Kinachojengwa Mbezi mwisho ni kuchezea kodi za Watanzania

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,111
18,327
Kwanza naomba kusema wazi naunga mkono wazo la upanuzi wa barabara ya Kimara Kibaha.

Pili nailaumu sana tena sana Tanroad na wizara ya ujenzi kwa kuchezea kodi za wananchi kwani kila baada ya miaka 10 miundombinu hufumuliwa na kujengwa upya.


Kinachojengwa pale Mbezi Mwisho hakitaishi zaidi ya miaka 10 kila kitu kitabomolewa na kujengwa upya.

Mbezi Mwisho ni makutano ya pande mbili za Dar es Salaam

Mbezi mwisho ni mji unaokua kwa kasi kuliko mji wowote hapa Dar.

Mbezi mwisho ni lango la kuingia na kutoka Dar.

Kwanini Tanroad hamtaki kufikiria design nzuri walau kwa miaka 50.

Hamjifunzi mkoloni alivyoweka mita 240 upana wa barabara toka Kimara hadi Kibaha.

Hivyo viraundi abauti mnavyovijemga hapo Mbezi ni kupoteza kodi za wananchi.

TANROAD INAHITAJI NEW BRAIN

Uzi huu tutakuja kuukumbuka siku wakianza kubomoa wanachokijenga
 
Wanazidiwa akili na MABEBERU waliona mbali miaka ya GIZA ila sie tupo millenium lakini bapo kama tupo Nineteen kweusi.
Tazama pale ubungo, baada ya kuweka mzunguko wa mabati. Hakuna foleni.
Kumbe foleni ilikuwa inaletwa na yale mataa mabovu mabovu. Sijui kwanini hawakuweka mzunguko tangia miaka yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu una utaalam wowote katika civil engineering?
Unajua sheria ya barabara?
Hata mwendokasi wakati inajengwa,kulikua na wataalam elekezi feki kama wewe wengi tu
Wewe ni mtu mjinga sana....hiyo civil engineering iliyoshauri BRT ipite jangwani bondeni ambapo maji hujaa kila siku mvua ikinyesha ndio unayoizungumzia? Inasikitisha sana.....kama ulienda shule..hakika ulienda kusindikiza wengine..pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tazama pale ubungo, baada ya kuweka mzunguko wa mabati. Hakuna foleni.
Kumbe foleni ilikuwa inaletwa na yale mataa mabovu mabovu. Sijui kwanini hawakuweka mzunguko tangia miaka yote

Sent using Jamii Forums mobile app
kilicho ondoa foleni pale sio mzunguko bali ni watukutumia njia mbadala!
unakumbuka mzunguko wa pale kariakoo? vipi kuhusu mzunguko wa kigogo na m.city mbona bado kuna foleni??
mzunguko haujawahi kua dawa ya foleni zaidi watanufaikia mafundi garage maana watu ni full kupasuana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ile rentention wall ya lile daraja pale Mbezi mwisho nafikiri inahitaji kuangaliwa. Kama barabara itamaliziwa hivyo ilivyo kwa sasa na kwa mvua kidogo iliyonyeesha imeshusha udongo kiasi kile toka kwenye hilo barabara; basi uimara na uhai wake hautakuwa mzuri sana.

Pili ni aina au tuseme ubora wa lami inayotumika, ukiangalia hiyo round about na barabara ya pembeni kuelekea kwa wafanya biashara ndogo ndogo hapo Mbezi, lami iliyowekwa inaacha maswali mengi sana ikiwemo pia suala la ubora na uimara wake. Ubora wake unashabihiana na ile lami iliyowekwa kwenye daraja pale Mbezi ambayo tayari kwa muda mfupi wa magari kupita imeshaanza kupukutika.

Lengo la haya si kubeza bali ni waweze kurekebisha kabla ya hali kuwa ndiyo sivyo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tupo kwenye raiti traki

TANROAD!tanzania karibu sekta nyingi ni hovyo tu.hapa kigoma kuna sehemu wanataka wawekewe nguzo za umeme ili wapate huduma hiyo umbali wa mita chache tu lkn majibu waliopewa na meneja wa tanesco kigoma ni ya hovyo sana.sehemu yenyewe ni kazegunga na zinahitajika nguzo kama sita tu na wateja wako kibao lkn wameambiwa kupeleka nguzo sita labda kiwe kiwanda ndo ingekuwa sawa lkn kwa mtu mmoja mmoja haiwezekani.juzi tu wameiomba serikali ati iwalipie Tillion 1.39 wanazodaiwa na watoa huduma.hiyo inaingia akilini?je hao tanesco wamesoma biashara?hao ndo kama TANROAD barabara wanazojenga hazikizi vigezo kabisa.kabla barabara haijaisha nyuma vinaanza kuwekwa viraka na wizara inaona sawa tu.ranroad ni wapigaji tu na wala hawakemewi.ten pasenti za wazabuni zimewalevya na zinawafanya waishi kama wafalme hata wengine wanapolia njaa wao huwaona wenzao kama wajinga wasiojua kutafuta pesa.
 
Back
Top Bottom