Ukweli ni kuwa kama siyo sheria kunibana basi ningekuwa nimeshafungua kesi kadhaa dhidi ya rais Magufuli kutokana na mwenendo wa matamko yake.
Kwanza nikiri kuwa yapo maeneo machache ambayo rais anafanya vizuri kama mkuu wa nchi na eneo hilo ni nidhamu ya kazi ingawa imechangishwa na uoga hivyo kukosa matokeo chanya kwa kiwango kikubwa juu ya ukuaji wa uchumi. Lakini kwa ukweli ulio mchungu kabisa, rais Magufuli kama ataendelea hivi basi huenda akawa ni rais wa bahati mbaya kabisa kwa nchi kuwahi kuwa naye na mbaya zaidi huenda hadi mwaka 2020 tukajikuta tuna taifa lenye taswira tofauti kabisa na wengi wetu wakabaki wakijiuliza kulikoni?
Kauli nyingi sana za rais Magufuli zinaliweka taifa katika mashaka makubwa sana, zinavutia mgawanyiko wa hali ya juu.
Kama kiongozi mkuu wa nchi pale unapoongea au kufanya jambo, ni tofauti kabisa na watu wengine hata kina Lowassa, Mbowe na Maalim Seif. Kiongozi wa nchi kama atashindwa kuchochea umoja basi ni heri ajiuzulu mapema kwani ameshindwa kuwa mkuu wa nchi kwa hatua za awali kabisa, umoja haujengwi kwa kuwatisha watu wenye ufuasi mkubwa nchini wala kuwatisha wafuasi wao. Kuendelea kuyatisha makundi mbalimbali kuna siku yanaweza kuungana na kuwa kitu kimoja kwa ajili ya kujibu mapigo na hapo ndipo yanapotokea mambo kama ya kaskazini mwa Uganda, Mashari mwa Congo na Sudan ya kaskazini vs Sudan ya kusini.
Sasa basi, kwa kuwa mheshimiwa rais anaonyesha kutokubadilika huku kasi hiyo ikizidi, ni bora akabanwa na mhimili wa kutekeleza sheria na ule mwingine wa kutunga sheria ingawa umeingiliwa ila bado unaweza kujipa meno ikiwa utakuwa kitu kimoja kwa wengi wao.
Ikiwa wabunge wataungana na kubadili sheria ama kuonyesha waziwazi kuwa yapo matamshi wasiyokubaliana nayo kutoka kwa rais (najua kwa sasa wapo wengi kutoka CCM) basi wanaweza kubadili sheria na kuifanya mahakama iwe na meno juu ya rais aliyeko madarakani na hapo kama nchi tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwa mustakabali wa taifa. Ama kwa kuonyesha tu uimara wao na kupaza sauti.
Haya yakiendelea hivi, basi ni majaaliwa mbeleni.
Tatizo akidi haitatimia bungeni