutibiwa wakiwa na fahamu vizuri. Pia kwa kuwa matibabu hayo yanaleta majaraha madogo tu, basi wagonjwa wanaweza kutembea saa 24 tu baada ya matibabu. Hivi sasa, wagonjwa wengi zaidi wa kiharusi wanachagua matibabu hayo.

  © China Radio International.CRI. All Rights Reserved.
  16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040

  china radio international
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mungu akusidishie MziziMkavu, kwa maelekezo yako ya tiba pamoja na tiba zako za asili.
  Wengi zimetusaidia
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 38,335
  Likes Received: 2,410
  Trophy Points: 280
  Asante sana na wewe pia akuzidishie Mungu kila la kheri sisi Mwenyeezi Mungu alituumba tuwe tunawasaidia watu wengine kimawazo,kidawa, kifikiria na kila kitu bila kuhitaji kitu chochote zaidi ya dua zenu tu. Ingawa sisi wengine hatujakwenda chuo kikuu

  lakini mwenyeezi Mungu ametupa talent Vipaji vya kuwasaidia watu Tangu mwaka 1980 nilikuwa naweza kuwasaidia wengi tu na pia nina kipaji cha kuweza kumsoma mtu uso wake yaani psikoloji, saikoloji na kumjuwa huyu mtu ana matatizo gani na njia gani aweze kuifanya ili matatizo yake yamuondokee nina mambo mengi tu lakini machache ni hayo asante sana Mkuu ubarikiwe.
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 38,335
  Likes Received: 2,410
  Trophy Points: 280
  Machungwa, Zabibu Hupunguza Uwezekano wa Kupata Kiharusi?
  [​IMG]

  Utafiti mpya uliofanyika nchini Marekani umesema ya kwamba kula machungwa na zabibu kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi (Stroke).

  Utafiti huo uliangalia faida za matunda chachu (Citrus Fruit) pekee kwa mara ya kwanza tofauti na tafiti nyingi ambazo tumezizoea zinazoangalia umuhimu wa matunda na mboga za majani kwa afya kiujumla.
  Utafiti huu umehusisha maelfu ya wanawake wanaoshiriki katika tafiti ya manesi Nurse’s Health Study lakini wataalamu wanaamini faida hizo za machungwa na zabibu pia zinapatikana kwa wanaume.

  Timu ya watafiti katika chuo cha Norwich Medical School katika Chuo Kikuu cha East Anglia wamechunguza umuhimu wa kemikali aina ya flavonoidsambayo ni jamii ya antioxidant (kemikali zinauwa kemikali hatari za kwenye mwili) inayopatikana katika matunda, mboga za majani, chocolate nyeusi na wine nyekundu.

  Utafiti huu ulifuatilia takwimu za miaka 14 za wanawake 69,222 ambao walikuwa wakishirki katika tafiti kwa kuandika kiwango chao cha kula matunda na mboga za majani kwa kila kipindi cha miaka 4. Timu hiyo ya utafiti iliangalia

  uhusiano wa aina sita ya flavonoids - flavanones, anthocyanins, flavan-3-ols, flavonoid polymers, flavonols na flavones na hatari ya aina mbalimbali za kiharusi kama Ischaemic, Hemorrhagic na Total Stroke. Ilionekna wanawake waliokula kiwango kikubwa cha flavanones kwenye matunda chachu walikuwa na asilimia 19 ya uwezekano wa

  kupunguza kiharusi kulinganisha na wanawake ambao walikula kiwango kidogo cha matunda hayo.
  Kiwango kikubwa cha flavanones kilikuwa 45mg kwa siku kulinganisha na kiwango kidogo cha 25mg kwa siku. Utafiti huu ulichapishwa katika jarida laMedical Journal Stroke umesema flavanones hupatikana kwa asilimia 82 kwenye

  machungwa na juisi ya machungwa na hupatikana kwa asilimia 14 kwenye zabibu na juisi ya zabibu. Hata hivyo watafiti hao wamesema kwa wale wenye kusudio la kuongeza kiwango kikubwa cha flavanones itawalazimu kula tunda la chungwa kwa wingi na si juisi za machungwa zinazotengenezwa kiwandani kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kinachopatikana katika juisi hizo za viwandani.

