Ugonjwa wa kiharusi/ kupooza (stroke): Kinga, tiba na jinsi ya kukabiliana na maradhi haya

Umeleta maana ya ya ugonjwa wa (stroke) Sio kiharusi na Tiba ya huo ugonjwa wa Kiharusi ni ngumu kutibika .

MziziMkavu,

Kama nimekupata vizuri ni kuwa kuna tofauti ya KIHARUSI na STROKE Please?
Mkuu Azimio Jipya Kiharusi ni neno la kiswahili kwa kiingereza maana yake ni Stroke mkuu nenda katafute dictionary ya Kiingereza kwa kiswahili utapata maana ya neno la Kiingereza Stroke kwa lugha yetu ya kiswahili ni kiharusi.

Mzimzi mkali where are you!!
Mkuu Azimio Jipya Nipo unasemaje?
 
Last edited by a moderator:
Habari Zenu Wanajamii,

Baba yangu anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza toka Mwaka jana, amepooza upande wa kushoto ila hakuahtirika kichwa, vilivyo athirika ni Mguu na Mkono. Tumenda kwa Wataalam tofauti wa wakienyeji na mahospital bila mafanikio. Kwa sasa mguu na mkono wake umekakamaa kiasi hata kuukunja inabidi utumie msuli. Mwenye kujua dawa au wapi naweza kumpeleka mzazi wangu akapata kupona naomba anijuze.

Asanteni
 
Ugonjwa wa Kiharusi

ImageProxy.mvc

Kiharusi ni hali inayotokea pale mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo inapopatwa na misukosuko kiasi cha kushindwa kupeleka damu kwenye ubongo na hivyo kuathiri ufanyaji kazi wa ubongo kwa zaidi ya masaa 24.

Kulingana na shirika la afya duniani kiharusi ni nakisi katika neva ambayo hutokana na tatizo katika mishipa ya damu ya ubongo na ambalo huendelea zaidi ya masaa 24 au kukoma ndani ya masaa 24. Muda wa masaa 24 umechukuliwa ili kutofautisha kiharusi na

kiharusi cha kukosa oksijeni katika ubongo (ischemia) ambacho hutokea na kudumu kwa muda mfupi yaani (transient ischemic attack).

Kwa kawaida dalili za TIA hupotea na mtu kurudia hali yake ya kawaida ndani ya masaa 24.

Aina za kiharusi

Kiharusi kimegawanyika katika aina kuu mbili kulingana na jinsi kinavyotokea (visababishi vyake). Aina hizo ni

1. Kiharusi cha kukosa hewa kwenye Ubongo (Ischemic stroke)

Aina hii ya kiharusi hutokea iwapo usambazaji wa damu katika sehemu ya ubongo hupungua na kupelekea tishu za ubongo za eneo liliathirika kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

Aina hii ya kiharusi husababishwa na nini?

Aina hii ya kiharusi husababishwa na

  • Damu iliyoganda kuziba mishipa midogo ndani ya ubongo (cerebral thrombosis) au
  • Kipande cha damu kumeguka na kwenda kuziba mshipa wa damu kwenye ubongo(cerebral embolism)
  • Kupungua kwa usambazaji wa damu kwa ujumla kwa mfano shock.
  • Vena thrombosis
2. Kiharusi cha kuvuja damu ndani ya Ubongo (Haemorrhagic Stroke)

Aina hii ya kiharusi hutokea pale ambapo mishipa midogo ya damu ndani ya ubongo hupasuka na kusababisha kusambaa kwa damu ubongoni (cerebral hemorrhage). Mara nyingi aina hii ya kiharusi hutanguliwa na dalili za kichwa kuuma, au kuwepo kwa historia ya ajali ya kichwa.
Visababishi vya Kiharusi (kwa ujumla)

  1. Wakati fulani, mishipa ya damu huzungukwa na aina fulani za mafuta yasiyofaa mwili, hali inayoitwa kitaalamu kama atherosclerotic plaque. Hali hii husababisha kuganda kwa damu katika mishipa (thrombosis) hiyo. Kuganda huku kwa damu kunaweza kutokea kwenye mishipa mikubwa au midogo inayopeleka damu kwenye ubongo. Baadhi ya mishipa mikubwa ya damu inayoweza kuathirika na tatizo hili ni pamoja na arteri za common carotid na interior carotid arteries, na arteri za vertebral. Nyingine ni mishipa midogo inayounda eneo linaloitwa circle of willis lililo katika ubongo.
  2. Kuganda kwa chembe nyekundu za damu za mgojwa wa sickle cell kunaweza pia kusababisha kuziba mishipa ya damu hivyo kusababisha Kiharusi.
  3. Kuganda kwa damu (embolus) kwenye mishipa ya damu ya sehemu nyingine za mwili au (hewa, mafuta, kusanyiko la vijimelea kama bakteria waletao ugonjwa wa endocarditis) huweza kusababisha kuziba kwa mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo kusababisha kiharusi.
  4. Upungufu wa usafirishaji damu mwilini (systemic hypoperfusion) - Wakati fulani moyo hushindwa kusukuma damu vizuri kwenda sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo ubongo kutokana na kufa kwa sehemu za nyama ya moyo kwa kukosa damu ya kutosha (Ischaemic Heart Diseases) au kutokana na kujaa kwa maji kwenye gamba lake la nje (pericardial effusion) au kupungua kwa damu mwilini, kunakoweza kusababishwa na mambo kadhaa. Hali hii husababisha sehemu kubwa ya mwili ikiwemo ubongo kukosa oksijeni ya kutosha na kusababisha kuathiriwa kwa sehemu ya ubongo.
  5. Shinikizo la damu la muda mrefu lisilothibitiwa linaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa midogo inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo damu kujaa kwenye ubongo (Intracerebral hemorrhage).
Dalili za kiharusi

Dalili za kiharusi hutegemea na eneo la ubongo liliathiriwa.

  1. Iwapo sehemu ya ubongo mkubwa ( Cerebellum) itaadhirika, mgonjwa atakuwa na dalili kama kushindwa kutembea vizuri, hivyo kuathiri mwendo wake, kujihisi kizunguzungu na pia kutapika.
  2. Iwapo sehemu ya ubongo wa kati (cerebral cortex) itakuwa imeathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za kushindwa kuongea,kushindwa kuelewa lugha inayozungumzwa, kushindwa kuona vizuri, kuwa na ukosefu wa kumbukumbu, kuwa na mvurugiko wa mpangilio wakw wa kufikiri, kuchanganyikiwa, na kubadilika kwa mwendo wa harakati za hiari.
  3. Iwapo mgonjwa ataadhirika sehemu ya ubongo kwenye shingo kuelekea kwenye uti wa mgongo (brain stem), mgonjwa anaweza kuwa na dalili za kuhisi mabadiliko ya harufu, ladha, kusikia na kuona; kulegea kwa misuli ya macho (ptosis); kupungua kwa ufahamu na kulegea kwa misuli ya uso; Ulegevu wa Ulimi (kushindwa kutoa nje au kusogeza upande upande); kupungua uwezo wa kumeza; ulegevu wa misuli ya shingo na kushindwa kugeuza shingo upande mmoja; kushindwa kusimama sawasawa na kuona vitu kwa hali ya utofauti; mabadiliko ya upumuaji na kiwango cha moyo kudunda.
  4. Iwapo sehemu mojawapo ya mfumo mkuu wa neva (central nervous system) imeathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za kupoteza ufahamu kwa upande mmoja wa mwili na kulegea kwa misuli ya uso, kuhisi ganzi mwilini, na kupungua kwa ufahamu wa hisia na hisia mtetemo.
Aidha bila kujalisha eneo lililoathiriwa, mgonjwa pia anaweza kuwa na dalili za kupoteza fahamu, maumivu makali ya kichwa na kutapika. Dalili hizi za kuumwa kichwa na kutapika kwa kawaida hutokea kwa mgonjwa mwenye kiharusi cha kuvuja damu (hemorrhagic stroke) ambacho husababisha ongezeko la shinikizo na mgandamizo wa ubongo ndani ya fuvu kutokana na kuvuja kwa damu.
Vipimo

  • Mionzi
  • CT-scan
  • MRI
  • PET
  • SPECT
Vipimo vingine ni;

  • ECG, ECHOCARDIOGRAM huwezesha kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia) na kama kuna damu iliyoganda kwenye moyo ambayo inaweza kufika kwenye ubongo
  • Holter monitor husaidia kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia) zinazotokea kwa vipindi
  • Angiogram huwezesha kugundua matatizo kwenye mishipa ya damu, na ni mishipa ipi ya damu iliyoziba.
  • Vipimo vya damu huwezesha kutambua uwepo wa lijamu mwilini (hypercholesterolemia) na mabadiliko mengine katika damu
Vihatarishi vya kiharusi

Vitu vinavyoweza kumuweka mtu katika hatari ya kupata kiharusi ni pamoja na

  • Shinikizo la damu lisilothibitiwa
  • Kisukari
  • Uvutaji sigara
  • Unywaji pombe kupita kiasi
  • Kutofanya mazoezi kabisa
  • Fetma (obesity)
  • Kuwa na cholesterol nyingi kwenye damu
  • Atrial fibrillation
Matibabu
Matibabu ya kiharusi hutegemea pia aina na visababishi vyake .
1. Matibabu ya kiharusi kinachotokana na ubongo kukosa hewa (Ischemic stroke)

Mgonjwa hutibiwa kwa kutumia dawa za kuyeyusha damu iliyoganda (thrombolytics) au kwa kuondoa damu iliyoganda kwa njia mbalimbali (thrombectomy). Dawa nyingine kama vile junior Aspirin na Clopidogrel hutolewa kwa ajili ya kuzuia chembe sahani kukusanyika na kuganda.
2. Matibabu ya kiharusi kinachotokana na damu kuvujia kwenye ubongo (Hemorrhagic stroke)

Aina hii ya kiharusi huitaji tathmini ya upasuaji wa neva ili kuchunguza na kutibu sababu ya damu kuvuja.Angalizo: ni hatari kumpa mgonjwa wa aina hii ya kiharusi dawa za kuyeyusha damu iliyoganda au za kuzuia kuganda maana uhatarisha maisha ya mgonjwa badal ya kumsaidia. Kwahiyo ni vizuri kwa wataalamu kufanya ufanya uchunguzi wa kutosha ili kuwa na uhakika na tatizo.
Huduma na Matunzo kwa mgonjwa wa Kiharusi
Mojawapo ya mambo muhimu ya kufanya kwa mgonjwa aliyepata kiharusi ni kumuongoza na kumuelimisha ili arudishe ujuzi wake wa maisha ya kila siku. Hapa uhitaji ushirikiano wa wauguzi, wataalamu wa viungo, wataalamu wa ushauri wa kazi na daktari. Kuna umuhimu pia wa kuwaelimisha ndugu kuhusu hali ya mgonjwa ili waweze kumsaidia katika matunzo yake nyumbani na kwenye jamii inayomzunguka.
Matarajio (prognosis)

Asilimia 75 ya wagonjwa wa kiharusi wanaonusurika kifo huwa walemavu na kusababisha kuathirika kwa ufanyaji kazi wao na kuajiriwa. Ulemavu unaweza kuwa wa kimwili au kiakili au vyote kwa pamoja.
Ulemavu wa kimwili ni pamoja na

  • Ulegevu wa misuli
  • Kujihisi ganzi sehemu mbalimbali za mwili hususani zilizoathirika
  • Kujikojolea
  • Kutoona vizuri
  • Kushindwa kuendelea na shughuli za kila siku
  • Vichomi
  • Vidonda shinikizo
  • Kukosa hamu ya chakula.
Ulemavu wa akili hujumuisha vitu kama

  • Mgonjwa kuwa na wasiwasi
  • Hofu ya mashambulizi, na
  • Unyongovu.
Jinsi ya kuzuia kiharusi

  • Zuia au tibu shinikizo la damu
  • Dhibiti kisukari
  • Fanya mazoezi
  • Acha kuvuta sigara
  • Punguza uzito
  • Acha kunywa pombe kupita kiasi
  • Tumia Junior Aspirin
  • Kula chakula kisichokuwa na mengi na kisicho na chumvi nyingi.
  • Tumia dawa za kupunguza mafuta mwilini (statins)kwa mfano Simvastatin

Mkuu.@
Logik Ukitaka dawa ya maradhi ya kiharusi nitumie barua ya Pepe Email Address yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com
 
JF Doctors naomba mnifahamishe;
Ugonjwa wa KIHARUSI ni ugonjwa wa aina gani?,unasababishwa na nini?Na dalili zake ni zipi na mwisho kabsa naomba nisaidieni kama una tiba
 
KULA NYANYA UJIEPUSHE NA KIHARUSI

  • SOTE tunajua ugonjwa wa kiharusi (stroke) ni miongoni mwa magonjwa hatari kwani ukikupata unaweza kudhoofisha baadhi ya viungo vyako vya mwili kama siyo vyote na kukufanya ushindwe kufanya kazi zako za kawaida na kuwa mtu wa ndani tu kwa maisha yako yote.
Lakini unaweza kujiepusha na ugonjwa huo hatari kwa kuzingatia ulaji wa vyakula sahihi pamoja na kufanya mazoezi. Utafiti wa hivi karibuni umebaini kwamba nyanya (tomatoes) hutoa kinga mwilini dhidi ya ugonjwa wa kiharusi au kupooza kama unavyojulikana na wengine.
Hivi karibuni, watafiti wa nchini Finland walifanya utafiti wa kina na kutoa taarifa kuhusu kirutubisho aina ya ‘lycopene’ kinachopatikana kwa wingi kwenye nyanya, matikitimaji na pilipili. Wamesema katika taarifa yao kuwa watu zaidi ya 1,000 waliowafanyia utafiti wenye kiwango kingi cha ‘lycopene’ kwenye mfumo wa damu zao, hawakuonesha dalili kabisa za kupatwa na kiharusi.
Aidha, Chama cha Taifa cha wenye Kiharusi cha nchini Marekani (The National Stroke Association) kimesema kuwa wanawake wengi hufariki dunia nchini humo kutokana na kiharusi kwa idadi sawa na wale wanaofariki kutokana na ugonjwa wa saratani ya matiti. Hii ina maana kwamba ugonjwa wa kiharusi nao ni tishio kama ilivyo kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.
Utafiti mwingine katika eneo hilo umeonesha pia kuwa wanaume wana hatari kubwa zaidi ya kufariki dunia au kupatwa na matatizo mengi kutokana na ugonjwa wa kiharusi kuliko wanawake. Hivyo kati ya wanaume na wanawake, wanaume zaidi ndiyo hupatwa na kiharusi au matatizo yatokanayo na ugonjwa huo kuliko wanawake.

Utafiti huu mpya umeendelea kuthibitisha ukweli wa siku zote kuwa matunda na mbogamboga hutoa kinga katika mwili wa binadamu dhidi ya magonjwa mengi hatari, hivyo wito umetolewa tena wa watu kupenda kula matunda na mbogamboga hasa nyanya, matikitimaji pamoja na pilipili ambavyo vimeonekana kuwa na kinga kubwa zaidi mwilini.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa baada ya matokeo ya utafiti huu, watu wamekumbushwa umuhimu wa kuendelea kula na aina nyingine ya matunda, kwani kila tunda au mboga ya majani ina faida na umuhimu wake katika mwili wa binadamu.
Mwisho imeelezwa kuwa ulaji wa nyanya za aina zote una faida, iwe ni ile inayopikwa pamoja na mboga au ile inayoliwa ikiwa imeiva bila kupikwa. Ni vizuri kuchangamkia ulaji wa vitu kama hivi ili kuipa miili yetu uwezo wa kujikinga wenyewe dhidi ya maradhi hatari, yakiwemo yale ya saratani ambayo kwa kiasi kikubwa huweza kuzuiwa kwa kula mboga za majani na matunda ya aina mbalimbali.
KULA NYANYA UJIEPUSHE NA KIHARUSI - Global Publishers

Habari zenu wakuu,
Nina mama yangu amepata strock. Hapo awali alikuwa akisumbuliwa na presha kwa muda mrefu. Kwenye mnamo mwezi wa nne wa mwaka jana ghafla tu aliamka asubuhi vidole vya mkono wa kulia vikawa vigumu kukunjika. Siku tatu baadaye hali ikazidi kubadilika kwani mkono pamoja na mguu wa kulia vyote vikawa havifanyi kazi kabisa. Siku kama mbili baadaye akazidiwa usiku. Tukaamua tumpeleke hospitali ambako madaktari eti wakasema ana malaria wadudu sita. Ndugu walio kijijini wakamtaka mgonjwa ili wakamtibie wao huku wakisema eti ugonjwa siyo wa hospital inatakiwa atibiwe kwa miti shamba na siyo sindano.

Kweli mgonjwa tukampeleka kijijini. Alikaa huko kuanzia mwezi wa nne hadi wa wa kumi na moja ndo akarudi Dar. Hali yake kidogo ilikuwa nzuri kwani anaweza kutembea japo siyo kama zamani ( anatembea ule mwendo wa kupapalalazi ). Anajitahidi kukimbia japo siyo kwa urahisi. Ulimi haujampinda. Anaongea vizuri tu japo zamani kabla hajaenda kijijini kuna wakati ulianza kumpinda.

Sasa tatizo liko hapa, ndiyo bado anaendelea kutumia dawa za mitishamba hdai sasa, lakini mara nyingi kichwa na presha huwa vinamsumbua sana. Kuna siku anakuwa fresh tu, ila kuna siku anasumbuliwa na kichwa na siku nyingine presha. Lakini pia kubwa zaidi ni GANZI kwenye miguu. Miguu yake huwa inashika ganzi hadi anahisi kama inachomachoma.

Ndugu zangu, kwa mwenye kujua chochote ambacho kitaweza kumsaidia mama yangu naomba anisaidie. Kama unajua dawa nitakushukuru sana. Au kama una wazo lolote liweke huru. Jamani mama yangu anateseka.
 
pole sana mkuu,.

Vuta subira wataalam wanakuja kukusaidia!
 
Huyu Mama Ana Chronic Hypertension With Neuropathy!!!! Naomba nilaani kitendo chenu cha kukimbilia miti shamba tena kwa miez 7 hii ime worsen situation.

Huyu Mama anatakiwa apigwe dose za PRESHA, anatakiwa apate dawa za Preshaa ilishushwe na iwe sawa siku zote, pia anatakiwa apate dawa za mishipa kuua ganzi, pia Afanye CT scan!

apate DAWA ZA PRESHA, APATE NEUROBION, NA JUNIOR ASPIRIN atapona, Pia apime na sukari
 
hospitali kamwe huwezi kupona presha labda itashuka tu kidogo na kujirudia tena mpaka utakapokufa nayo, ukitaka kupona presha waone tiba mubadala. Ili apone strock/kiharusi utatakiwa kumponya kwanza presha, ukihitaji dawa nitumie PM.
 
Habari zenu wakuu,
Nina mama yangu amepata strock. Hapo awali alikuwa akisumbuliwa na presha kwa muda mrefu. Kwenye mnamo mwezi wa nne wa mwaka jana ghafla tu aliamka asubuhi vidole vya mkono wa kulia vikawa vigumu kukunjika. Siku tatu baadaye hali ikazidi kubadilika kwani mkono pamoja na mguu wa kulia vyote vikawa havifanyi kazi kabisa. Siku kama mbili baadaye akazidiwa usiku. Tukaamua tumpeleke hospitali ambako madaktari eti wakasema ana malaria wadudu sita. Ndugu walio kijijini wakamtaka mgonjwa ili wakamtibie wao huku wakisema eti ugonjwa siyo wa hospital inatakiwa atibiwe kwa miti shamba na siyo sindano.

Kweli mgonjwa tukampeleka kijijini. Alikaa huko kuanzia mwezi wa nne hadi wa wa kumi na moja ndo akarudi Dar. Hali yake kidogo ilikuwa nzuri kwani anaweza kutembea japo siyo kama zamani ( anatembea ule mwendo wa kupapalalazi ). Anajitahidi kukimbia japo siyo kwa urahisi. Ulimi haujampinda. Anaongea vizuri tu japo zamani kabla hajaenda kijijini kuna wakati ulianza kumpinda.

Sasa tatizo liko hapa, ndiyo bado anaendelea kutumia dawa za mitishamba hdai sasa, lakini mara nyingi kichwa na presha huwa vinamsumbua sana. Kuna siku anakuwa fresh tu, ila kuna siku anasumbuliwa na kichwa na siku nyingine presha. Lakini pia kubwa zaidi ni GANZI kwenye miguu. Miguu yake huwa inashika ganzi hadi anahisi kama inachomachoma.

Ndugu zangu, kwa mwenye kujua chochote ambacho kitaweza kumsaidia mama yangu naomba anisaidie. Kama unajua dawa nitakushukuru sana. Au kama una wazo lolote liweke huru. Jamani mama yangu anateseka.

Presha, Stroke au Kiharusi n.k kwa ujumla wake yanajulikana kitaalamu kama Noncommunicable Diseases NCD, ni magonjwa ya mfumo, WHO wanasema yanaongoza kwa vifo duniani kwa asilimia 65, lakini yanaepukika na kutibika kwa kuanza kurekebisha mfumo ulioathirika.

Noncommunicable diseases (NCDs), such as heart disease, stroke, cancer, chronic respiratory diseases and diabetes, are the leading cause of mortality in the world.
This invisible epidemic is an under-appreciated cause of poverty and hinders the economic development of many countries.
The burden is growing - the number of people, families and communities afflicted is increasing. Common, modifiable risk factors underlie the major NCDs. They include tobacco, harmful use of alcohol, unhealthy diet, insufficient physical activity, overweight/obesity, raised blood pressure, raised blood sugar and raised cholesterol.
The NCD threat can be overcome using existing knowledge. The solutions are highly cost-effective. Comprehensive and integrated action at country level, led by governments, is the means to achieve success

FUATILIA LINK HII kwa taarifa zaidi au tuwasiliane 0784475576 ili upate mbinu zaidi na jinsi ya kurekebisha mfumo ulioathirika.
Thanks.
 
Huyu Mama Ana Chronic Hypertension With Neuropathy!!!! Naomba nilaani kitendo chenu cha kukimbilia miti shamba tena kwa miez 7 hii ime worsen situation.

Huyu Mama anatakiwa apigwe dose za PRESHA, anatakiwa apate dawa za Preshaa ilishushwe na iwe sawa siku zote, pia anatakiwa apate dawa za mishipa kuua ganzi, pia Afanye CT scan!

apate DAWA ZA PRESHA, APATE NEUROBION, NA JUNIOR ASPIRIN atapona, Pia apime na sukari

Nimekuelewa mkuu, ubarikiwe sana
 
Presha, Stroke au Kiharusi n.k kwa ujumla wake yanajulikana kitaalamu kama Noncommunicable Diseases NCD, ni magonjwa ya mfumo, WHO wanasema yanaongoza kwa vifo duniani kwa asilimia 65, lakini yanaepukika na kutibika kwa kuanza kurekebisha mfumo ulioathirika.

Noncommunicable diseases (NCDs), such as heart disease, stroke, cancer, chronic respiratory diseases and diabetes, are the leading cause of mortality in the world.
This invisible epidemic is an under-appreciated cause of poverty and hinders the economic development of many countries.
The burden is growing - the number of people, families and communities afflicted is increasing. Common, modifiable risk factors underlie the major NCDs. They include tobacco, harmful use of alcohol, unhealthy diet, insufficient physical activity, overweight/obesity, raised blood pressure, raised blood sugar and raised cholesterol.
The NCD threat can be overcome using existing knowledge. The solutions are highly cost-effective. Comprehensive and integrated action at country level, led by governments, is the means to achieve success

FUATILIA LINK HII kwa taarifa zaidi au tuwasiliane 0784475576 ili upate mbinu zaidi na jinsi ya kurekebisha mfumo ulioathirika.
Thanks.

ahsante mkuu
 
Habari zenu wakuu,
Nina mama yangu amepata strock. Hapo awali alikuwa akisumbuliwa na presha kwa muda mrefu. Kwenye mnamo mwezi wa nne wa mwaka jana ghafla tu aliamka asubuhi vidole vya mkono wa kulia vikawa vigumu kukunjika. Siku tatu baadaye hali ikazidi kubadilika kwani mkono pamoja na mguu wa kulia vyote vikawa havifanyi kazi kabisa. Siku kama mbili baadaye akazidiwa usiku. Tukaamua tumpeleke hospitali ambako madaktari eti wakasema ana malaria wadudu sita. Ndugu walio kijijini wakamtaka mgonjwa ili wakamtibie wao huku wakisema eti ugonjwa siyo wa hospital inatakiwa atibiwe kwa miti shamba na siyo sindano.

Kweli mgonjwa tukampeleka kijijini. Alikaa huko kuanzia mwezi wa nne hadi wa wa kumi na moja ndo akarudi Dar. Hali yake kidogo ilikuwa nzuri kwani anaweza kutembea japo siyo kama zamani ( anatembea ule mwendo wa kupapalalazi ). Anajitahidi kukimbia japo siyo kwa urahisi. Ulimi haujampinda. Anaongea vizuri tu japo zamani kabla hajaenda kijijini kuna wakati ulianza kumpinda.

Sasa tatizo liko hapa, ndiyo bado anaendelea kutumia dawa za mitishamba hdai sasa, lakini mara nyingi kichwa na presha huwa vinamsumbua sana. Kuna siku anakuwa fresh tu, ila kuna siku anasumbuliwa na kichwa na siku nyingine presha. Lakini pia kubwa zaidi ni GANZI kwenye miguu. Miguu yake huwa inashika ganzi hadi anahisi kama inachomachoma.

Ndugu zangu, kwa mwenye kujua chochote ambacho kitaweza kumsaidia mama yangu naomba anisaidie. Kama unajua dawa nitakushukuru sana. Au kama una wazo lolote liweke huru. Jamani mama yangu anateseka.
Pole sana Wasiliana na mimi kwa njia ya Email yangu Address hii hapa fewgoodman@hotmail.com ninaweza kumtibu na akapona kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu.
 
Maradhi ya kiharusi (stroke)

Maana ya Kiharusi

webmd_rm_illustration_of_stroke_causes_.jpg

What Is a Stroke?

Stroke is a medical emergency and a leading cause of death in the U.S. It occurs when a blood vessel in the brain bursts or, more commonly, when a blockage develops. Without treatment, cells in the brain quickly begin to die. The result can be serious disability or death. If a loved one is having stroke symptoms, seek emergency medical attention without delay.

getty_rm_illustration_of_stroke.jpg

Stroke Symptoms

Signs of a stroke may include:

  • Sudden numbness or weakness of the body, especially on one side.
  • Sudden vision changes in one or both eyes, or difficulty swallowing.
  • Sudden, severe headache with unknown cause.
  • Sudden problems with dizziness, walking, or balance.
  • Sudden confusion, difficulty speaking or understanding others.

Call 911 immediately if you notice any of these symptoms.

phototake_rm_photo_of_brain_damage_from_stroke.jpg

Stroke: Time = Brain Damage

Every second counts when seeking treatment for a stroke. When deprived of oxygen, brain cells begin dying within minutes. There are clot-busting drugs that can curb brain damage, but they have

to be used within three hours of the initial stroke symptoms. Once brain tissue has died, the body parts controlled by that area won't work properly. This is why stroke is a top cause of long-term disability.

MARADHI YA KIHARUSI:

Kiharusi ni hali inayotokea pale mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo inapopatwa na misukosuko kiasi cha kushindwa kupeleka damu kwenye ubongo na hivyo kuathiri ufanyaji kazi wa ubongo kwa zaidi ya masaa 24.

Kulingana na shirika la afya duniani kiharusi ni nakisi katika neva ambayo hutokana na tatizo katika mishipa ya damu ya ubongo na ambalo huendelea zaidi ya masaa 24 au kukoma ndani ya masaa 24. Muda wa masaa 24 umechukuliwa ili kutofautisha kiharusi na kiharusi cha kukosa oksijeni katika ubongo (ischemia) ambacho hutokea na kudumu kwa muda mfupi yaani (transient ischemic attack).

Kwa kawaida dalili za TIA hupotea na mtu kurudia hali yake ya kawaida ndani ya masaa 24.

Aina za kiharusi

Kiharusi kimegawanyika katika aina kuu mbili kulingana na jinsi kinavyotokea (visababishi vyake). Aina hizo ni

1. Kiharusi cha kukosa hewa kwenye Ubongo (Ischemic stroke)

Aina hii ya kiharusi hutokea iwapo usambazaji wa damu katika sehemu ya ubongo hupungua na kupelekea tishu za ubongo za eneo liliathirika kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

Aina hii ya kiharusi husababishwa na nini?

Aina hii ya kiharusi husababishwa na

Damu iliyoganda kuziba mishipa midogo ndani ya ubongo (cerebral thrombosis) au
Kipande cha damu kumeguka na kwenda kuziba mshipa wa damu kwenye ubongo(cerebral embolism)

Kupungua kwa usambazaji wa damu kwa ujumla kwa mfano shock.
Vena thrombosis

2. Kiharusi cha kuvuja damu ndani ya Ubongo (Haemorrhagic Stroke)

Aina hii ya kiharusi hutokea pale ambapo mishipa midogo ya damu ndani ya ubongo hupasuka na kusababisha kusambaa kwa damu ubongoni (cerebral hemorrhage). Mara nyingi aina hii ya kiharusi hutanguliwa na dalili za kichwa kuuma, au kuwepo kwa historia ya ajali ya kichwa.

Visababishi vya Kiharusi (kwa ujumla)

Wakati fulani, mishipa ya damu huzungukwa na aina fulani za mafuta yasiyofaa mwili, hali inayoitwa kitaalamu kama atherosclerotic plaque. Hali hii husababisha kuganda kwa damu katika

mishipa (thrombosis) hiyo. Kuganda huku kwa damu kunaweza kutokea kwenye mishipa mikubwa au midogo inayopeleka damu kwenye ubongo. Baadhi ya mishipa mikubwa ya damu inayoweza

kuathirika na tatizo hili ni pamoja na arteri za common carotid na interior carotid arteries, na arteri za vertebral. Nyingine ni mishipa midogo inayounda eneo linaloitwa circle of willis lililo katika ubongo.

Kuganda kwa chembe nyekundu za damu za mgojwa wa sickle cell kunaweza pia kusababisha kuziba mishipa ya damu hivyo kusababisha Kiharusi.

Kuganda kwa damu (embolus) kwenye mishipa ya damu ya sehemu nyingine za mwili au (hewa, mafuta, kusanyiko la vijimelea kama bakteria waletao ugonjwa wa endocarditis) huweza

kusababisha kuziba kwa mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo kusababisha kiharusi.

Upungufu wa usafirishaji damu mwilini (systemic hypoperfusion) - Wakati fulani moyo hushindwa kusukuma damu vizuri kwenda sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo ubongo kutokana na kufa kwa

sehemu za nyama ya moyo kwa kukosa damu ya kutosha (Ischaemic Heart Diseases) au kutokana na kujaa kwa maji kwenye gamba lake la nje (pericardial effusion) au kupungua kwa damu mwilini,

kunakoweza kusababishwa na mambo kadhaa. Hali hii husababisha sehemu kubwa ya mwili ikiwemo ubongo kukosa oksijeni ya kutosha na kusababisha kuathiriwa kwa sehemu ya ubongo.

Shinikizo la damu la muda mrefu lisilothibitiwa linaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa midogo inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo damu kujaa kwenye ubongo (Intracerebral hemorrhage).

Dalili za kiharusi

Dalili za kiharusi hutegemea na eneo la ubongo liliathiriwa.

Iwapo sehemu ya ubongo mkubwa ( Cerebellum) itaadhirika, mgonjwa atakuwa na dalili kama kushindwa kutembea vizuri, hivyo kuathiri mwendo wake, kujihisi kizunguzungu na pia kutapika.

Iwapo sehemu ya ubongo wa kati (cerebral cortex) itakuwa imeathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za kushindwa kuongea,kushindwa kuelewa lugha inayozungumzwa, kushindwa kuona vizuri, kuwa

na ukosefu wa kumbukumbu, kuwa na mvurugiko wa mpangilio wakw wa kufikiri, kuchanganyikiwa, na kubadilika kwa mwendo wa harakati za hiari.

Iwapo mgonjwa ataadhirika sehemu ya ubongo kwenye shingo kuelekea kwenye uti wa mgongo (brain stem), mgonjwa anaweza kuwa na dalili za kuhisi mabadiliko ya harufu, ladha, kusikia na

kuona; kulegea kwa misuli ya macho (ptosis); kupungua kwa ufahamu na kulegea kwa misuli ya uso; Ulegevu wa Ulimi (kushindwa kutoa nje au kusogeza upande upande); kupungua uwezo wa

kumeza; ulegevu wa misuli ya shingo na kushindwa kugeuza shingo upande mmoja; kushindwa kusimama sawasawa na kuona vitu kwa hali ya utofauti; mabadiliko ya upumuaji na kiwango cha moyo kudunda.

Iwapo sehemu mojawapo ya mfumo mkuu wa neva (central nervous system) imeathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za kupoteza ufahamu kwa upande mmoja wa mwili na kulegea kwa misuli ya uso, kuhisi ganzi mwilini, na kupungua kwa ufahamu wa hisia na hisia mtetemo.

Aidha bila kujalisha eneo lililoathiriwa, mgonjwa pia anaweza kuwa na dalili za kupoteza fahamu, maumivu makali ya kichwa na kutapika. Dalili hizi za kuumwa kichwa na kutapika kwa kawaida

hutokea kwa mgonjwa mwenye kiharusi cha kuvuja damu (hemorrhagic stroke) ambacho husababisha ongezeko la shinikizo na mgandamizo wa ubongo ndani ya fuvu kutokana na kuvuja kwa damu.

Vipimo

Mionzi
CT-scan
MRI
PET
SPECT
Vipimo vingine ni;

ECG, ECHOCARDIOGRAM huwezesha kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia) na kama kuna damu iliyoganda kwenye moyo ambayo inaweza kufika kwenye ubongo

Holter monitor husaidia kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia) zinazotokea kwa vipindi

Angiogram huwezesha kugundua matatizo kwenye mishipa ya damu, na ni mishipa ipi ya damu iliyoziba.
Vipimo vya damu huwezesha kutambua uwepo wa lijamu mwilini (hypercholesterolemia) na mabadiliko mengine katika damu
Vihatarishi vya kiharusi

Vitu vinavyoweza kumuweka mtu katika hatari ya kupata kiharusi ni pamoja na

Shinikizo la damu lisilothibitiwa
Kisukari
Uvutaji sigara
Unywaji pombe kupita kiasi
Kutofanya mazoezi kabisa
Fetma (obesity)
Kuwa na cholesterol nyingi kwenye damu
Atrial fibrillation
Matibabu

Matibabu ya kiharusi hutegemea pia aina na visababishi vyake .

1. Matibabu ya kiharusi kinachotokana na ubongo kukosa hewa (Ischemic stroke)

Mgonjwa hutibiwa kwa kutumia dawa za kuyeyusha damu iliyoganda (thrombolytics) au kwa kuondoa damu iliyoganda kwa njia mbalimbali (thrombectomy). Dawa nyingine kama vile junior Aspirin na Clopidogrel hutolewa kwa ajili ya kuzuia chembe sahani kukusanyika na kuganda.

2. Matibabu ya kiharusi kinachotokana na damu kuvujia kwenye ubongo (Hemorrhagic stroke)

Aina hii ya kiharusi huitaji tathmini ya upasuaji wa neva ili kuchunguza na kutibu sababu ya damu kuvuja. Angalizo: ni hatari kumpa mgonjwa wa aina hii ya kiharusi dawa za kuyeyusha damu

iliyoganda au za kuzuia kuganda maana uhatarisha maisha ya mgonjwa badal ya kumsaidia. Kwahiyo ni vizuri kwa wataalamu kufanya ufanya uchunguzi wa kutosha ili kuwa na uhakika na tatizo.

Huduma na Matunzo kwa mgonjwa wa Kiharusi

Mojawapo ya mambo muhimu ya kufanya kwa mgonjwa aliyepata kiharusi ni kumuongoza na kumuelimisha ili arudishe ujuzi wake wa maisha ya kila siku. Hapa uhitaji ushirikiano wa wauguzi,

wataalamu wa viungo, wataalamu wa ushauri wa kazi na daktari. Kuna umuhimu pia wa kuwaelimisha ndugu kuhusu hali ya mgonjwa ili waweze kumsaidia katika matunzo yake nyumbani na kwenye jamii inayomzunguka.

Matarajio (prognosis)

Asilimia 75 ya wagonjwa wa kiharusi wanaonusurika kifo huwa walemavu na kusababisha kuathirika kwa ufanyaji kazi wao na kuajiriwa. Ulemavu unaweza kuwa wa kimwili au kiakili au vyote kwa pamoja.

Ulemavu wa kimwili ni pamoja na

Ulegevu wa misuli
Kujihisi ganzi sehemu mbalimbali za mwili hususani zilizoathirika
Kujikojolea
Kutoona vizuri
Kushindwa kuendelea na shughuli za kila siku
Vichomi
Vidonda shinikizo
Kukosa hamu ya chakula.
Ulemavu wa akili hujumuisha vitu kama

Mgonjwa kuwa na wasiwasi
Hofu ya mashambulizi, na
Unyongovu.
Jinsi ya kuzuia kiharusi

Zuia au tibu shinikizo la damu
Dhibiti kisukari
Fanya mazoezi
Acha kuvuta sigara
Punguza uzito
Acha kunywa pombe kupita kiasi
Tumia Junior Aspirin
Kula chakula kisichokuwa na mengi na kisicho na chumvi nyingi.
Tumia dawa za kupunguza mafuta mwilini (statins)kwa mfano Simvastatin
 
Habari zenu wakuu,
Nina mama yangu amepata strock. Hapo awali alikuwa akisumbuliwa na presha kwa muda mrefu. Kwenye mnamo mwezi wa nne wa mwaka jana ghafla tu aliamka asubuhi vidole vya mkono wa kulia vikawa vigumu kukunjika. Siku tatu baadaye hali ikazidi kubadilika kwani mkono pamoja na mguu wa kulia vyote vikawa havifanyi kazi kabisa. Siku kama mbili baadaye akazidiwa usiku. Tukaamua tumpeleke hospitali ambako madaktari eti wakasema ana malaria wadudu sita. Ndugu walio kijijini wakamtaka mgonjwa ili wakamtibie wao huku wakisema eti ugonjwa siyo wa hospital inatakiwa atibiwe kwa miti shamba na siyo sindano.

Kweli mgonjwa tukampeleka kijijini. Alikaa huko kuanzia mwezi wa nne hadi wa wa kumi na moja ndo akarudi Dar. Hali yake kidogo ilikuwa nzuri kwani anaweza kutembea japo siyo kama zamani ( anatembea ule mwendo wa kupapalalazi ). Anajitahidi kukimbia japo siyo kwa urahisi. Ulimi haujampinda. Anaongea vizuri tu japo zamani kabla hajaenda kijijini kuna wakati ulianza kumpinda.

Sasa tatizo liko hapa, ndiyo bado anaendelea kutumia dawa za mitishamba hdai sasa, lakini mara nyingi kichwa na presha huwa vinamsumbua sana. Kuna siku anakuwa fresh tu, ila kuna siku anasumbuliwa na kichwa na siku nyingine presha. Lakini pia kubwa zaidi ni GANZI kwenye miguu. Miguu yake huwa inashika ganzi hadi anahisi kama inachomachoma.

Ndugu zangu, kwa mwenye kujua chochote ambacho kitaweza kumsaidia mama yangu naomba anisaidie. Kama unajua dawa nitakushukuru sana. Au kama una wazo lolote liweke huru. Jamani mama yangu anateseka.
Mimi ninakusaidia kuhusu

hiyo miguu kufa Ganzi kamnunulie mama yako Dawa ya Vidonge inayoitwa

kwa jina hili (Vitamin B12) itamsaidia kutibu hiyo ganzi miguuni mwake na pia ukikosa hiyo (Vitamin B12) waweza pia kununuwa Dawa hii hapa (Neurobion Tablets) pia ni dawa ya kutibu Ganzi ya miguu pia mpeleke akapime Ugonjwa wa

kisukari Hospitalini. Na awe anapenda kunywa sana Maji ya Uvuguvugu kila siku kwa wingi sana. Je hiyo Presha yake

mam ni ya kupanda au Presha ya kushuka?
 
ni ya kupanda
 
Back
Top Bottom