Elections 2010 Kinana alia na REDET adai imeilima CCM katika kura ya maoni!!!!!!!!!!!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Huku akionekana mwenye furaha tofauti na wakati alipokuwa analalamikia Chadema walipodai SYNOVATE wameficha matokeo, Abdulrahaman Kinana ameikosoa REDET kwa kile alichokiita ni kutumia mtindo wa kimikoa badala ya majimbo na hivyo kupunguza wastani wa kukubalika kwa CCM hususani mgombea wake wa uraisi.

Akihoji utaratibu wa kura hiyo ya maoni alidai CCM itaibuka na asilimia 88 badala ya ile ya 71% ambayo wengi wanaona ilikuwa imechakachuliwa na hivyo kutowatendea haki watanzania.

La kushangaza, Kinana hakuelezea ni vipi majimbo yaliyo ndani ya mikoa yawe hayakujumuishwa kwenye utafiti huo. Hivyo, alishindwa kuthibitisha hoja yake ni vipi CCM ilikuwa imeathirika na utafiti huo wa REDET iwe ya kimikoa au ya kimajimbo.

Vilevile, Kinana alikuwa bubu juu ya inakuwaje Dr. Slaa awe ana mvuto mkubwa kwa wananchi kwenye kampeni zake lakini asiweze kuwa anakubalika kuliko JK ambaye watu huenda kwenye mikutano yake kusikiliza burudani za kizazi kipya.
 
Kinana anajua kilichofanyika, anahofu sana. Dr slaa anakubalika kuliko JK.

TBC wafanye utaratibu kura za live , unapiga simu na kumtaja mgombea unayempenda awe rais 2010.

Then wapime nani ataongoza. Matokeo yatawashangaza.
 
Hili jambazi la kisomali linatufanya sisi wajinga kwamba hatuna akili! Yamechakachua kura za maoni kwa kushirikiana na REDET, then anajifanya analalamika ili tuone kuwa hakukuwa na mawasiliano yoyote katika uchakachuaji kati ya CCM na REDET. 2010 sidanganyiki, mama, baba,wadogo na kaka zangu hatudanyanyiki.
 
Bwa ha ha ha .. kuna watu wamefanya uozo maishani mwao to a point kwamba hawajali tena kama wanachoongea au kufanya kinachukuliwa vipi na wasikilizaji wao.

Kinana:

1. Meli yake ilikamatwa ikiwa na mali haramu
2. Uraia wake ni wa utata
3. Amekuwa akihusishwa na ughaidi wa somalia
4. Biashara zake za utata zinahusishwa na ukwepaji mkubwa sana wa kodi Tanzania
5. Alifoji risiti za mama salma

....

Na bado anapewa microphone na kumwaga upupu kwa watanzania as if nchi haina vyombo vya usalama na sheria?!
 
Amehusika na milipuko ya mabomu ya Kigaidi Uganda!
 
Kinana anadhani kwa kutoa msisitizo na kulalamika kwamba REDET imewaonea atabadili mawazo ya Watanzania wapenda maendeleo na mageuzi... Hatudanganyiki!!! Mi nimeshawaelimisha watu wote kijijini kwetu na wanamkubali Slaa kupita maelezo. Wanamapinduzi wenzangu, tukawaelimishe ndugu na jamaa zetu vijijini. Hata wao wanaona machungu ya kuongozwa na CCM ila hawapewi elimu ya Uchaguzi. Siku moja utakayotumia kijijini kwenu italeta mabadiliko kuliko siku 365 tunazotumia kukaa mijini na kutaka mabadiliko. Vitendo ni sasa.
 
Hili jambazi la kisomali linatufanya sisi wajinga kwamba hatuna akili! Yamechakachua kura za maoni kwa kushirikiana na REDET, then anajifanya analalamika ili tuone kuwa hakukuwa na mawasiliano yoyote katika uchakachuaji kati ya CCM na REDET. 2010 sidanganyiki, mama, baba,wadogo na kaka zangu hatudanyanyiki.
Umeniwakilisha mkuu! This is what i was also thinkin.
 
Kinana anajua kilichofanyika, anahofu sana. Dr slaa anakubalika kuliko JK.

TBC wafanye utaratibu kura za live , unapiga simu na kumtaja mgombea unayempenda awe rais 2010.

Then wapime nani ataongoza. Matokeo yatawashangaza.

mzee watu wangapi wanauwezo wa kumiliki simu na pia kupiga? uwezo wa tibisii kupokea simu ukoje?
 
Yaani ccm wan a mbinu za kizamani sana..wanajua jk hapati hat a kura asilimia 30 lakini bado wamo tu
 
Yaani ccm wan a mbinu za kizamani sana..wanajua jk hapati hat a kura asilimia 30 lakini bado wamo tu

kweli bana hebu na wewe kesho itisha presi konferensi utangaze matukeo ya utafiti wako labda wataacha.
 
Bwa ha ha ha .. kuna watu wamefanya uozo maishani mwao to a point kwamba hawajali tena kama wanachoongea au kufanya kinachukuliwa vipi na wasikilizaji wao.

Kinana:

1. Meli yake ilikamatwa ikiwa na mali haramu
2. Uraia wake ni wa utata
3. Amekuwa akihusishwa na ughaidi wa somalia
4. Biashara zake za utata zinahusishwa na ukwepaji mkubwa sana wa kodi Tanzania
5. Alifoji risiti za mama salma

....

Na bado anapewa microphone na kumwaga upupu kwa watanzania as if nchi haina vyombo vya usalama na sheria?!

Hili ni tatizi kubwa la CCM -- kukosa mtu safi wa kuwa msemaji wao mkuu hasa wakati huu wa kampeni. Mimi nadhani CCM sasa hivi hawana kabisa viongozi wasafi na ndiyo maana watu kama kina Kinana wanafanya kazi hiyo. Tatizo linakuja pale chochote anachotamka watu kwanza huanza kushambulia uchafu wake na kutupilia mbali yale aliyoyatamka. Nawaonea huruma CCM kufikia level hii... INASIKITISHA!!!!!!
 
Back
Top Bottom