Kwanza kabisa wachawi wanaongozwa na roho ya kishetani (evil spirit) au viumbe vibaya vilivyo ndani yao. Wachawi kwa ujumla hutumia ujuzi, na uchawi ili kudumisha afya zao. Matokeo yake Wachawi wanaongoza kwa kuishi muda mrefu. Wachawi wengi huishi miaka 80, 90 au 100 au zaidi.
Inakuwaje ndani ya familia au ukoo ni vigumu kuwajua wachawi hata kama ni mzazi wako ila nje ya familia inakuwa inajulikana mji ule au ukoo ule ni wa walozi? Je, ni kitu gani unaweza kufanya kujua mzazi au ndugu wa karibu ni mchawi? na je, inawezekana mchawi kumchukua msukule mtoto wake mwenyewe wa kumzaa? mwisho nini kina wa motivate watu kufanya uchawi au ushirikina?