Kilicho mpata Dr.Ulimboka ndiyo hali halisi itakayo wapata wengi kabla na baada ya 2015

Chaimaharage

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
211
78
Kutokana na hali ilivyo sasa ni bora wapenda mabadiliko wakaanza maandalizi mapema ili kukabliana na udhalimu ambao umeanza kujitokeza. Msidhanie walioficha mabilioni ya pesa Uswiss na maovu mengine watakuwa tayari kuona utawala unao walinda uanguke. Wako radhi hata kumwaga damu ili maslahi yao yasihujumiwe. Wanajua mkono wa sheria utakuwa juu yao baada ya anguko la utawala ambao wanatumia udhaifu wake kujikita mizizi ya unyonyaji.

Kutegemea sanduku la kura pekee halita tosha, ni budi kufanya maandalizi zaidi kuondoa udhalimu kwa sababu vyombo vya ulinzi na mahakama mwelekeo wake siyo mzuri. 2010 bilashaka mlishuhudia tume ya uchaguzi madudu iliyofanya. Mpaka tunafika 2015 hali itakuwa mbaya sana kwa wanaounga mkono M4C. Nchi yetu tunako elekea siyo muda mrefu tutaanza kushuhudia matukio ya ugaidi. Matukio ya aina hii hufanywa kama tunavyo shuhudia kwenye nchi nyingine na watu ambao wameona maisha hayana thamani tena kutokana na ugumu na kupoteza matumaini na wako radhi kujitoa mhanga ili kutetea haki za wanyonge.
 
Watanzania msilalamike! Mliyataka wenyewe!! Acheni serikali ifanye kazi yake! Hiyo serikali mnayoilalamikia mliiweka madarakani wenyewe. Mkatanguliza ushabiki wa Yanga na Simba katika siasa bila kujali uhalisia wa mambo. Sasa tulieni mnyooshwe vizuri hadi hapo mtakapopata akili 2015.
 
Watanzania walichagua chadema wenye mabavu wakasema hapana. Sasa risasi nje nje. Utawala wa mtu mjinga na dhaifu vs werevu wengi. Hali inaelekea mabadiliko. Hakuna chama kilicholeta mapinduzi duniani kisha kikaleta maendeleo ya kiuchumi.
 
Mimi naona tusiwe watu wa kuconferm kila kitu kwa kuhisi tuu. Sawa dr ulimboka alivamiwa akapigwa akaumizwa lakini naona tuangalie mambo matatu ndiyo tuyahisi na sio kukazania only serikali ndiyo itakuwa imefanya hivyo. Mambo hayo ni kama yafuatayo.
moja; may be serikali inahusika kutokana na huo mgogolo
mbili; labda dr ulimboka alikuwa na ugomvi na watu fulani labda kwa yeye mwenyewe kujua au kutokujua kuwa kuna mtu au watu wanamchukia so watu hao binafsi waliamua kutumia mwanya huu ili kumshambulia daktari huyu wakijua kuwa lolote litakalotokea sasa watu wengi watainyooshea selikari
tatu; labda kuna mtu au wtu waliopoteza ndugu zao wapenzi katika kipindi hiki cha mgomo so wameamua kulipa kisasi kwa mtu ambaye ni kinala wa suala hilo.

Kwa hiyo tukiwa ni watu wa kujchangia maada katika uwanja huu ni vyema tuthink big sio kufikiria tuu karibukaribu.
Ahsanteni
 
Chukua like zaidi..unafaa kufanya kazi ya upelelezi...ningekufahamu ningeku-suggest mahali.
 
hilo linajulikana long time.Utawala dhalimu hulewa na sifa,sifa zikipotea kuanza vitisho na baadaye kuadhibu, ila wapinzani wakiongezeka hukimbia.

Ni mfano wa mwanamume mbabe wa hela, na mwili ila hana mvuto kwa wachumba huwa wanachagua kuwapiga wapendwao na baadaye ikibidi mchumba.Hiyo ndio habari ya chama tawala kibaya, serikali mbaya,dini mbaya, watu wabaya,
 
kweli chadema wamevamia JF, lete habari zingine basi, hii issue mbona imesha chuja.
 
watanzania walichagua chadema wenye mabavu wakasema hapana. Sasa risasi nje nje. Utawala wa mtu mjinga na dhaifu vs werevu wengi. Hali inaelekea mabadiliko. Hakuna chama kilicholeta mapinduzi duniani kisha kikaleta maendeleo ya kiuchumi.
acha kuleta siasa kwenye maisha ya watu lazima ufikilie kwa hali ya juu sio kila kitu kikitokea moja kwa moja serikali. Tunavyo jadili mambo yanayohusu maisha ya watu tuziweke siasa pembeni uchadema, uccm, ucuf ukae pembeni msitumie kipigo cha ulimboka kufanyia kampeni
 
Back
Top Bottom