Kinaitwaje Kifaa kinachotafsiri Lugha kwenye kumbi za mikutano ya kimataifa?

King Octavian

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
403
349
Wakuu naomba kusaidiwa kwa kufahamishwa jina la kifaa na undani wa teknolojia inayotumika katika vifaa vinavyo-interprete lugha katika kumbi mbalimbali za mikutano ya kimataifa. kwani mara nyingi huwa naona baadhi ya watu wanaohudhuria mikutano kama hiyo wanavaa vifaa kama headphones, nilipouliza ni nini nikaambiwa ni vifaa vya kutafsiri lugha kwa wale wasioielewa.
Je, ni kweli hii teknolojia ipo? na inakuwaje wataalam naomba maujuzi yenu vinafanyaje kazi hivi vitu?.
 
Sijui kama kuna kifaa kama hicho, mimi ninachojua kumbi hizo zinakuwa na control room ambayo mara nyingi inakuwa above ukumbi,na watu wanaokaa huko huwa wanaangalia meza kuu bila washiriki wengine kuwaona na huko kunakuwa na wakalimani wa lugha mbalimbali,ambao wanachofanya ni kumskiliza mzungumzaji mkuu na wao kufafsiri kwa lugha zingine. Sasa kuna kifaa ambacho kinakuwa na chanel mbalimbali kwenda kwenye headphone wanazotumia washiriki. Mshiriki anakuwa anachagua chanel mbalimbali kama inavyokuwa kwenye radio ili kupata tafsiri mbalimbali za lugha kutoka kwa wakalimani walioko control room. Hii ni kwa uzoefu wangu katika conference nilizowahi hudhuria. Wengine karibuni za uzoefu na uelewa wenu
 
Hakuna kifaa kama hicho, zile ni headphones za kawaida na ni kama mdau alivyoeleza. Vifaa hivyo vipo kwenye stage ya majaribio akina Microsoft na Google wanavifanyia kazi, vinatumia computer science nzito.
 
Back
Top Bottom