KILEMBA: Dhuluma/ uporaji/ unyang'anyi kwa wafanyabiashara wapangaji katika majengo ya Kariakoo

Kete Ngumu

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
6,644
6,830
Serikali au Wizara husika angazieni kwa kufuatilia uhujumu uchumi unaoendelea katika soko kubwa kabisa Tanzania la Kariakoo.

Utaratibu ambao sio rasmi ila unafuatwa upo hivi, Kariakoo kwa mtu anaetaka kuanzisha biashara. Kwanza kuonana na madalali na kuwaambia unataka kufungua biashara gani ili wakutafutie kwenye eneo linaloendana na biashara yako, namaanisha kama unataka kufungua duka la kuuza jeans za kiume basi kuna maeneo ambayo wafanyabiashara wa aina hiyo wapo ili muende sawa kibiashara hasa katika kupata wateja.

Ukishapata fremu unaambiwa kuna KILEMBA, hii kilemba ni pesa utakayoitoa aidha kwa mfanyabiashara anaekuachia hiyo frem au kwa mwenye nyumba, kiasi cha chini kabisa cha fremu ni kuanzia milioni 20-30 fremu za ndani na milioni 30-80 kwa fremu za nje yaani fremu zinazotizamana na barabara.

Pointi yangu ni hii, siku hizi kumeibuka wimbi la wenye nyumba kuwaondoa wafanya biashara wote katika nyumba kwa kigezo cha kukarabati nyumba na kutangaza KILEMBA kipya kwa anaetaka kurudi kwa uwiano wa hisabu ya kilemba ilioainishwa hapo juu.

Ikumbukwe kilemba sio kodi ya pango, unalipa kilemba na kodi ya pango unalipa. Wafanyabiashara wengi wameathirika na hili na wengine wamezifunga kabisa biashara zao kwa kushindwa kulipa kilemba kipya na kodi mpya kwa wakati mmoja.

Nyumba mbili zilizopo mtaa wa Raha na Mchikichi moja ilijengwa upya nyingine ikafanyiwa marekebisho kidogo tu na watu wote hao wakaumizwa.

Nyumba moja yenye underground inaweza kuwa na fremu zaidi ya 60 sasa ukizidisha kwa kilemba tu cha milioni 20 mara 60 unaona kabisa hawa wenye nyumba au wanaojiita wajenzi wanavyopata pesa nyingi kwa njia zisizo halali.

Serikali au wizara husika tafadhalini fuatilieni swala hili na hatua kali zichukuliwe kunusuru uchumi wa Taifa na familia kwa ujumla.
 
Ila wabongo wana upole wa kipumbavu mpaka wamekuwa wajinga.

Nchi hii CCM itatawala miaka 6000000.

Kuwa masikini nchi hii kama huna element za ucha Mungu ni kujitakia tu.
 
Nyie wenyewe kwa umoja wenu ndio mtaweza kulimaliza hili, bila ushirikiano mtaendelea kupigwa, mfano hai pale Urafiki mahakama ya ndizi kuna frame mpya zimejengwa na mtu binafsi japo eneo ni la kiwanda cha urafiki, mwanzo frame ilikuwa laki 7, malipo yote bank, watu wakagoma ikafika laki 5, wakataka kugoma walioharibu ni wamiliki wa mabus ya mikoani, walichukua kwa mpigo flame 10. Mambo mengine yanafanyika kutokana hatuna umoja, roho zetu zimejaa ubinafsi, unafiki, chuki na nidhamu ya woga. Kwa hilo serikali ni ngumu sana kuingilia.
 
Serikali ipi unayoishauri ifatilie,

Hii iliyowaacha Machinga kuzagaa mpaka njia za waenda kwa Miguu.

Hapo Kariakoo ni tatizo tena siyo dogo, Ukishamaliza kulipa Kilemba unalipa na kodi ya pango, ukishaweka bidhaa TRA nao hao hapo wanataka kodi yao mara sijui watu wa Uchafu nao hawachezi mbali. Mtapata wapi faida kwenye hizo biashara zenu. Hakuna Mwananchi mwenye furaha siyo Mfanyakazi, Mfanyabiashara, Mkulima ndiyo usiseme kote ni vilio tu Mkuu.
 
Mbona nasikia Kariakoo frame nyingi tupu watu wamefunga biashara? Kukubali kulipa 20m nje ya Kodi ya pango ina maana kuna uhitaji mkubwa wa frame. Kwa sehemu ambayo inasemekana biashara zimefungwa na frame nyingi tupu hili linawezekanaje?
 
Nyie wenyewe kwa umoja wenu ndo mtaweza kulimaliza hili, bila ushirikiano mtaendelea kupigwa, mfano hai pale Urafiki mahakama ya ndizi kuna flame mpya zimejengwa na mtu binafsi japo eneo ni la kiwanda cha urafiki, mwanzo flame ilikuwa laki 7, malipo yote bank, watu wakagoma ikafika laki 5, wakataka kugoma walioharibu ni wamiliki wa mabus ya mikoani, walichukua kwa mpigo flame 10. mambo mengine yanafanyika kutokana hatuna umoja, roho zetu zimejaa ubinafsi, unafiki, chuki na nidhamu ya woga. kwa hilo serikali ni ngumu sana kuingilia
Kibaya zaidi tunapotaka kukomalia jambo kwa umoja wetu kunaibuka wasaliti aidha wanaojipendekeza kwa mwenye nyumba au mjenzi na kuvujisha mchachotaka kufanya, likitokea hilo wengine wanahofia kukataliwa katika manyumba mengine kwa kupewa majina mabaya, umoja unakosa nguvu unajipata umebaki 1.

Binafsi nilikuwa muhanga ila niliwakomalia na mkwara mzito kwakuwa hawakuwa wakinijua kiundani wakanipa changu kwa siri.
 
Mbona nasikia Kariakoo frame nyingi tupu watu wamefunga biashara? Kukubali kulipa 20m nje ya Kodi ya pango ina maana kuna uhitaji mkubwa wa frame. Kwa sehemu ambayo inasemekana biashara zikefungwa na frame nyingi tupu hili linawezekanaje?
Fremu kweli zipo zinapatikana KIRAHISI tofauti na kipindi cha nyuma, kilemba cha milioni 20 pia ni rahisi kutokana na upepo wa biashara ulivyo mbaya. Uchumi wa Kkoo sio uchumi wa kipindi cha nyuma, mtu mmoja aliweza kuwa na maduka 2-4 lakini wengi wameyauza na kubakia na duka moja kama sehemu ya kupatia riziki ya familia.

Ni wengi ikifika kipindi cha kulipa kodi inamlazimu kupata pesa kutoka chanzo kingine kwaajili ya kulipa pango.
 
Mbona nasikia Kariakoo frame nyingi tupu watu wamefunga biashara? Kukubali kulipa 20m nje ya Kodi ya pango ina maana kuna uhitaji mkubwa wa frame. Kwa sehemu ambayo inasemekana biashara zikefungwa na frame nyingi tupu hili linawezekanaje?
Kuna mitaa ni hot cake hasa aliyotaja mleta mada ukiongozea Kongo na mchikichi.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom