Kimetokea nini Tanzania Daima?

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Mbona wanazipa uzito habari za Chadema peke yake???Au ndo mvutia kamba???Kama ni hivi na tusimlaume mtu si ndio?
 
Kweli nmeamini unakaa tandalee tena kwa mtogole au uwanja wa fisi, manake maswali yako ni ya kitandaletandale keep it up
 
Kweli nmeamini unakaa tandalee tena kwa mtogole au uwanja wa fisi, manake maswali yako ni ya kitandaletandale keep it up

Junior Member,good.Unakuja kujibu maswali ya msingi.Maswali yangu yanaelekea kwenye maswali ya nyongeza.Jibu hilo then tuendelee.
 
Upuuzi gani huu? Hawa jamaa wanawatumia hata ma-tabula rasa! Kweli wameshikwa pabaya!
 
Mbona wanazipa uzito habari za Chadema peke yake???Au ndo mvutia kamba???Kama ni hivi na tusimlaume mtu si ndio?

Ndugu TandaleOne (Mchakachuaji) Kimetokea nini Mtanzania, Rai, Uhuru, Habari Leo Mbona wanazipa uzito habari za kashfa za Mgombea wa Chadema peke yake?

Waandishi makini hawawezi kuandika kashfa za mtu. Soma kwa makini Tanzania Daima utapata jinsi sera za CCM zinavyojibiwa na za Chadema zinavyouzwa. Sidhani kuwa na wewe ni kilaza kama Ma"rope"
 
Changiani hoja ki tanzania "kupingana bila kupigana" kwani mkikashifiana hamtafika kokote na badala yake mtaacha hoja ya msingi mtaanza kuangaliana makovu ya uso. Forum hii inaendeshwa na wapenda nchi sio wala nchi hivyo ingekuwa vyema kama itatumika kwa maslahi ya taifa zaidi ya kuwa kijiwe cha micharuko.
Ni uhuru wa kutoa maoni ulionipelekea kuchangia hivyo, tuendelee na mwaka wa siasa!
 
Naomba niulize swali:Hivi ni kinamtofautisha mpenda nchi na mla nchi???Nafsini mwao.?
 
Upuuzi gani huu? Hawa jamaa wanawatumia hata ma-tabula rasa! Kweli wameshikwa pabaya!

Mkuu naomba nitoa tafsiri kwa neno lenye red!
Akili ya mtoto aliyezaliwa leo huwa haina kitu, yaani Empty, hiyo ndo tabula-rasa
 
Upuuzi gani huu? Hawa jamaa wanawatumia hata ma-tabula rasa! Kweli wameshikwa pabaya!
Badala ya CCM kutafuta watu wenye uelewa wanatuletea ma-tabula rasa watu kama Malaria Sugu na TandaleOne, imekuwa badala ya wao kuleta hamony kwa wanajamii wakipende chama sasa ndio wamekuwa wavurugaji na kufanya kichukiwe zaidi.

Akili ya CCM ni moja kujaza watu kwenye mikutano wanafikiri itafanya kazi humu JF kwa kutujazia ma-tabula rasa tupu. Kazi yangu ni simple kila atakaye fungua thread ya ma-tabula rasa atakutana na ujumbe wa video hii,

Last edited by a moderator:
Mbona wanazipa uzito habari za Chadema peke yake???Au ndo mvutia kamba???Kama ni hivi na tusimlaume mtu si ndio?

Ukitaka habari nzuri za Chadema soma Tanzania Daima na Mwanahalisi na ukitaka kuzijua weakness zao Soma Rai, Habari Leo na Mtanzania na kinyume chake kwa CCM, ukitaka news ambazo ziko balanced soma Mwananchi.
 
simply, tanzania daima ni gazeti la mbowe na chadema yake, kwa hiyo habari utakazozikuta hapo ni za kuipamba chadema tu. Nilikuwa nikinunua sana kipindi cha nyuma lakini kilichokuwa kinanisumbua ni jinsi ya kuchuja habari, kwani si zote ni za kweli zingine ni porojo tu. Niliona napoteza muda kwa hiyo binafsi siku hizi nimeshaachaga kununua kwani kupoteza pesa tu. Mara nyingi huwa nasomaga mwananchi kwani ni mara chache tu huwa linaegemea chadema. Pia yanayoegemea CCM huwa sinunui kwani, ni kama tanzania daima ambapo habari huwa zimechakachuliwa.
Sasa hivi ukitoa mwanchi huwa nanunuaga mwanahalisi japokuwa nalo limeanza kunibore kwani siku zote zimekaa kuisifia chadema tu na ile ladha halisi niliokuwa nikiipata imeshaanza kupotea.
Nakumbuka kama wiki 3 zilizopita nilikuta title; nasema mapema siichagui CCM, kuja kusoma muandishi eti yeye ni mwalimu na anaishi canada. Nilishangaa sana. Soon hata gazeti la mwanahalisi nitaachana nalo, nitabaki na mwananchi tu.
 
Back
Top Bottom