Kindumbwendumbwe cha ujana na maisha...!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
  • Ilikuwa ni siku moja Kibaha na mimba ikatungwa sawia.
  • Mama akaiba redio nikimwona, asubuhi akasema ni binti.
  • Picha ikaletwa kimzaha, lakini hali ikabadilika ghafla sana.........................

    Nilikaa na wale jamaa kwa siku tatu tu, lakini niliona mambo ambayo binadamu anaposimuliwa anaweza kudhani kwamba kuna dhihaka anayotakiwa kufanyiwa, yaani haiwezekani.

    Niliondoka Dar Es Salaam siku ya ijumaa kwenda Tanga. Nakumbuka ilikuwa ni Agost mwaka 1995. Nilikuwa nakwenda kwa jamaa ambaye aliniita kwake kwenda kumsaidia kukagua shughuli fulani ambazo alitaka kuzifanya. Wakati ule nilikuwa najitegemea, nilikuwa sijaingia serikalini kiajira.

    Nilifika mjini Tanga na kumkuta mwenyeji wangu na mkewe wakiwa kituo cha basi wakinisubiri. Tulisalimiana na walisema wamefurahi kunifahamu nami nilisema nimefurahi kuwafahamu. Ilikuwa ni mara yetu ya kwanza kukutana. Walipewa jina na mawasiliano yangu na jamaa yangu mmoja.

    Nilifika nao nyumbani kwao na kukaribishwa vizuri sana. Walikuwa wakiishi Raskazoni. Ilikuwa ni nyumba ya kifahari kwa kweli. Lakini nilibaini kwamba mama au mke wa yule mwenyeji wangu ndiye aliyekuwa na kauli pale nyumbani. Kwa kipindi cha saa moja tu tangu kufika nilipata picha hiyo bila matatizo.

    Wakati wa kula chakula cha usiku, nilitambulishwa kwa watu wa nyumba ile. Haikuwa nyumba ya watu wengi. Kulikuwa na watoto watatu wa yule mwenyeji wangu. Mkubwa alikuwa wa kiume aliyekuwa na umri kama miaka tisa, wa pili wa kike na wa tatu wa kike pia. Halafu kulikuwa na ndugu wa kiume wa mwanamke, kijana ambaye alikuwa ndio kwanza amemaliza kidato cha nne.

    Halafu kulikuwa na msichana wa kumsaidia kazi za ndani au house girl kama wanavyoitwa. Hawa wote nilitambulishwa kwao hapo mezani wakati wa kula. Lakini wakati tunakaribia kumaliza kula msichana mwingine mwembamba mweusi alikuja pale mezani na kukaa kitini, karibu wote tulikuwa tumeshashiba.

    Alianza kujipakulia chakula bila kusema neno. Ilikuwa inaonesha kwamba alikuwa ametoka kufanya kazi kwenye sehemu yenye maji kwani gauni lake lilikuwa na majimaji. Nilijua ni msaidizi wa ndani pia. Lakini niliona kwamba sio haki kumtendea vile , yaani kumwacha afanye kazi wakati wengine wanakula . lakini sikuwa nimeenda pale kwa sababu ya upelelezi.

    Nilianza kazi yangu iliyonipeleka pale usiku ule. Nilipewa chumba kilicho karibu kabisa na sebule, ilikuwa nifanye kazi ya kupitia mafaili kadhaa kabla sijaandika tarifa yangu ya kuwasaidia wale jamaa kupata walichokuwa wanahitaji. Naomba nisiseme ni kazi gani hasa. Kwa hiyo nilikuwa nimepania kufanya kazi hadi usiku mkubwa sana kama sio alfajiri.Nilianza kazi kwenye saa nne, nikimwacha mwenyeji wangu na familia yake hapo sebuleni, wakiangalia televisheni. Ilipofika saa sita usiku nilihisi kiu. Niliamua kuvumilia, lakini kiu ilinizidi na niliamua kwamba ningekwenda tu jikoni kutafuta maji ya kunywa.

Nilikuwa na uhakika alikuwa analia na alikuwa pia anajitahidi kufuta machozi ili nisijua. Kalikuwa ni kasichana kadogo, kazuri sana pamoja na kufujwa kule. Kama ningekuwa kijana bado ni wazi ningeoa msichana wa aina ile. Bahati mbaya zaidi ni kwamba mke wangu alifariki miaka mitano tu nyuma na nilikuwa bado na maumivu. Hisia zile ziliniumiza zaidi.

