Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Ikiwa Rais akifanya madudu makubwa kama vile kuvunja katiba, kuwasababishia wananchi madhara kwa sababu tu ya ubinafsi wake au kikundi chake kidogo cha kifisadi, siyo tu anatakiwa ashtakiwe baada ya kustaafu bali pia anatakiwa aondolewe madarakani hata kabla ya muda wake na mashtaka kuanza mara moja.
Mtazamo huu ni mzuri kwa mustakabali wa vizazi vijavyo. Ni haki ya msingi ya wananchi kuondoa utawala mbovu ama kwa njia ya kisheria na ikishindikana basi nguvu itumike inapobidi.
 
JAJI mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Raymond Mwaikasu, amewataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuondoa kinga inayomlinda rais wakati anapostaafu ili aweze kufikishwa mahakamani pindi inapobainika amevunja katiba wakati wa utawala wake.

Jaji Mwaikasu alitoa wito huo jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na viongozi wa dini walipokutana kujadili mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma.

Alisema kuondolewa kwa kinga hiyo kutasaidia kudhibiti baadhi ya watu wanaotarajia kuingia madarakani kwa ajili ya kujinufaisha binafsi badala ya kulinda katiba.

Chanzo: Tanzania Daima la 27/3/2014

Na hasa HUYU aliyepo sasa hivi madarakani....ni tatizo kuu na nchi kuvurugika na kuelekea kukosa Katiba bora inayomlinda kila raia na urithi aliopewa na Muumba wake...hadi anajionyesha wazi na kujitoa kabisa mawazo (RASIMU) ya watanzania wote zaidi ya 61% waliojitoa kwa tanganyika mpya, na yeye kupinga ili kujinufaisha binafsi na kundi la chama chake kilichojaa wezi na majangili? Hakuna kinga tena...! Ni mahakama ndiyo inawafaaa kuwaadabisha viongozi kama hawa! period.
 
Naunga mkono hoja 100%. Akiondolewa hii kinga atafikiri mara mbili kabla ya kufanya ufisadi; kumuwekea kinga ni sawa na kumruhusu kufanya ufisadi bila woga!!!!
 
JAJI mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Raymond Mwaikasu, amewataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuondoa kinga inayomlinda rais wakati anapostaafu ili aweze kufikishwa mahakamani pindi inapobainika amevunja katiba wakati wa utawala wake.

Jaji Mwaikasu alitoa wito huo jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na viongozi wa dini walipokutana kujadili mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma.

Alisema kuondolewa kwa kinga hiyo kutasaidia kudhibiti baadhi ya watu wanaotarajia kuingia madarakani kwa ajili ya kujinufaisha binafsi badala ya kulinda katiba.

Chanzo: Tanzania Daima la 27/3/2014
itakuwa safi sana!
 
Kwanza hata hili swala la kiongozi kuwa na kinga ya kushitakiwa ni sheria ya kipuuuzi kuliko sheria nyingine yoyote. wewe ni nani ufanye utakalo bila kufanywa chochote? tena ukizingatia wewe n ikiongozi mkuu wa nchi, na hzi sheria za kipuuzi ndizo zinazo sababisha hawa mabwana wakubwa kujisahau na kulopoka utumbo ambao unaweza kusababisha vurugu kubwa, kama "wapingwe tu" Ohhh CCM wamechoka uvumilivu"...hili swala la kutoa kinga lilitakiwa lifanyiwe marekebosho ata kesho bila hata kusubiri katiba mpya
 
sasa mkuu huoni kumwajimbisha akiwa madarakani ndio jambo jema zaidi kuliko akiondoka??
 
Kwanza hata hili swala la kiongozi kuwa na kinga ya kushitakiwa ni sheria ya kipuuuzi kuliko sheria nyingine yoyote. wewe ni nani ufanye utakalo bila kufanywa chochote? tena ukizingatia wewe n ikiongozi mkuu wa nchi, na hzi sheria za kipuuzi ndizo zinazo sababisha hawa mabwana wakubwa kujisahau na kulopoka utumbo ambao unaweza kusababisha vurugu kubwa, kama "wapingwe tu" Ohhh CCM wamechoka uvumilivu"...hili swala la kutoa kinga lilitakiwa lifanyiwe marekebosho ata kesho bila hata kusubiri katiba mpya

mkuu sheria kama hiyo si upuuzi ni katika kujaribu kuipa heshima taasisi ya Urais, kwa maana kwamba Rais ndiyo ofisi kubwa kabisa na yenye mamlaka nchini, hivyo ni matumaini ya wengi kwamba anayeshika hiyo ofisi ni mtu mwenye maadili na anayesheshimika katika jamii, hivyo kulinda heshima ya ofisi hiyo na kumpa aliyeshika ofisi hiyo muda mzuri wa kuwatumikia wananchi, kupunguza mianya ya kumshtaki mara kwa mara mahakamani, kwani mwenye ofisi anaweza kuwa busy na kesi mahakamani akashindwa kutimiza wajibu wake vyema, ofisi ya rais kutokana na majukumu yake kwa wananchi ipo katika nafasi ya kupata mashitak amengi kutokana na kuhusika kwake moja kwa moja kwa mambo yanayowagusa wananchi kisiasa, kutoa mwanya wa kushitakika kutafungua nafasi kwa mashitaka mengi mengine yasiyo na lazima kuyafungua na kusababisha utendaji wa ofisi namba moja kupungua kwa kiasi kikubwa
 
Ila mara tu baada ya kutoka ofisini(kuachia ofisi) anyooke moja kwa moja kortini kujibu tuhuma.
 
Kwa mujibu wa katiba yetu,raisi wa nchi hawezi kushitakiwa akiwa madarakani na hata baada ya kustaafu kwa makosa atakayoyafanya akiwa madarakani.Kipengele cha ajabu kabisa hiki.

Kinachonishangaza na kunisikitisha ni kuona nguvu na juhudi ndogo sana inayoelekezwa katika kudai mabadiliko ya kipengele hiki cha katiba.

Si UKAWA,si Warioba na tume yake,si wanaharakati, wala makundi mengine ya kijamii yanayoonekana kushikia bango mabadiliko haya.

Kila siku ni muundo wa serikali,tunu za taifa,miiko ya uongozi,n.k.Lakini kipengele hiki kinacholitafuna taifa kinaonekana kusahaulika.

Nafikiri wakati umefika tubadilike na endapo mwakani tutapata wabunge wengi wa UKAWA,basi mmoja wao apeleke hoja binafsi bungeni akilenga kukifanyia marekebisho kipengele hiki na ikiwezekana hata hawa maraisi waliopita washitakiwe endapo itabainika wanastahili kushitakiwa.

Ni ajabu nchi tajiri maraisi wanashitakiwa alafu sisi nchi "ombaomba" eti raisi ni "mungu mtu" huku kila siku viongozi hao wanatuhumiwa kwa ufisadi!!

Bila kufanya hivyo,tutaendelea kulia na ufisadi usioisha na kuna siku "mwehu" ataingia Ikulu na kuuza sehemu ya nchi hii na mtashindwa kumshitaki popote.
 
Huyu jamaa nae hayuko sawa,unataka watu waanze kung'ang'ania madaraka?
 
Tungekuwa na katiba bora JK asingemaliza hii term yake ya pili, ameidhalilisha sana Ikulu na nafasi ya Urais.
 
Back
Top Bottom