Kinana atumia dk zaidi ya 45 kuiongelea CHADEMA

Utajiju, kwani kuna mkutano gani wa chadema usiozingumzua ccm?

Nadhani mikutano yote ya UPINZANI lazima izungumzie CCM na JINSI ya kuiondoa Madarakani iwe CUF; NCCR; CCJ na Vingine sio hicho CHADEMA pekee... au unataka kusema vyama vingine vya upinzani haviongelei CCM hata kidogo?

Sasa Vinaongelea nini kwenye Majukwaa yao?
 
Watanzania wenzangu unamfurahia mtu anayekupa tonge mdomoni kwa siku moja na kukufunga ulimi?, mzee huyu wa miaka zaidi 50 anae wanywea wajukuu wake mchuzi kwa kuiba rasilimali za nchi hii bila kufikiria kizazi kilichopo na kijacho shame on him sidanganyiki ngo!
 
CCM ni mbaya acha kulemba
  • Walimu wananyanyasika na wanadai zaidi ya bilioni 25...soma mwananchi la leo ukurasa wa 4 column ya 4 paragraph 5 utaona.
  • Polisi pesa zao za kwenda kufanya mauaji ya Mwandishi wa habari kule Nyororo mufindi walikuwa wanalalamika hawajalipwa.
  • Kutekwa kwa ulimboka wamekamata mtuhumiwa mkichaa na wakati wameambiwa wahusika wanatoka ikulu
  • Madaktari wanalia
  • Wagonjwa wanakosa vipimo vya CT scan muhimbili sasa hospitali ndogondogo za wilaya inakuwaje
  • Ardhi ya wakulima na wafugaji wameichukua,,,....kumbuka hotuba ya Halima mdee bunge la mwaka juzi
  • Viwanda wamejiuzia
  • Nyumba za serikali wamewapa wake zao
  • Miradi wanajigawia
  • EPA wamekula
  • Richmondi @day mil 152 wamekula kwa miezi 22
  • Dowazi inadai fidia wapewe mafishadi.
  • Tembo wamewamaliza....alafu unataka kinana aseme shishiem mbaya na tembo wanamkimbilia!!!!!!!!!!!!
  • Elimu wanajipatia Udokta bure bure wameshindwa uprofessor tu.
  • Wezi wanajiudhuru wasamalia wanaozea jela kwa kubambikizwa kesi.
  • Vyeo wanapeana kwa kujuana na sio weredi.
  • Watoto wao wanapewa ukuu wa wilaya ona wakina John Mongela, wengine wamejaa ikulu na BTo alafu unataka waseme cdm nzuri wakati inawakosoa!!!!!
  • Wakurugenzi wanatuibia sana na wanahamishwa vituo.

Jamani kama macho yenu hayaoni si hata mnuse na kama hamuwezi kunusa basi na mpapase

Haya ni kwauchache tu,ulitaka waambiwe nani wakati ccm ndio wanaofanya haya na ndio wanaongoza inchi hii tangu uhuru????? :yo:

kula tano! jamaa wanajitahidi kumpa mbwa jina baya! badala ya kutimiza wajibu wao!
 
chadema unatisha hualazi usingizi chama cha kijani unatisha mpaka mwenye njii hakai vyema kwenye kiti
 
Katibu Mkuu wa CCM amemaliza hotuba yake jioni hii huko Morogoro. Katiba hutuba yake iliyokuwa na kauli za kipropaganda zaidi, alitumia muda mwingi kuikandia Chadema kuwa ni chama ovyo kisichofaa kuungwa mkono na wasikilizaji wake. Alitoa kauli nyingi ambazo zimepindisha ukweli kwa lengo la kuithibitishia hadhira yake kuwa Chadema si chama makini. Alisema, 'Chadema walisema kuwa wakiingia madarakani watabadili Katiba ndani ya siku 100 na sasa wanadai muda uongezwe hadi 2016". Ninchfahamu mimi Chadema walisema wataanzisha mchakato ndani ya siku 100. Pia amesema, Kiongozi wa Upinzani Bungeni amesema Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi hawafai..." Mimi sijasikia kiongozi wa Upinzani akisema hivyo. Hotuba yake ilijaa kauli za namna hiyo ambazo wanajamvi wenzangu mliokuwepo au mliosikiliza mtazitaja hapa ili kuonyesha jinsi CCM inavyoonyesha kuwa maji yako shingoni na sasa imeamua kujitoa kimaso maso kupambana na Chadema. Bahati nzuri watanzania wengi hivi sasa wanajua nani anasema ukweli na nani anawafanya mazoba. Mpambano unaendelea na upande wa pili (chadema) watajibu mapigo. Tusubiri tuone.
 
Ni LAZIMA kuitahadharisha jamii na chama kinachotaka nchi isitawalike.

walitakiwa kuwaeleza wanachi ni kwa nn maisha bora yameshindikana kwa miaka 50 badala ya kuijadili chadema maana chadema hawajatawala nchi hivyo ccm kuiongelea ni kupoteza dira,
ila cdm kuiongelea ccm ni sawa maana wao ndy wanaogiza nchi hivyo wizi wa mali za umma, ukiukwaji wa haki za raia na kila aina ya upuuzi. Hivyo ni wajibu wa cdm kuwaambia watz sababu na chanzo cha umaskini wao.
 
Yaani mkuu unataka huduma isirejeshwe kweli? Kwa sababu za kisiasa, ili chama fulani kipate sababu ya kusema serikali haijali?
na hii mtaiweka kwenye mafanikio ya chama?kweli?hospitali ya rufaa ya mkoa kwa miaka 50 ya uhuru mnaongelea Ultra sound kwa hospitali ya mkoa?
 
Mbona Dr. Slaa na Mbowe walitumia robo tatu ya muda waliopewa kuiponda CCM? hayo ni ya kawaida ndugu mleta mada, kama uyapendi basi anza kuwakosoa viongozi wako wa CHADEMA.

Hayo majina yanawakosesha usingizi CCM.

CDM wanaiponda serikali ya CCM na siyo CCM kama unavyotaka tuamini.
 
ameiongelea cdm zaidi kuliko chama chake.mpaka anataka kulia.cdm kiboko yao

umeonae hata mi nimemuona Chadema imewabana mbavu jamani sio siri tena! Kinachomuumiza zaidi kinana ni mkanda waofake wa ugaidi kukosa mvuto pamoja na list ya mashetani 10 waliotajwa na marando,kazi kweli kweli.
 
katibu mkuu wa ccm amedai kua chadema sasa kimekua na hivyo migogoro haiepukiki.pia medai kuwa hata ccm kuna matatizo na migogoro lkn wanapambana kuitatua badala ya kutafuta mchawi kama wanavyofanya cdm.pia amewashauri viongozi wa vyama vya siasa kuwa na utamaduni wa kuachia madaraka mapema badala ya kung`ang`ania mpaka wachokwe na wanachama wao.pia amewashauri wabunge kuikosoa serikali kwa kujenga hoja badala ya kupiga makelele na kufanya vurugu bungeni.ni katika mkutano wa ccm morogoro
 
Hiyo haina tatizo kwani msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Hawa jamaa sijui wanafanya nini! Hawaelewi kuwa watanzania wa sasa hawadanganywi na propaganda zisizokuwa na miguu wala macho. Kwanza ni aibu tu kusimama mbele ya watu unaanza kuelezea mambo ya chama cha upinzani! Waeleze wanannchi unawafanyia nini ili waondokane na matatizo ya maisha kuwa magumu. Yeye huyo sijui anishi wapi? Hizo propaganda za siasa za kichina zimepitwa na wakati. Fanya kazi ili watu waone what chama tawala can deliver to the Tanzanian people. Blaa blaa imekwisha. Muulize mama yangu mwenye miaka 79 anasema chama tawala kimezeeka vibaya kwani yeye mbali na kuwa na mika 79 bado anaweza kuchambua na kuona uongo wa chama hicho. Haya sasa semeni nyie wenye nchi
 
na hii mtaiweka kwenye mafanikio ya chama?kweli?hospitali ya rufaa ya mkoa kwa miaka 50 ya uhuru mnaongelea Ultra sound kwa hospitali ya mkoa?

Mkuu kweli hiyo ni mbaya sana.

Lakini mbaya zaidi ni pale watanzania wanaojiita wazalendo wanachukia kuona ultra sound imenunuliwa kwa ajili ya kupatia wananchi huduma. Chadema inaharibu kabisa vijana na kuwafanya wachukie maendeleo kwa sababu za kisiasa.
 
Back
Top Bottom