Nilirudi kule chumbani nikiwa nimeanza kuingiwa na wasiwasi. Lakini sio wasi wasi tu bali hata huruma. Kwa nini awe yule binti, na kwa nini sikutambulishwa kwake?
Sikupata jibu

Sikupata jibu. Ile hali ya kusafisha vyombo hadi saa 6:30 usiku, tena peke yake huku akilia, ilinikera sana, na nilijiambia siondoki pale bila kujua kitu kuhusu binti yule. 8:30 nilisikia kama miguu ya mtu huko sebuleni, nilihisi kwamba angekuwa ni yule binti. Hali hii ilinifanya niwe na hofu kidogo, kwa sababu mawazo yangu yalikwenda kwenye ushirikina hasa kwa kuamini kwangu kwamba, hapo Tanga palikuwa na ushirikina sana.

Nilizima taa ya chumbani mwangu pole polepole na kuchungulia. Aliyekuwa hapo sebuleni alikuwa ni mke wa yule mwenyeji wangu. Alikuwa amevaa gauni lake la kulalia na alikuwa anachukua kitu juu ya kabati ya sebuleni. Nilivutiwa kutazama zaidi. Niliona akichukua redio fulani ndogo nzuri sana ambayo hata jioni ile niliiona na kuitamani.

Bila shaka kwa shughuli za yule mwenyeji wangu, kuwa na vitu kama redio ya aina ile lingekuwa ni jambo la kawaida. Yule mama aliichukua redio ile na kuitia kwenye mkoba wake mkubwa wa kike na aliuweka mkoba huo kwenye kabati nyingine ndogo pale sebuleni. Halafu aligeuza na kurudi chumbani mwake.

Nilirejea chumbani mwangu nikijiuliza ni kitu gani hicho. Nilishindwa kujua yule mama alitaka kuipeleka wapi ile redio, na kwa nini aliiweka kwenye mkoba wake, usiku kama ule. Sikuweza kupata jibu , bila shaka hata kama ingekuwa ni wewe ingekuwia vigumu kupata jibu. Niliamua kuendelea na kazi nyangu.

Kwenye saa kumi kamili usiku nilisikia mtu huko sebuleni. Nilifungua amlango wangu wa chumba na kugundua kwamba ni yule binti. Alikuwa anafanya usafi. Niliwaza. Kulala saa saba na kuamka sa kumi alifajiri! Lakini kwa nini iwe ni yeye tu. Hilo likawa ndilo swali. Niliamua kulala nikiwa nimeumia sana.

Kwenye saa 12:30 asubuhi nilishtushwa na kelele za kilio cha mtu. Mtu huyo alikuwa akipigwa hapo sebuleni. Nilitaka kurejea kulala, lakini ilikuwa vigumu kwangu kutokana na kipigo na kelele hizo. Niliamua kufungua mlango wa chumba changu na kwenda sebuleni.

Yule binti wa usiku na alfajiri ambaye nilikuwa sijajua jina lake ndiye aliyekuwa akipigwa. Alikuwa akipigwa na mke wa mwenyeji wangu kwa mkanda. Kutokana na kauli za mama yule na yule binti mwenyewe , ilionekana kuwa alikuwa akituhumiwa kuiba kitu fulani. Mwenyeji wangu na wanaye pamoja na yule house girl walikuwa wakishuhudia kipigo kile kama vile wakiangalia sinema..

"Shangazi mimi sikuiba,siwezi kuiba, mimi sio mwizi" Yule binti alikuwa akilia kwa maumivu na alikuwa amelala chini akiwa hoi. Yule mama aliponiona aliacha kumpiga na aliondoka kwenda chumbani kwake huku akisema, "Nikija jioni nikute redio yangu, ama marehemu mama yako anilipe"
"Yaani mtoto kila siku wewe tu ndio kisirani ndani ya nyumba. Nimeshamwambia mjombako wewe ni kibwengo na mikosi haitaisha humu ndani……
Nilijua ni ile redio ambayo yule mama alikuwa ameiweka kwenye mkoba wake ambao bado ulikuwa pale juu kabati ndogo pale sebuleni. Nilijua kwamba, yule binti alikuwa akipigwa kwa kuonewa kabisa.
Lakini ni mimi tu na yule mama ndio tuliokuwa tunaujua ukweli huo, halafu na mungu.

Nilimtazama yule binti pale chini alipokuwa amelala kwa maumivu na nilihisi tu machozi yakinidondoka, Ingawa nilikuwa sijajua, yule msichana ni nani pamoja na kwamba likuwa akimwita yule mama shangazi, kwangu alionekana kuwa binti mwenye adabu na hekima pia.

Baada ya kunywa chai yule mke wa mwenyeji wangu akiwa hayupo , nilimuuliza yule mwenyeji wangu kuhusu yule binti. Aliniambi yule binti ni mtoto wa marehemu dada yake, ambaye alimzaa na mwanaume ambaye mama yake alikuwa anadai kwamba walikutana tu kwa bahati mbaya na hakujua kama alipata ujauzito. Hivyo hakuwa na anuani yake kamili. Huyo dada yake alifariki miaka sita iliyopita akimuacha yule binti na umri wa miaka minane.

‘Ndio nikamchukua, lakini kumbe alishaharibika na kwa kweli anatusumbua sana.
Ni msichana ambaye hata shule alikataa, alipomaliza tu la saba. Na kazi yake ndio hiyo ya wizi, kama hakuiba redio, simu, saa, deki basi utapata kesi ya umalaya.

Kama siyo hivyo basi umbeya mtupu. Mtaa wote unapata habari zinazoenda nyumba hii, basi tu sijui inakuwaje, siju ni laana kutoka huko kwa upande wa baba yake…….!

Nilianza kuipata picha na niliojua kwamba yule mke wa mwenyeji wangu hakuwa akitaka yule binti kuishi nao, kwa sababu zake. Alikuwa akifanya mambo na kumsingizia yule binti. Nilijiambia kwamba siku ya kuondoka pale ningemambia yule jamaa kuhusu ile redio. Lakini ingesaidia chochote?

Kesho yake jumapili nyumba nzima ilijianda kwenda kanisani, isipokuwa yule binti ambaye niliambiwa kwamba anaitwa Patience. Huyu aliachwa kwa ajili yakupika chakula cha familia. Niliona bila shaka ule ungekuwa muda mzuri kwangu kuzungumza na binti yule. Walipoondoka wote nilimfuata Patience jikoni na kumwomba nimsumbue wakati anapika kwa kuzungumza naye.Alisema wala simsumbui. "Nitashukuru maan sina mtu ninayezungumza naye humu. Wote wananidharau hadi huyu dada anayesaidia kazi" Alisema.

Nilimwambia ninaelewa, nimeona na nilimpa pole. Nilimuuliza kama ni kweli anaibana ni mbeya na anafanya tabia chafu za kihuni. Yule binti alibadiliaka ghafla na kusema, "Yqaani wameshakwambia niko hivyo, sasa mimi nimemkosea nini mjomba na familia yake" Akianza kulia, nilijisikia vibaya na kujilaumu kwa kumwambia vile. "Patience, nisikilize. Hebu nichukulie mimi kama baba yako. Naomba utulie unisikilize, kw sababu siamini hata jambo moja waliloniambia" Patience aliacha kulia na kunitazama sana hadi nikaogopa. "unasemaji?" Nilijikuta namuuliza. "hapana" alisema akijifuta machozi. Kwa kweli nilipokuw nikimtizama nilishinda kujua kama nilikuwa ninampenda, ninamwogopa, ninamwonea aibu au ninamfananisha. Ili mradi tu nilishindwa kuelewa.


Nilijisikia vibaya kuwa katika hali hiyo, lakini sikuweza kujizuia. "samahani, mama na wewe mlikuwa manishi wapi kabla hajafariki? Nilimuuliza. Alinitazama tena kama awali. "Tulikuwa tunaishi Arusha" Nilitaka kujua vitru fulani ili niamue kama ningeweza kumsaidia kumpata baba yake.

Lakini nilikuwa naogopa, maswali mengine huenda yangemkera.