  Professa Aedin Cassidy wa masuala ya lishe bora (nutrition) na ambaye alikuwa kiongozi wa utafiti huo amesema “kula kwa wingi kwa matunda, mboga za majani, na hasa Vitamin C uhusishwa na kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi”. Flavanones hutoa kinga dhidhi ya kiharusi kutokana na kuongeza ufanisi wa mishipa ya damu kwenye ubongo

  na kutokana na kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi mwilini (Anti-inflammatory effect).
  Utafiti uliofanyika hapo awali ulionyesha ya kwamba ulaji wa matunda chachu na juisi yake na si matunda ya aina nyingine yoyote hupunguza uwezekano wa kupata kiharusi aina ya Ischaemic Stroke na kuvuja damu kwenye ubongo(Intracerebral Haemorrhage).

  Utafiti mwingine uliofanyika kipindi cha nyuma ulionyesha hakuna uhusiano wowote wa matunda ya njano na machungwa katika kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi lakini ulionyesha ya kwamba kuna uhusiano wa zabibu na mapeasi wa kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi.

  Katika utafiti mwingine uliofanyika nchini Sweden umeonyesha ya kwamba wanawake ambao walikula kiwango kikubwa cha antioxidant karibia asilimia 50 kutoka kwenye matunda na mboga za majani, ni wachache tu kati yao waliopata kiharusi ikilinganishwa na wanawake ambao walikuwa na kiwango kidogo cha antioxidant.

  Matokeo ya utafiti huu yasiwafanye watu kuacha kula matunda ya aina nyingine pamoja na mboga za majani kwani nayo yana faida kubwa katika mwili wa binadamu.

  Kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi inawezekana kama mtu atakula lishe bora iliyo na virutubisho vyote muhimu, kula matunda na mboga za majani kwa wingi, kufanya mazoezi mara kwa mara, kupunguza kiwango cha ulaji chumvi (kwani watu wenye asili ya Kiafrika wana kiashiria cha asili kinachojulikana kama salt retention gene ambacho hufanya

  kiwango kidogo cha matumizi ya chumvi mwilini kuonekana kama kiwango kikubwa na hivyo kuongeza hatari ya kupata kiharusi), kupunguza uzito (kuwa kwenye uzito unaotakikana kiafya kulingana na umri na urefu wako), kupunguza kiwango cha matumizi ya mafuta katika chakula, kulala masaa ya kutosha na kupunguza msongo wa mawazo.BUGANDO HEALTH MOVEMENT: Machungwa, Zabibu Hupunguza Uwezekano wa Kupata Kiharusi?
   
 5. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  MziziMkavu pamoja sana. yaani nafutatiria sana kujua afya zetu na kutupa dawa pengine ushauri unatusaidia sana.
   
 6. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mkuu shuke bila hekima ya Mungu ni bure ninachoamini ni ufahamu wa Mwenyezi Mungu ni bora sana kuliko hata kusoma shule na kumaliza shahada, Master na pengine Phd.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2014
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 38,335
  Likes Received: 2,410
  Trophy Points: 280
  KULA NYANYA UJIEPUSHE NA KIHARUSI


  [​IMG]

  SOTE tunajua ugonjwa wa kiharusi (stroke) ni miongoni mwa magonjwa hatari kwani ukikupata unaweza kudhoofisha baadhi ya viungo vyako vya mwili kama siyo vyote na kukufanya ushindwe kufanya kazi zako za kawaida na kuwa mtu wa ndani tu kwa maisha yako yote.

  [​IMG]

  Lakini unaweza kujiepusha na ugonjwa huo hatari kwa kuzingatia ulaji wa vyakula sahihi pamoja na kufanya mazoezi. Utafiti wa hivi karibuni umebaini kwamba nyanya (tomatoes) hutoa kinga mwilini dhidi ya ugonjwa wa kiharusi au kupooza kama unavyojulikana na wengine.

  Hivi karibuni, watafiti wa nchini Finland walifanya utafiti wa kina na kutoa taarifa kuhusu kirutubisho aina ya ‘lycopene’ kinachopatikana kwa wingi kwenye nyanya, matikitimaji na

  pilipili. Wamesema katika taarifa yao kuwa watu zaidi ya 1,000 waliowafanyia utafiti wenye kiwango kingi cha ‘lycopene’ kwenye mfumo wa damu zao, hawakuonesha dalili kabisa za kupatwa na kiharusi.

  Aidha, Chama cha Taifa cha wenye Kiharusi cha nchini Marekani (The National Stroke Association) kimesema kuwa wanawake wengi hufariki dunia nchini humo kutokana na

  kiharusi kwa idadi sawa na wale wanaofariki kutokana na ugonjwa wa saratani ya matiti. Hii ina maana kwamba ugonjwa wa kiharusi nao ni tishio kama ilivyo kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.

  Utafiti mwingine katika eneo hilo umeonesha pia kuwa wanaume wana hatari kubwa zaidi ya kufariki dunia au kupatwa na matatizo mengi kutokana na ugonjwa wa kiharusi kuliko

  wanawake. Hivyo kati ya wanaume na wanawake, wanaume zaidi ndiyo hupatwa na kiharusi au matatizo yatokanayo na ugonjwa huo kuliko wanawake.
  [​IMG]

  Utafiti huu mpya umeendelea kuthibitisha ukweli wa siku zote kuwa matunda na mbogamboga hutoa kinga katika mwili wa binadamu dhidi ya magonjwa mengi hatari,

  hivyo wito umetolewa tena wa watu kupenda kula matunda na mbogamboga hasa nyanya, matikitimaji pamoja na pilipili ambavyo vimeonekana kuwa na kinga kubwa zaidi mwilini.

  Hata hivyo, imeelezwa kuwa baada ya matokeo ya utafiti huu, watu wamekumbushwa umuhimu wa kuendelea kula na aina nyingine ya matunda, kwani kila tunda au mboga

  ya majani ina faida na umuhimu wake katika mwili wa binadamu.
  Mwisho imeelezwa kuwa ulaji wa nyanya za aina zote una faida, iwe ni ile inayopikwa pamoja na mboga au ile inayoliwa ikiwa imeiva bila kupikwa. Ni vizuri kuchangamkia ulaji

  wa vitu kama hivi ili kuipa miili yetu uwezo wa kujikinga wenyewe dhidi ya maradhi hatari, yakiwemo yale ya saratani ambayo kwa kiasi kikubwa huweza kuzuiwa kwa kula mboga za majani na matunda ya aina mbalimbali.


   

  Attached Files:

 8. jobel

  jobel JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2014
  Joined: Mar 26, 2013
  Messages: 322
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mkuu MziziMkavu, asante sana kwa kuendelea kutupa elimu ya mambo mengi.Mwenyezi Mungu azidi kukujalia afya njema na nguvu.
   
 9. Tarime one

  Tarime one JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2014
  Joined: Nov 12, 2013
  Messages: 1,822
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 160
  Asante sana Mzizimkavu nimekupata vilivyo, naomba mawasiliano yako please.
   
 10. issa mahamba

  issa mahamba Member

  #10
  Feb 15, 2014
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Vizuri hii ni nzuri
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2014
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 38,335
  Likes Received: 2,410
  Trophy Points: 280
  Mwasilianao yangu nitafute nitumie email baruwa ya pepe Email Address yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com
   
 12. Mshomba

  Mshomba JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2014
  Joined: Apr 7, 2013
  Messages: 1,521
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Mzizi mkavu Mungu pekee ndie wa kukulipa kwa hili na usichoke kutuwekea elimu ya tiba hapa jamvini
   
 13. C

  CHIGANGA JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2014
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakushukuru sana kaka,umenipa elimu ya kutosha,mungu akubariki sana,
   
 14. pandagichiza

  pandagichiza JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2014
  Joined: Jul 9, 2013
  Messages: 659
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Naomba kujua matibabu kwa aliye pata stroke miaka 4 iliyopita
   
Loading...