Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Tuanze kufikiria pia kilimo cha umwagiliaji. Maji ni mengi sana hapa TZ chini ya ardhi na hayatumiki vilivyo. Hii ndiyo njia pekee ninayoona itakayoitoa nchi hii kwenye huu MKWAMO tuliomo.

Kilimo cha umwagiliaji na kilimo cha ndani kwa ndani au greenhouse farming ndiyo the only way out of this poverty ACHANA NA PROPAGANDA ZA KILIMO KWANZA! Hayo ni masango tu ya politicians.
 
chonde chonde kaka,usizilete hizo mbegu,it may cause GM contamination,wasiliana na wataalam wa kilimo watatoa ushauri mzuri.ila bora uziache huko huko,hizi za kwetu ni poa sana tu.
wajapan wametengeneza watermelon la square kama box ili iwe rahisi kusafirisha matunda hayo,Mh! madhara yatajulikana baadae,ktk cancer na magonjwa mengineyo.
Umechanganya mambo mkuu,

GM na mbegu za norh ni vitu viwili tofauti, GM nyingi hazia mbegu, kinachohofiwa ni diseases na sio gm

Kwa mleta mada, bado nimeexperience faida ndogo sana kutokana na magonjwa, wadudu, maji nk.
pnadhani it is jot as simple as you presented

thanks to ramthods for h useful comment as well
 
Mbegu zinapatikana wapi mimi nataka kujaribu kulima hapa nyumbani naitaji mbegu ilinifanye kilimo hicho
 
Asante sana mkuu kwa kutupa ujuzi,,mimi nipo Arusha nataka kujaribisha hichi kilimo cha matikiti kwenye shamba ambalo lipo maeneo ya Oljoro na ni zaid ya ekari 2 na pia lina kisima na pump ndani yake kwa hiyo maji hayatakuwa shida, ninachopenda kujua ni vitu vifiutavyo

1,Je kwa siku moja natakiwa kumwagia maji kiasi gani kwa kila mche

2,Mbegu bora kwa maeneo ya Arusha zitakuwa zipi

3,ni wakati gani unafaa kuanza kilimo i.e miezi ipi

4,na upatikanaji wa soko lake huku Arusha lipoje kama una uzoefu

Thanx in Advance
 
Mimi nalima aina ya Sugar baby inachukua siku 60 tu kuvuna tangu plus siku 3-5 za kukaa ardhini, kwa hiyo kwa mwaka nalima mara 4 tu nina ekari 5 na kila eka napata kuanzia 2M-3M.

Spacing ni 2mx2m na kila shimo naweka mbegu 2 ambazo zinazaa matunda 2-3 kwa maana kila shimo napata matunda 4-6 ( wastani matunda 5).

Hivyo kwa spacing hiyo napata mashimo 1000-1200

Idadi ya matunda: Mashimo x Matunda kwa shimo x ekari [1,000 x 5 x 5 = 25,000]

Mapato: wastani wa shilingi 500 kwa tikiti x idadi ya matikiti kwa eneo la ekari 5 [25,000 x 500 = 12,500,000]

Mapato kwa mwaka: 12,500,000 x 4= 50,000,000

Gharama za uendeshaji wa shamba ni Tsh 25,000,000

Faida Kuu ni Tshs 25,000,000 M.

Tujenge taifa letu kwa kilimo
Mimi pia nataka kujaribu hiki kilimo, tafadhari niambie wewe unazalisha sehemu gani? Ni maeneo ya Pwani?

Kama ni Pwani, je huwa unapanda mwezi wa ngapi? Unatumia kilimo cha umwagiliaji au cha kutegemea mvua? Nataka pia kulima matikiti maji huko Mkuranga.
 
Edmund

Mkuu umemaliza yote. Sina cha kuongeza.

Hiki ndicho kilimo cha matikiti maji..Tofauti ndogo ni mimi huwa naanza kuvuna siku ya 54.

Tulijenge taifa kwa Kilimo!

Asante sana mkuu kwa taarifa yenya hamasa, ninapenda kujua kuhusu soko la matikiti, hakuna tatizo la ukosefu wa soko?
 
Wakubwa mimi nina swali moja, jee mbegu kutoka north america zinaweza kumea vizuri hapa nyumbani?

Uwe makini, kuna siku nilkuja huko nikaktua matikiti makubwa na matamu ajabu ktk Fleas Market ama kitu kama hicho, nilitaka kukununua mbegu lakini walinieleza kuwa siruhusiwi kama siyo mmarekani mwenzao, pia Airport niliulizwa kama nimebeba kitu kama hicho ama jamaa yeyote kanipa hela niwapelekee jamaa zao home.
 
KAKA HII HABARI UMETOA HAIKO SAHIHI husasan unaposema unapanda kwa umbali wa 2 by 3 metres halafu unapata mashimo 1000. hicho kitu hakipo since one acre ina 70 by 70 metres na surface area ya 4900 meter squared. kama unapanda kwa 2 by 3m, utakua na mashimo 575 tu katika acre moja. this means kama unapataga matunda matano kwenye shimo moja basi utapata 575*5*5= 14375 manke utakua na mashimo 575. iyo inamaanisha utapata matunda 14375 kwa acre tano, kulingana na bei yako ya kuuzia shamba sh mia tano ambayo utakua ulipunjwa sana, manake tikiti moja bei shamba ni buku dsm, hata mikoani. revenue yako itakua 14375*500= 7187500 tsh only, or lets say 7200000. kitu kingine u realy have to explain inakuaje unatumia million 25 kulima na kumwagilia kwa mwaka mmoja. wakati sisi tunatumia just 2. mil kulima acre tano izo izo kwa msimu, kwa mwaka roughly 10 million. hebu tuelezee kuhusu garama zako, manake naanza kuhisi untaka kukatisha watu tamaa ya kulima hayo matunda

WANAOJUA, 1 by 1m space kutoka kwenye mmea mmoja mpaka mwingine. that means kunakua na mashimo 4900 kwa acre. kama target ni kupata matunda matatu makubwa kila shimo then tunfanya simple calculations 4900*3= 14700 fruits per one acre. fanya iyo times the market price ya shamba ambayo ni buku revenues inakua 14700000 ( forteen million tsh). iyo forteen milion toa garama ya 250,000 tsh ya kuhudumia iyo acre moja kuanzia unapopanda, palizi, DAWA, ulinzi, mbegu, trekta, harrow, kila kitu mpaka kuvuna.
 
Mimi nililima matikiti maji wakati wa kiangazi kwa mbegu ambazo ni hybrid na ninaweza kushare uzoefu wangu kama ifuatavyo;

  1. Haya matunda yanashambuliwa sana na Fungi aina ya Powdery Mildew. Inafikia wakati unakuwa unapiga zile broad spectrum fungicides hadi weekly ili kupambana na huu ugonjwa maana unasababisha matunda kuoza wiki moja tu baada ya fruit set. Mbegu ya Hibrid inazaa sana lakini matunda mengi yalikuwa yanaoza kutokana na tatizo la fungi
  2. Kuna Aphids walinisumbua sana. Wakulima tunapenda kuwaita sisimizi weusi lakini mtaalam akaniambia kuwa hawa ni aphids. Wana tabia ya kunyonya kwenye stems, ukizembea siku mbili tu unakuta mmea mzima wa tikiti maji unakaribia kukauka. Ilikuwa ni challenge kubwa kukabiliana nao na mtaalam aliniambia kwa kuwa ni kiangazi njia pekee ya kukabiliana nao ni dawa. Kumbuka aphids huwa wanakufa kukiwa na mvua hivyo hawasumbui sana wakati wa mvua
  3. Matunda yalipoanza kukomaa nikakumbana na fisi waliokuwa wanaibuka usiku, nyani waliibuka siku moja na pia binadamu walikuwa wanaiba, tena majirani zangu wa shambani. Kwa kuwa nilikuwa nimeambiwa hizi changamoto nifanikiwa kufense shamba langu kwa wakati muafaka na pia nilikuwa na ulinzi mzuri. Kwa mkulima anayeanza lazima ajiandae kukabiliana na haya matatizo
  4. Changamoto nyingine kubwa ilikuwa kwenye mauzo. Ingawa nilitoa matunda yangu wakati ambao sio watu wengi walikuwa nayo na nilikuwa na strategy ya kuuza kidogo kidogo na kwa bei ya soko hasa kwa kutarget watu wenye mahoteli na migahawa kuna kipindi nikalazimika kuwapelekea wanunuzi wa jumla wanaouzia sokoni. Nilimpelekea jamaa sample, bahati nzuri nilishauriwa nisiwakaribishe kabisa shambani kwa kuwa wakiona idadi ya matunda uliyo nayo wanapanga mbinu za kukufrustrate uuze bei poa. Baada ya kumpa jamaa sample ya matunda mawili makubwa, (average weight ya matikiti yangu ilikuwa 4kg but kuna yaliyofika 7 Kg na nilijitahidi kupima yale matunda makubwa zaidi) akaniambia nimpelekee kwa bei ya 1,500 kwa tunda. Nilipopeleka Pick Up yangu imejaa matunda jamaa alikuwa na visingizio kibao tukashuka bei hadi 1,300 kwa tunda na siku hiyo nilibeba 200 tu. Nilipopeleka mara ya pili akashuka hadi shs 800. Nikaacha kupeleka sokoni nikawa nauza moja kwa moja mahotelini, migahawani na kwa majirani kutokana na order but siku ukiuza sana ni matikiti 50. Kabla ya kupanda kama hauna uhakika na soko ni vizuri kupanda kidogo kidogo, let say kila baada ya siku 7 hadi 10 unapanda nusu hekari au hekari moja kama una shamba zaidi ya hekari 3. Hii itakusaidia kutoivisha matunda mengi kwa wakati mmoja, ingawa utakutana na mengine ambayo yatakomaa wakati bei sio nzuri sana, kama unauza kwa watumiaji moja kwa moja bei sio ishu
  5. Uzalishaji sio mkubwa kama watu wanavyoongelea theoreticaly. Kuna tatizo kubwa la fruit set kwenye haya matunda na inashauriwa kama una nafasi weka mizinga ya nyuki shambani wasaidie pollination. Nilipanda miche 2000 kamili tena kwa kuhesabu, ikakomaa miche 1700 na idadi ya matunda yaliyofika sokoni ni kama 2500 (Kila mche ulizaa tunda moja au mawili yaliyokomaa na kufika sokoni ingawa kulikuwa na maua yenye matunda hadi 12 kwa mche) tu kutoka shamba zima na nilikuwa nauza kwa kati ya shs 2000 na 3500 ukiondoa zile Pickup mbili zenye matunda kama 400 nilipeleka kwa walanguzi. Gharama za uzalishaji hazikufika 1M but faida yote ilikuwa ni kulipia uwekezaji kwenye fensi.

Nimefuatilia mawazo ya watu wengi humu wanatoa uzoefu wa kwenye vitabu au wanavyowashauri wakulima. Uzuri wa ushauri wa humu unakupa mtu hamasa kujaribu, which is a good thing na baada ya kupata challenges kama mimi unakuwa determined kufanya vizuri next time.

Nitafurahi mkulima mwingine akinipa ushauri wa vikwazo nilivyokutana navyo maana huenda ni poor practice na best practice huwa inapatikana kwa ku-benchmark kwa wakulima wenzio wanaofanya vizuri. Next time target yangu ni kuhakikisha angalau matunda manne kwa mche mmoja yanafika sokoni badala ya moja hadi mawili niliyopata mwaka jana.
 
KAKA HII HABARI UMETOA HAIKO SAHIHI husasan unaposema unapanda kwa umbali wa 2 by 3 metres halafu unapata mashimo 1000. hicho kitu hakipo since one acre ina 70 by 70 metres na surface area ya 4900 meter squared. kama unapanda kwa 2 by 3m, utakua na mashimo 575 tu katika acre moja. this means kama unapataga matunda matano kwenye shimo moja basi utapata 575*5*5= 14375 manke utakua na mashimo 575. iyo inamaanisha utapata matunda 14375 kwa acre tano, kulingana na bei yako ya kuuzia shamba sh mia tano ambayo utakua ulipunjwa sana, manake tikiti moja bei shamba ni buku dsm, hata mikoani. revenue yako itakua 14375*500= 7187500 tsh only, or lets say 7200000. kitu kingine u realy have to explain inakuaje unatumia million 25 kulima na kumwagilia kwa mwaka mmoja. wakati sisi tunatumia just 2. mil kulima acre tano izo izo kwa msimu, kwa mwaka roughly 10 million. hebu tuelezee kuhusu garama zako, manake naanza kuhisi untaka kukatisha watu tamaa ya kulima hayo matunda

WANAOJUA, 1 by 1m space kutoka kwenye mmea mmoja mpaka mwingine. that means kunakua na mashimo 4900 kwa acre. kama target ni kupata matunda matatu makubwa kila shimo then tunfanya simple calculations 4900*3= 14700 fruits per one acre. fanya iyo times the market price ya shamba ambayo ni buku revenues inakua 14700000 ( forteen million tsh). iyo forteen milion toa garama ya 250,000 tsh ya kuhudumia iyo acre moja kuanzia unapopanda, palizi, DAWA, ulinzi, mbegu, trekta, harrow, kila kitu mpaka kuvuna.

mkuu

haupo sahihi kabisa .... rekebisha hesabu zako tena

1 acre = 4046 sqm (square meters)

one acre ni sawa na approximate 70x70 yards na siyo meters
 
MI napenda sana hicho kilimo na drip irrigation, niambieni inakuwaje? kuhusu gharama za uendeshaji wa shamba kwa heka ni kiasi gani? mashamba yanapatikana wapi, na masoko yake yakoje? simu yangu ni 0768 417121, na 0713 658618 ni mgeni sana kwenye mtandao naomba msaada wenu.
 
Mimi nililima matikiti maji wakati wa kiangazi kwa mbegu ambazo ni hybrid na ninaweza kushare uzoefu wangu kama ifuatavyo;

  1. Haya matunda yanashambuliwa sana na Fungi aina ya Powdery Mildew. Inafikia wakati unakuwa unapiga zile broad spectrum fungicides hadi weekly ili kupambana na huu ugonjwa maana unasababisha matunda kuoza wiki moja tu baada ya fruit set. Mbegu ya Hibrid inazaa sana lakini matunda mengi yalikuwa yanaoza kutokana na tatizo la fungi
  2. Kuna Aphids walinisumbua sana. Wakulima tunapenda kuwaita sisimizi weusi lakini mtaalam akaniambia kuwa hawa ni aphids. Wana tabia ya kunyonya kwenye stems, ukizembea siku mbili tu unakuta mmea mzima wa tikiti maji unakaribia kukauka. Ilikuwa ni challenge kubwa kukabiliana nao na mtaalam aliniambia kwa kuwa ni kiangazi njia pekee ya kukabiliana nao ni dawa. Kumbuka aphids huwa wanakufa kukiwa na mvua hivyo hawasumbui sana wakati wa mvua
  3. Matunda yalipoanza kukomaa nikakumbana na fisi waliokuwa wanaibuka usiku, nyani waliibuka siku moja na pia binadamu walikuwa wanaiba, tena majirani zangu wa shambani. Kwa kuwa nilikuwa nimeambiwa hizi changamoto nifanikiwa kufense shamba langu kwa wakati muafaka na pia nilikuwa na ulinzi mzuri. Kwa mkulima anayeanza lazima ajiandae kukabiliana na haya matatizo
  4. Changamoto nyingine kubwa ilikuwa kwenye mauzo. Ingawa nilitoa matunda yangu wakati ambao sio watu wengi walikuwa nayo na nilikuwa na strategy ya kuuza kidogo kidogo na kwa bei ya soko hasa kwa kutarget watu wenye mahoteli na migahawa kuna kipindi nikalazimika kuwapelekea wanunuzi wa jumla wanaouzia sokoni. Nilimpelekea jamaa sample, bahati nzuri nilishauriwa nisiwakaribishe kabisa shambani kwa kuwa wakiona idadi ya matunda uliyo nayo wanapanga mbinu za kukufrustrate uuze bei poa. Baada ya kumpa jamaa sample ya matunda mawili makubwa, (average weight ya matikiti yangu ilikuwa 4kg but kuna yaliyofika 7 Kg na nilijitahidi kupima yale matunda makubwa zaidi) akaniambia nimpelekee kwa bei ya 1,500 kwa tunda. Nilipopeleka Pick Up yangu imejaa matunda jamaa alikuwa na visingizio kibao tukashuka bei hadi 1,300 kwa tunda na siku hiyo nilibeba 200 tu. Nilipopeleka mara ya pili akashuka hadi shs 800. Nikaacha kupeleka sokoni nikawa nauza moja kwa moja mahotelini, migahawani na kwa majirani kutokana na order but siku ukiuza sana ni matikiti 50. Kabla ya kupanda kama hauna uhakika na soko ni vizuri kupanda kidogo kidogo, let say kila baada ya siku 7 hadi 10 unapanda nusu hekari au hekari moja kama una shamba zaidi ya hekari 3. Hii itakusaidia kutoivisha matunda mengi kwa wakati mmoja, ingawa utakutana na mengine ambayo yatakomaa wakati bei sio nzuri sana, kama unauza kwa watumiaji moja kwa moja bei sio ishu
  5. Uzalishaji sio mkubwa kama watu wanavyoongelea theoreticaly. Kuna tatizo kubwa la fruit set kwenye haya matunda na inashauriwa kama una nafasi weka mizinga ya nyuki shambani wasaidie pollination. Nilipanda miche 2000 kamili tena kwa kuhesabu, ikakomaa miche 1700 na idadi ya matunda yaliyofika sokoni ni kama 2500 (Kila mche ulizaa tunda moja au mawili yaliyokomaa na kufika sokoni ingawa kulikuwa na maua yenye matunda hadi 12 kwa mche) tu kutoka shamba zima na nilikuwa nauza kwa kati ya shs 2000 na 3500 ukiondoa zile Pickup mbili zenye matunda kama 400 nilipeleka kwa walanguzi. Gharama za uzalishaji hazikufika 1M but faida yote ilikuwa ni kulipia uwekezaji kwenye fensi.

Nimefuatilia mawazo ya watu wengi humu wanatoa uzoefu wa kwenye vitabu au wanavyowashauri wakulima. Uzuri wa ushauri wa humu unakupa mtu hamasa kujaribu, which is a good thing na baada ya kupata challenges kama mimi unakuwa determined kufanya vizuri next time. Nitafurahi mkulima mwingine akinipa ushauri wa vikwazo nilivyokutana navyo maana huenda ni poor practice na best practice huwa inapatikana kwa ku-benchmark kwa wakulima wenzio wanaofanya vizuri. Next time target yangu ni kuhakikisha angalau matunda manne kwa mche mmoja yanafika sokoni badala ya moja hadi mawili niliyopata mwaka jana.

Mkuu hatua uliyofikia ni kubwa sana huitaji kupunguza uzalishaji kwa kuhofia soko Bakresa anatoa bei nzuri sana kwa matikiti last time ilikuwa 800 TZS per kg ila ananunua minimum 250 tones so kama una eneo kubwa kacheki nao ustrike hiyo dili then uongeze uzalishaji
 
Mimi nalima aina ya Sugar baby inachukua siku 60 tu kuvuna tangu plus siku 3-5 za kukaa ardhini, kwa hiyo kwa mwaka nalima mara 4 tu nina ekari 5 na kila eka napata kuanzia 2M-3M.

Spacing ni 2mx2m na kila shimo naweka mbegu 2 ambazo zinazaa matunda 2-3 kwa maana kila shimo napata matunda 4-6 ( wastani matunda 5).

Hivyo kwa spacing hiyo napata mashimo 1000-1200

Idadi ya matunda: Mashimo x Matunda kwa shimo x ekari [1,000 x 5 x 5 = 25,000]

Mapato: wastani wa shilingi 500 kwa tikiti x idadi ya matikiti kwa eneo la ekari 5 [25,000 x 500 = 12,500,000]

Mapato kwa mwaka: 12,500,000 x 4= 50,000,000

Gharama za uendeshaji wa shamba ni Tsh 25,000,000

Faida Kuu ni Tshs 25,000,000 M.

Tujenge taifa letu kwa kilimo

Asante Edmund kwa ufafanuzi huu, lakini umeacha maswali mengi yasiyo na majibu.

1. Unalima wapi?

2. Hujaainisha mchanganuo wa hizo gharama za TZS 25,000,000/=. Unaweza kutuelezea zinatumikaje?

3. Hujaeleza kama kuna kodi zozote zile ambazo zinatozwa.

4. Hujaeleza kama unatumia kilimo cha umwagiliaji.

Asante. Kwa sasa ni hayo tu.
 
1) Mtaji unategemea na jinsi wewe mwenyewe unavyofanya kilimo chako, watu uliowaajiri n.k. Kwa mfano, kama unamwagilia inategemea unamwagilia na nini, pump ya mguu kama MoneyMaker au ya Petrol? Zote mwisho wa siku utapata faida tofauti. To be on the safe size, weka 1M hadi kuvuna. Ila inaweza ikazidi au ikapungua.

2) Matikiti yanachukua miezi miwili hadi kukomaa

3) Kama wewe ni mjasiriamali unapaswa kujua soko kabla ya kuamua kulima. So tafuta soko kwanza, then ndo uamue kulima.

4) Kipindi cha kipupwe ndio kizuri kwa matikiti maji. Matikiti maji hayapendi mvua nyingi. Yakipata maji mengi karibia na mavuno yanaweza kupasuka yakiwa shambani ukapata hasara.

5) Karibu Mkuranga tulime matiki. Ila maeneo mengi ya ukanda wa pwani ni mazuri kwa matikiti maji.

Hope that helps.

Nusu ekari nahitaji mtaji wa kiasi gani?
 
Nusu ekari nahitaji mtaji wa kiasi gani?

Mkuu,

Kwanza samahani sana kwa kuchelewa kujibu swali lako. Nimekua mvivu sana wa kuingia JF kutokana na kutingwa kwa shughuli za hapa na pale.

Kwanza kabisa nisingependa kukushauri silime nusu ekari, ni kidogo sana. Kama upo karibu sana na soko, basi haina shida, ila kama unaishi mbali na soko, kulima eneo dogo kunaweza kukufanya upate hasara kutokana na gharama kubwa ya usafiri.

Kadiri unavyokua na mzigo mkubwa, gharama kwa tonne (cost per tonne) ndivyo inavyoshuka na kukuwezesha kupata faida zaidi. Hivyo ukilima eneo dogo, gharama ya kusafiri itakuumiza.

Pili, gharama za kilimo zinategemea sana na aina ya kilimo unachofanya. Maswali ya kujiuliza ni kama ifuatavyo:

1. Je, unatumia kilimo cha kisasa au bora liende?
2. Je, unamtumia bwana shamba?
3. Hapo unapolima, unatumia trekta? Trekta lipo umbali gani toka shambani?
4. Unatumia mbolea ya namna gani? Mbolea inapatikana umbali gani toka shambani?
5. Hapo unapolima kuna vibarua wa kutosha wanaojua kuhudumia matikiti maji?
6. Eneo unapolima, hali ya uchumi ipoje? Hali ya uchumi ikiwa juu, gharama ya vibarua itakua juu pia.
7. Unafanya kilimo cha umwagiliaji au unategemea mvua?
8. Kama unamwagilia, je unatumia mashine ya aina gani? Au unamwagilia kwa mikono?

Na mambo mengineyo mengi.

Kwa ujumla, mambo kama hayo hapo juu hufanya maeneo tofauti kua na gharama tofauti. Hivyo uchaguaji wa eneo ni kitu muhimu sana kabla ya kuanza kulima.

Mimi nilishalima mkuranga mara kadhaa, na za kilimo kwa ekari zilikua around laki saba hadi nane.

Kama wahitaji kujua zaidi, niulize.

I hope that helps.
 
Mkuu,

Mimi nilishalima mkuranga mara kadhaa, na za kilimo kwa ekari zilikua around laki saba hadi nane.

Kama wahitaji kujua zaidi, niulize.

I hope that helps.

Mkuu, umesema humshauri kulima nusu ekari vipi ushauri wako kiwango cha chini eka ngapi zinatakiwa?

Binafsi ninampango wa kulima Mkuranga mwezi wa sita, gharama umesema ni around laki 7 -8 vipi kuhusu mavuno kwa ekari(yield per acre) na ulipanda kwa spacing gani.

Ni hayo tu mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom