TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
- Thread starter
- #21
simply, tanzania daima ni gazeti la mbowe na chadema yake, kwa hiyo habari utakazozikuta hapo ni za kuipamba chadema tu. Nilikuwa nikinunua sana kipindi cha nyuma lakini kilichokuwa kinanisumbua ni jinsi ya kuchuja habari, kwani si zote ni za kweli zingine ni porojo tu. Niliona napoteza muda kwa hiyo binafsi siku hizi nimeshaachaga kununua kwani kupoteza pesa tu. Mara nyingi huwa nasomaga mwananchi kwani ni mara chache tu huwa linaegemea chadema. Pia yanayoegemea CCM huwa sinunui kwani, ni kama tanzania daima ambapo habari huwa zimechakachuliwa.
Sasa hivi ukitoa mwanchi huwa nanunuaga mwanahalisi japokuwa nalo limeanza kunibore kwani siku zote zimekaa kuisifia chadema tu na ile ladha halisi niliokuwa nikiipata imeshaanza kupotea.
Nakumbuka kama wiki 3 zilizopita nilikuta title; nasema mapema siichagui CCM, kuja kusoma muandishi eti yeye ni mwalimu na anaishi canada. Nilishangaa sana. Soon hata gazeti la mwanahalisi nitaachana nalo, nitabaki na mwananchi tu.
That means wako biased na wanapindisha maadili ya uandishi wa habari.Sasa mbona bado maadili hayo hayo yakikiukwa na vyombo vingine vya habari wanalia?????