Kinana atumia dk zaidi ya 45 kuiongelea CHADEMA

Ukisikia utaahira ndio huu. Bado siasa zilezile za majitaka ambazo wapinzani wao wakitaka wanaweza kuzihubiri vizuri sana. Bado hawajifuzi kutokana na la ugaidi na udini ambalo waliliasisi lakini leo hadi Mkuu wa nchi kisha ingizwa humo! Bado hajajifunza muda sio mrefu Chadema watathibitisha CCM ndio waasisi wa udini nchini? Bado anaendekeza siasa za maji taka?

Nawaonea huruma sana hawa CCM kwa sisasa zao hizi. Sawa kaifananisha CDM na Savimbi; kesho CDM nao wakiibuka na kunadi kwa wananchi CCM ni sawa na tawala za kifashisti za Ulaya Mashariki ya enzi hizo akina Romania ambao walikuwa washirika wazuri wa magamba? Kama watawala wa tawala hizi walipigwa risasi hadharani kutokana na matendo maouvu kwani swahiba wao CCM viongozi wake nao wasipigwe risasi kutokana na ukatili waliolitendea taifa hili?


Wasishangae wananchi kuandamana kudai viongozi wetu wastaafu wanyongwe hadharani! Huyo anacheza michezo ya hatari sana sababu tu ya ukusoefu wa busara au ulevi wa madaraka au vyote. Siasa za maji taka hazijengi sana sana zitakurudia! Ni ushauri tu.
 
Ameona wanamuumbua katika biashara yake ya meno ya tembo. Pia anafikiria chadema ikishinda uchaguzi 2015 yeye akimbilie nchi gani kujihifadhi, hatma ya biashara yake na namna mpya ya kujiongezea kipato. Hivyo lazima cdm imnyime usingizi
 
CCM ni mbaya acha kulemba
  • Walimu wananyanyasika na wanadai zaidi ya bilioni 25...soma mwananchi la leo ukurasa wa 4 column ya 4 paragraph 5 utaona.
  • Polisi pesa zao za kwenda kufanya mauaji ya Mwandishi wa habari kule Nyororo mufindi walikuwa wanalalamika hawajalipwa.
  • Kutekwa kwa ulimboka wamekamata mtuhumiwa mkichaa na wakati wameambiwa wahusika wanatoka ikulu
  • Madaktari wanalia
  • Wagonjwa wanakosa vipimo vya CT scan muhimbili sasa hospitali ndogondogo za wilaya inakuwaje
  • Ardhi ya wakulima na wafugaji wameichukua,,,....kumbuka hotuba ya Halima mdee bunge la mwaka juzi
  • Viwanda wamejiuzia
  • Nyumba za serikali wamewapa wake zao
  • Miradi wanajigawia
  • EPA wamekula
  • Richmondi @day mil 152 wamekula kwa miezi 22
  • Dowazi inadai fidia wapewe mafishadi.
  • Tembo wamewamaliza....alafu unataka kinana aseme shishiem mbaya na tembo wanamkimbilia!!!!!!!!!!!!
  • Elimu wanajipatia Udokta bure bure wameshindwa uprofessor tu.
  • Wezi wanajiudhuru wasamalia wanaozea jela kwa kubambikizwa kesi.
  • Vyeo wanapeana kwa kujuana na sio weredi.
  • Watoto wao wanapewa ukuu wa wilaya ona wakina John Mongela, wengine wamejaa ikulu na BTo alafu unataka waseme cdm nzuri wakati inawakosoa!!!!!
  • Wakurugenzi wanatuibia sana na wanahamishwa vituo.

Jamani kama macho yenu hayaoni si hata mnuse na kama hamuwezi kunusa basi na mpapase

Haya ni kwauchache tu,ulitaka waambiwe nani wakati ccm ndio wanaofanya haya na ndio wanaongoza inchi hii tangu uhuru????? :yo:
 
Haijawahi kutokea kwa katibu mkuu wa CCM kuiongelea CHADEMA kwa muda zaidi ya dakika 45.

Ama kweli CHADEMA ni mwiba kwa CCM.bado kitambo kidogo tu!
Hata mimi nimemsikiliza mwanzo hadi mwisho. Anaonekana ameathiriwa sana na CHADEMA. Hakuna sentensi aliyosema ambayo haikihusu CHADEMA. LAKINI PIA KILICHOZIDI KUNISHANGAZA NI KUWA UMATI MKUBWA ULIOKUWEPO ULIKUWA HAUMSHANGILII HATA KIDOGO! Huenda ni kweli kuwa walikwenda hapo kwa kuona wasanii kama Diamond na si kuhudhuria mkutano wa CCM.
 
Kinana anatia huruma!!! leo nusura alie jukwaani, dah sijawahi kuona!!!
 
CCM ni mbaya acha kulemba
  • Walimu wananyanyasika na wanadai zaidi ya bilioni 25...soma mwananchi la leo ukurasa wa 4 colum ya 4 paragrapg 5 utaona.
  • Polisi pesa zao za kwenda kufanya mauaji ya Mwandishi wa habari kule Nyororo mufindi walikuwa wanalalamika hawajalipwa.
  • Kutekwa kwa ulimboka wamekamata mtuhumiwa mkichaa na wakati wameambia wahusika wanatoka ikulu
  • Madaktari wanalia
  • Wagonjwa wanakosa vipimo vya CT scan muhimbili sana hospitali ndogondogo za wilaya inakuwaje
  • Ardhi ya wakulima na wafugaji wameichukua,,,....kumbuka hotuba ya Halima mdee bunge la mwaka juzi
  • Viwanda wamejiuzia
  • Nyumba za serikali wamewapa wake zao
  • Miradi wanajigawia
  • EPA wamekula
  • Richmondi @day mil 152 wamekula kwa miezi 22
  • Dowazi inadai fidia wapewe mafishadi.
  • Tembo wamewamaliza
  • Elimu wanajipatia Udokta bure bure wameshindwa uprofessor tu.
  • Wezi wanajiuzuru wasamalia wanaozea jela kwa kubambikizwa kesi.
  • Vyeo wanapeana kwa kujuana na sio weredi.
  • Wakurugenzi wanatuibia sana na wanahamishwa vituo.

Jamani kama macho yenu hayaoni si hata mnuse na kama hamuwezi kunusa basi na mpapase

Haya ni kwauchache tu,ulitaka waambiwe nani wakati ccm ndio wanaofanya haya na ndio wanaongoza inchi hii tangu uhuru????? :yo:
 
Lazima wagangamale kitumbua kinaondoka cdm wataitwa majina yote mabaya lakini haitasaidia.azungumzie na ujangili wake.
 
hivi kama kweli wao ccm ni bora kwa nini watumie gharama kubwa kusomba watu kupeleka kwenye mkutano wao na badala ya kutangaza tu kisha kuwaacha watu waamue wenyewe kama watakwenda ama hawataki kwenda. Wakifanya hili watakuwa wameweza kujipima vizuri zaidi kuhusu kukubalika kwao ili wasiendelee kuishi kwenye ndoto
 
Ni LAZIMA kuitahadharisha jamii na chama kinachotaka nchi isitawalike.

Hata Deo Filikunjombe alishawahi kuwambia CCM inazani ina hati miliki ya nchi hii mi sipingani na hotuba ya Kinana hata kidogo kaongea masuala mengi sana kuhusu CDM na kuna machache ya muhimu na mengine yalikua ya kipuuzi. Kuna mawili aliyozungumza kuhusu CDM kwangu mimi naona ni ya muhimu kwa CDM
1.CDM ina uzoefu wa muda wa miaka 20 sasa kwa muda huo lazima kuwepo na mapungufu na changamoto ndani ya chama so nijukumu la uongozi kukaa na kutafakali kwa kina na kutatua migogoro hiyo sio kila tatizo ndani ya chama ni kuilalanikia CCM.
2.Wanatakiwa wajue kuwa People's power ipo katika box la kura sio kwa maandamano na migomo.
MY TAKE.
1.Kwa kauli ya Kinana ni kweli kabisa kuwa CDM chama changu karibia migogoro yote inayotokea lawama inaielekeza kwa CCM tumesahau kuwa hata CDM wanachama wake sio malaika kuna sehemu wanakosea so tukubali hilo na pia tujue kuwa CCM nao wanapambana kukiua chama so tuwe makini ndani ya Chama na nje ya chama.
2.Kauli yake ya People's Power ni ionekene katika box la kura. Nakubaliana na Kinana kwani ni muda muafaka sasa kwa CDM katika mikutano yake kuwahamasisha wanachama na wafuasi wake wote kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili muda ukifika kweli umati unaoonekana katika mikutano na maandamano yetu uonekane katika kupiga kura,kwa kufanya hivyo naamini kabisa tutafikia lengo.
So tuchukue mazuri na mabaya tuyatupe.
 
Utajiju, kwani kuna mkutano gani wa chadema usiozingumzua ccm?

ukiona mtu mzima anatumia lughaya utajiju basi jua huyo mtu si riziki, pole kwa kukubali kutumika na kuwa punga. Ushauri wangu kwako ningekuomba kwanza urejee shule maana hata kiswahili bado hujafuzu,
 
Ukishaona mtu mzima tena wa Kiume ameacha kufuatilia mambo yake yanayomuhusu yeye akaanza kufuatilia mambo ya watoto wa jirani zake ujue kwake kumeshaharibika totally, ni kwamba mke wako hakuheshimu anarudi amelewa, baba anakula housegirl, mama analiwa na jirani, mtoto wa kike analiwa na houseboy, mtoto wa kiume anakula bange, gongo kiroba nyumba nzima shaghalabagagla, hapo baba hana say yoyote inabidi aanze kuongea mambo ya watu yasiyomuhusu, ndiyo kina Nepi na Kinana (CCM)
 
Ukishaona mtu mzima tena wa Kiume ameacha kufuatilia mambo yake yanayomuhusu yeye akaanza kufuatilia mambo ya watoto wa jirani zake ujue kwake kumeshaharibika totally, ni kwamba mke wako hakuheshimu anarudi amelewa, baba anakula housegirl, mama analiwa na jirani, mtoto wa kike analiwa na houseboy, mtoto wa kiume anakula bange, gongo kiroba nyumba nzima shaghalabagagla, hapo baba hana say yoyote inabidi aanze kuongea mambo ya watu yasiyomuhusu, ndiyo kina Nepi na Kinana (CCM)

Akili za bavicha hizi...
 
Back
Top Bottom