"Mama yako alikwambia baba yako alikuwa anaitwa nani?" Yule binti alishika vidole vyake na kuchezesha miguu kwa muda kabla hajasema, "kama jina lako" nilijua alikuwa akinitania au alitaka kutumia mbinu ili niondoke naye. Ningeweza hata kufanya hilo kwa sababu kwa maisha kama yale ni wazi angeharibikiwa.
"Kwanza wewe unajua jina langu?" Niliuliza kwa mzaha. " nalijua, si nilimsikia mjomba akisema akimwambia shangazi, Mr……….akija atatumia chumba cha kwanza. Alisema na nilianza kuingiwa na wasi wasi.

Alilotaja ni jina la ukoo, hivyo niliona niendelee na maswali, nikijua labda binti yule angekuwa ni mtoto wa ndugu yangu "Jina la kwanza na baba yako alikwambia ni nani?" Nilimuuliza. "Alinitajia, nimelisahau, alikuwa akipenda kutaja hilo la pili" Binti alisema.

Halafu alisema, " Ninayo picha yake alipiga na mama, mnafanana naye kidogo. Ngoja nikaichukue ." aliondoka na kwenda huko chumbani kwake. Alikuwa akilala, kwenye kijichumba ambacho nadhani kilikuwa hasa ni stoo karibu na choo cha jumla cha mle ndani.

Nilijua ni mzaha mwingine, lakini nilitaka kumjua huyo mama na baba yake. Alirudi baada ya dakika kumi, bila shaka hiyo picha ilifichwa mbali sana. Alinipa picha hiyo na niliipokea kwa shauku kubwa. Nilitegemea kumwona ndugu yangu au mtu yeyote ninayemfahamu. Sikumwona yeyote kati ya hao ninaowafahamu. Ilikuwa ni picha ya mwanamke ambaye nilikutana naye kwenye semina ya maziwa, pale Shirika la Elimu kibaha mwaka 1981.

"Germana!" Nilinong'ona. Nilihisi nikiloa jasho mwili mzima na kwa muda fulani sikujua hasa nilipokuwa. Nilijikuta nikikaa kweky kiti hapo jikoni. Ni kama ndoto, ni ka hadithi, ni ka sinema fulani. Nakwambia ukweli sijawahi kuhisi hali ile maishani na sijui kama nitakuja kuhisi, maana nashindwa hata kukueleza.

Yule binti alinishika na kunitazama machoni, "Unamjua mareehemu mama?" Alniuliza na sikuweza kumjibu. Nilitembe na mwanamke huyu ambaye ndio najua kwamba ni marehemu, siku moja tu kwenye semina ile. Hakuna aliyekumbuka kuchukua taaarifa kamili za mwenzake, kwa kuzingatia kwamba hatukuwa waajiriwa na tulikuwa ndio tuaanza maisha, vijana tunaochemka. Mambo ya semina, kutenda na kusahau.

"Kumbe Germana alizaa aliza mtoto mzuri hivi, mtoto wangu. Damu yangu inateswa na kudhalilishwa hivi". Niliinama na kuanza kulia. Halafu niliinua kichwa na yule binti alikuwa akibubujikwa na machozi pia.
"Mi-mi, mimi ni baba yako Patience. Nisamehe, tusa-tusamehe sana halikuwa kosa letu……sikuweza kuendelea.

Waliporudi kanisani walishngaa kukuta tukiwa na Patience kule chumbani mwangu tukiongea na kucheka sana. Yule mke wa mwenyeji wangu ambaye sasa ni shemeji yangu alimwita Patience kwa nguvu na kisirani.

"Umeanza siyo? Unataka kumvuruga huyo baba wa watu, kisa?"
"Yaani wewe mtoto nitakuuwa tu, lazima" Nilimambia Patience akae kwanza hapo chumbani. Nilitoka mimi na kumfuata mke wa jamaa yangu, "Hapana dada, ni mimi nilimwita"

halafu nilimwita mwenyeji wangu aliyekuwa akitokea chumbani mwake kuja sebuleni.
Alipokuja nilimkabidhi ile picha niliyopiga na dada yake, alipoichukuwa aliitizama na kunitizama, aliitizama tena na kunitizama. Halafu alikwenda kukaa kwenye kochi na kushusha pumzi kwa nguvu.

"Naomba radhi, mimi ni baba wa mtoto Patience. Nimeamini kilichonileta huku Tanga siyo hii kazi yako bali ni nguvu ya damu yangu…..Mke wamwenyeji wangu aliingilia kati. "Ni kitu gani?"
Niliwasimulia kila kitu.

Sitaki kukuchosha. Hivi sasa Patience anasubiri kujiunga na masomo chuo kikuu baada ya kufaulu vizuri mtihani wake wa kidato cha sita. Amechelewa kusoma, ndiyo, lakini anataka kusoma na anamudu. Kumbuka jambo moja, Kila binadamu unayemtendea jambo baya, unaitendea damu yako jambo baya bila kujua. Kila binadamu unayemtendea jema, unaitendea jema damu yako bila kujua.

Sisemi kwa ubaya, lakini yule mke wa rafiki yangu alifariki mwaka 2001 kwa ugonjwa ambao inadaiwa kwamba ni ukimwi. Hali ya uchumi ya mumewa inatisha sana. Tazama naye yule mama marehemu aliacha watoto watatu. Je huko alipo atajisikia vipi watoto wake leo wakitendwa kama alivyokuwa akimtenda Patience? Kwani kuwapenda wengine gharama yake ni kiasi gani?

Je sisi wanaume tuna watoto wangapi huko nje ambao hatuwajuiwala kuwatambua? Lakini ni mara ngapi tunatamani na kuwafanya watoto hao kuwa wapenzi wetu?
Hatuoni tunafanya mapenzi na damu zetu?



Habari hii iliwahi kuandikwa katika gazeti la JITAMBUE..............
 
  • Je sisi wanaume tuna watoto wangapi huko nje ambao hatuwajuiwala kuwatambua? Lakini ni mara ngapi tunatamani na kuwafanya watoto hao kuwa wapenzi wetu?
    Hatuoni tunafanya mapenzi na damu zetu?



    Habari hii iliwahi kuandikwa katika gazeti la JITAMBUE..............
  • Hii point inatosha kabisa kuliko kuja na gazeti :biggrin:
 
Niliona haingenoga bila kuandika gazeti...........
Hata hivyo nashukuru umesoma gazeti..........................LOL
Inabid tuyasome magazeti ya mtambuzi on line...Yana point nyingi zenye faida lakini ukisha maliza kulisoma gazeti mpaa unaona K kama R na B kama D :biggrin:
 
Mtambuzi moyo umeitika gudu...LOL hii ni nouma na ndivyo midume mingi ilivyo inaproduce tu bila tahadhali kisha inajikuta ndo mi end users.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nimesoma nimeelewa vizuri,
pole kwa kufiwa na mpenzi wako wa zamani,
pole kwa binti yako,

Kumbe hata wale ombaomba pale fire wanababa zao
humu jf.

Huyo binti bila shaka ni Cantalisia, mpe pole sana.
 
thanks mtambuzi,habari ni nzuri mno.mara nyingine watoto wanaolelewa kimateso na walezi na wakiwa wanabaguliwa kimalezi,mfano watoto wako uwadekeze na ambae sio wako umlee kimateso.akiwa mkubwa anakuwa anamudu na kukomaa kimaisha.na wengine huwa na maisha mazuri baadae,wababa mnapozaa nje,msiwatelekeze watoto.kwani watoto hawana makosa.
 
Kwa hili una haki ya kupokea mahari mara mbili mbili
kwa Cantalisia, kweli umemtoa mbali sana.
 
Duh! Hii imekuwa kama mahubiri ambayo tunapewa kabla hatujaungama dhambi zetu...
Honestly sipendi wala huwa simfanyii mtu uovu ila this post set me thinking deep.
Hasa hasa wanaume ambao hupenda vibinti vidogo na kusahau na wao wana right ya kukua kwanza kama binti zao walivyo nayo...
 
I almost droped tears...thanx
Edoedward1 ..............Mkuu hii ni fujo sasa......... Iweje u-quote habari yote kwa comment ambayo hata haijai mstari mmoja.........!
Naomba kwa hisani yako u-edit na kuondoa hiyo quote ili kutupa nafasi sisi wenye kutumia CM...........
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom