Kina dada, kwani kuolewa ni lazima?

Kuna ukweli ambao binafsi nimeuona kwa shemeji yangu naye ishi nae, yaani amekata tamaa ya kuolewa wakati yupo 24 age. Sasa hv amekuwa muumini mzuri sana wa kanisa. kapoteza kabisa kujiamini lakini najitahidi kumshauri asione kama kuolewa ni kila kitu na nashukuru ameanza kubadili mtazamo huo potofu.
 
pressure ipo,hata kwa wanaume..
Kupata mume au mke sio kazi ndogo
ila haileti maana unaolewa ukiwa 22 na divorce at 25,.
Umri ni moja tu ya vitu vya kuangalia,ila sio the only thing..
 
kuwa na gf mwenye umri kuanzia miaka 25 na kuendelea ni presha tu ya kutaka umuoe..! ndo maana watu tunakimbilia wakusoma..! mkikaa kidogo tu...! UNAMPANGO GANI NA MIMI..? looooooooo
Hizo tumekutana nazo sana, lakini kwa age hiyo kuna kaukweli kidogo kwa kuwa katika umri huo mtu anakuwa amemaliza majukumu mengi ya kielimu na anaangalia hatima yake ya maisha (hii ni both kwa wanaume na wanawake though kinadada wanakuwa makini maana ukimlamba usije ukaangia mitini) lakini pia si kwamba wanapenda kuolewa bali wanachotaka wakati mwingine ni kukuelewa mtazamo wako katika mahusiano yenu kama kweli ni mwanaume reasoning au vipi, majibu yako ndio yatafanya uhusiano wenu uendelee hata kama hutamuuoa. ( hapa ni katika kulinda heshima yake kwani mara nyingi jamii zetu bidada akiwa na wanaume watatu katika interval fupi watu wanamwona hajatulia lakini the same ikitokea kwa mwanaume inaonekana poa, kwahiyo hiyo ni part of screening na ndio maana kuna bidada wengine itakuchukua wiki kadhaa kutembea nae though ameonyesha kukubali). Kuna majibu mengine ukiyatoa mara moja anaingia mitini si kwa kuwa umemwonyesha kwamba hutamuuoa bali anakuona kama haupo organized kiasi kwamba mnaweza mkawa mnajadiliana issue mbalimbali in the course of your relationship (hii ni kwa wadada makini maana kuna wengine wao bora twende)
 
ukute we ni sista wangu make hapo rocky city nina ndg kibao teh teh teh..................eti nikimbilie ndoa kisa umri umeenda loh charminglady ntaingia huko nikiamua na kuona sasa ninahitaji kukaa nyumbani na mtu as husband and wife haijalishi niko 22,25 or 30,40 ilimradi nimeridhia toka moyoni maana ndoa ni kijiba cha roho.

Safi sana my invisible sis....... :teeth:
 
Pressure ni kubwa coz wengi wanahofu jamii kuwachukulia vibaya na pia wanahofu kupoteza mvuto kabla hawaajaolewa hivo wana pressure kweli
 
mutu kaolewa mume yake tajiri sana huyo muke yeye hafanyi kazi na hata kijiraum hana anapigwa na jua kazi yake kupika muchuzi na chapati zilizoungua.
Kwenye handbag hata kijilaki hana kazi yake kuagiza migalaxy.
Mama yake anashida sana hamsaidii.
Huyu kaolewa kaajiriwa kuzaa na kupika muchuzi au ni mutumwa?
 
Hahahaha. Yaani nimecheka utasema mazuri!
Sasa anaunguza chapati akiwa busy anafuatilia 'mchezo' ama bongo movie?
Hahahaha, you made my day.

Sumu ya ndoa bwana ni ugolikipa. Financial dependency is a No-Go zone kwenye mahusiano hata ya kindugu!
 
Kama utakuwa unakaa na kidiscuss maisha anayoishi mwenzako daima utabaki hapo hapo huku mwenzako akiendelea kufanikiwa siku hadi siku.

Kwani umeambiwa kukaanga chapati siyo kazi? Chamsingi ni jinsi gani mtu huyo anaweza kubalance faida yake anayoipata katika hicho kidogo anachokipata.

Unaweza ukawa unalipwa million 3 kwa mwezi lakini usiwe na mafanikio yoyote yale, ukaishia kuponda mali wakati mwenzio anayepata faida ya sh.15000 kwa kila siku ila akawa amepiga hatua ile mbaya.

Tunachoangalia hapa ni jinsi gani huyo mtu anavyoweza kuipangilia pesa yake anayoipata.
 
mutu kaolewa mume yake tajiri sana huyo muke yeye hafanyi kazi na hata kijiraum hana anapigwa na jua kazi yake kupika muchuzi na chapati zilizoungua.
Kwenye handbag hata kijilaki hana kazi yake kuagiza migalaxy.
Mama yake anashida sana hamsaidii.
Huyu kaolewa kaajiriwa kuzaa na kupika muchuzi au ni mutumwa?

Wewe ni Mnyarwanda?
 
Back
Top Bottom