Kimenuka Bungeni Sakata la Trilioni 1.5, Wabunge Wasemeana Mbovu

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,353
2,137
Kimenuka! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mvutano mkubwa uliotokea Bungeni Dodoma leo na kusababisha mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga kuchemka kuliongoza bunge na kurudisha kijiti kwa Spika Ndugai.



Chanzo cha mvutano mkubwa uliotokea ni sakata la shilingi trilioni 1.5 zilizotajwa na CAG ambapo Mbunge John Mnyika alimtolea maneno makali waziri wa fedha na kumuita ni 'waziri wa fedheha', jambo lililosababisha kelele nyingi bungeni, Waziri Jenista Mhagama akasimama na kutoa mwongozo.

Baadaye, Halima Mdee naye alipigilia msumari na kusababisha Waziri Jenista Mhagama kuinuka kwa mara nyingine na kuwataka wabunge wafuate utaratibu.

Pia Mbunge wa Jang'ombe, akazidi kutibua hali baada ya kusema 'mbwa; wanaopiga kelele watolewe nje! Wabunge wa upinzani wakaliamsha dude na kusababisha hali iwe tete mjengoni. Mwenye updates zaidi...

Nawasilisha.

====

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amewataka Wabunge kutojadili suala la Trilion 1.5 ndani ya bunge kutoka kwenye ripoti ya CAG hadi kamati ya PAC itapowasilisha ripoti yake,ametoa kauli hiyo baada ya Mbunge Mnyika,kusimama na kuihoji Serikali kuhusu fedha hizo

Habari zaidi...

Dodoma. Wabunge wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na John Mnyika (Kibamba) wamemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kuwaeleza Watanzania Sh1.5 trilioni zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ziko wapi.

Wakizungumza leo Juni 5 bungeni, wabunge hao wamemtaka CAG kufanya ukaguzi maalumu wa fedha hizo na deni la Taifa huku wakisema kama Dk Mpango ameshindwa kuongoza wizara hiyo ni bora akajiuzulu ili asiwe waziri wa fedheha.

Hoja hiyo imeibua mvutano bungeni kati ya wabunge hao, Waziri Mpango na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwazuia kujadili ripoti hiyo ndani ya Bunge.

Akianza kuchangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya wizara ya fedha na mipango ya mwaka 2018/19, Mnyika amesema waziri wa fedha, Dk Mpango na taasisi zilizo chini yake, zinaandika barua kwamba mtu fulani asipewe msahama wa kodi halafu mlango wa nyuma anakwenda kutoa msamaha, kama sio fedheha ni nini?

Kauli hiyo ilimnyanyua, Dk Mpango ambaye alisema;

“Mheshimiwa Mwenyekiti (wa Bunge- Najima Giga) naomba(Mnyika) athibitishe hilo.”

Mnyika akiendelea kuchangia amesema kumekuwa na kawaida wizara ya fedha kutoa kauli humu bungeni zinazokinzana.

“Aprili 20, 2018 Naibu waziri wa fedha (Dk Ashatu Kijaji) alitoa kauli humu bungeni kuhusu utata wa Sh1.5 trilioni ambazo hazijulikanani zimeenda wapi. Akasema Sh209 bilioni zimepelekwa Zanzibar, nimefuatilia mjadala wa baraza la wawakilishi sijaona hilo, CAG achunguze na ufanyike ukaguzi maalum,” amesema Mnyika.

Baada ya kutoa kauli hiyo, Waziri Mhagama amesimama na kusema; “Kauli za mawaziri, huwa hazijadiliwi bungeni, ninaomba nisisitize kauli za mawaziri hazijadiliwi bungeni.”

Waziri Mhagama amesema ripoti za CAG zitajadiliwa ndani ya Bunge mara baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuijadili na kuwasilisha taarifa yake ndani ya Bunge.

“Kwa hiyo hapa ndani ya Bunge tutaenda na kanuni na kama ni kujadili nje ya bunge wako wabunge wengine watalijadili,”amesema.

Baada ya kumaliza, kelele ziliibuka kutoka upinzani wakipinga huku Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga akimtaka Mnyika kuendelea kuchangia.

“Lazima CAG akalifanyie uchunguzi maalumu suala la Sh 1.5trilioni na kuhusu vile vifungu namba 22 kuhusu deni la Taifa,”amesema Mnyika

Kwa upande wake, Mdee amesema taarifa ya CAG ni halali kwa wabunge kulijadili.

Mdee amesema Waziri Mpango anatakiwa ajibu hoja kuhusu Sh1.5 trilioni na Sh200 bilioni zilizotajwa kupelekwa Zanzibar ni zipi?

Hata hivyo, Spika Job Ndugai alimtaka Mnyika kujiandaa kuthibitisha hoja yake kuhusu Dk Mpango kuzuia msamaha wa kodi.

Chanzo: Mwananchi
 
Kimenuka! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mvutano mkubwa uliotokea Bungeni Dodoma leo na kusababisha mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga kuchemka kuliongoza bunge na kurudisha kijiti kwa Spika Ndugai.

Chanzo cha mvutano mkubwa uliotokea ni sakata la shilingi trilioni 1.5 zilizotajwa na CAG ambapo Mbunge John Mnyika alimtolea maneno makali waziri wa fedha na kumuita ni 'waziri wa fedheha', jambo lililosababisha kelele nyingi bungeni, Waziri Jenista Mhagama akasimama na kutoa mwongozo.

Baadaye, Halima Mdee naye alipigilia msumari na kusababisha Waziri Jenista Mhagama kuinuka kwa mara nyingine na kuwataka wabunge wafuate utaratibu.

Pia Mbunge wa Jang'ombe, akazidi kutibua hali baada ya kusema 'mbwa; wanaopiga kelele watolewe nje! Wabunge wa upinzani wakaliamsha dude na kusababisha hali iwe tete mjengoni. Mwenye updates zaidi...

Nawasilisha.
Kumbe bado mpo mnaofuatilia bunge? Mna moyo.
 
lakini kuna la kujifunza sisi kama raia wa kawaida maana kuna msemo kuwa eti sisi ndiyo tunawapa ajira hawa wabunge kwa maana wanalipwa kwa kodi zetu kwa ajili ya kazi ya kutunga sheria lakini ili kuwa mbunge unatakiwa kujua kusoma na kuandika kwa lugha ya kiswahili tu inatosha na hapohapo wao wanajipangia mishahara wenyewe ,kwa maana hiyo mtu ambaye ameishia std III anaweza kuwa na mshahara zaidi ya Professor? Je kweli huyo mhadhiri wa chuo anaweza kweli kufanya tafiti za ukweli za kusaidia serikali ambaye ndy mtendaji mkuu wakati mshahara wake ni mdogo na anazidiwa na mtu ambaye anajua kusoma na kuandika tu?
Wananchi inabidi tubadilike kwanza sisi kwa kusema hapana kwa hili la kuwa na mbunge ambaye anatakiwa kujua kusoma na kuandika tu wakati hata dereva wake anatakiwa kuwa wa kidato cha nne
Maendeleo ya nchi yeyote duniani hayaletwi na mtu mmoja lazima kila raia kupamabana na kusema ukweli ili kuboresha ili tuweze kuleta maendeleo kwa pamoja
Wabunge lazima sisi kama raia wa kawaida tuweze kuwatuma Bungeni nini mahitaji yetu lkn kwa sasa kila mbunge akishashinda uchaguzi ndy basi tena mpaka wakati wa uchaguzi tena sasa kunakuwa hamna la maana katika uwakilishi
Tukiwa na wabunge waelewa kwa ujumla wake lkn simaanishi kuwa wote siyo waelewa HAPANA ila kipengele cha kujua kusoma kuandika na wao kulipwa mishahara mikubwa kuliko watumishi wengine siyo haki kabisa na kinafanya wahadhiri wetu kukimbilia kwenye Ubunge na kuacha taaluma zako ambazo zinatakiwa kusaidia vijana wetu
 
huwa mnajulia wapi hayo, au mkuu na wewe ni mbunge ulikuwep.
bungegiza lidumu wawe wanamalizana hukohuko tu sisi huku tuachwe tuendelee na ligi zetu za jf.
Nahisi amepata muhtasari mengine ameongeza kwa utashi wake.

Ndio watanzania tulivyo ata kama haupo kwenye eneo la tukio basi tunajiongeza tu.
 
Nahisi amepata muhtasari mengine ameongeza kwa utashi wake.

Ndio watanzania tulivyo ata kama haupo kwenye eneo la tukio basi tunajiongeza tu.
Mkuu unataka kusema nimeongeza chumvi ili kunogesha mjadala? Hujui hilo ni kosa kisheria? Exageration!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom