Kilango amwambia waziri kasema uongo!

viongozi wetu legelege sana kwa nini hawaendi kwenye miradi na kuishuhudia wenyewe na badala yake wanakaa ofisini na kupokea taarifa ambazo wao hawajazithibitisha? mfano kuna waziri leo wakati akijibu moja ya maswali ya wizara yake amesema watendaji wengi ni wabadhilifu, je unategemea mtendaji mbadhilifu atakupa majibu ya kweli?tutaendelea kudanganywa sana kama hali ndiyo hii.

Nami nimejionea mwenyewe na Waziri kasema, Taarifa hizi ameambiwa na mkurungezi wake muda mfupi kabla ya kuingia mjengoni.

Nashukuru Waziri kakiri kuwa yeye hawezi kupingana na mbunge wa sehemu husika ila baada ya bunge watakwenda wote kujionea uhalisia. Inaonekana MAJIBU YA MJENGONI MENGI NI YA UONGO[/QUOTE]

Penye Ukweli kubali ukweli uishe nampa big up naibu waziri maana ndio democrasia unasema umeletewa habari zisizo na ukweli na ukakubali ila wengine wakiambiwa ni kubisha sasa kuna haja ya kureview majibu yote hata ya Waziri Mkuu kwani hujibu tokana na taarifa anazoletewa serikali inatudanganya kweli,

My Take;
Ni halali wananchi wakaandamana kuipinga serikali yao kwa muda mrefu imekuwa ikitoa taarifa za uongo nyingi tu

Na hiyo sheria yao wanayo taka kuwabana watu wasiandamane hatuitaki tena IGUNGA ndio iwe fundisho kwao kuanzia sasa.

Wana Magamba wenzake hawajamwambia afute kauli.? Manafiki sana mabunge ya Ccm.

hata kama amekili amendanganywa na mkurungezi hata yeye anahaju wajibu wake maana kwa wazir mwenye dhamana anatakiwa ajue nini kinaendelea hivyo hawajibiki kama inavyotakiwa

Mawaziri Wanapojibu maswali Mjegoni wajue wanapaswa kujibu ule ukweli si kusema ili mradi wamejibu Please Guys be serious it is a New Tanzania now with new generation not of that 47 years ago! Hey peopleeee get up!!!!

Leo katika kikao cha bunge cha maswali na majibu mbunge Anna Kilango Malechela amemwambia naibu waziri Agrey Mwanri kuwa kalidanganya bunge wakati akijibu swali kuhusu hali ya maji katika jimbo lake.

Waziri alijibu akisema kuwa visima vimejengwa katika vijiji ndani ya jimbo lake lakini mama Kilango alikuja juu na kupingana na majibu ya naibu waziri.

Sasa haya majibu yanayotolewa na mawaziri au manaibu waziri huwa wanayatoa wapi?

MAGOGONI.

Huyu Mama angekuwa ni wa kutoka upinzani LAZIMA angetakiwa atoe uthibitisho kwa maandishi haraka vinginevyo angetolewa nje.Swala la waziri kukiri kwamba hana taarifa zaidi ya mbunge husika lisingekuwepo kabisaa.

ndo hvo bana, waarabu wapemba hao

Kwa uelewa wangu mdogo wa sheria za bunge na kulifuatilia kwa muda mrefu sijaona wala kusikia kifungu chochote kwenye sheria za bunge kinacho toa adhabu kwa waziri endapo atalidanganya bunge au kutoa majibu yasiyo sahihi.kama hawawajibishwi si wataendelea kutudanganya?

Huyu Mama angekuwa ni wa kutoka upinzani LAZIMA angetakiwa atoe uthibitisho kwa maandishi haraka vinginevyo angetolewa nje.Swala la waziri kukiri kwamba hana taarifa zaidi ya mbunge husika lisingekuwepo kabisaa.

Umeona eeh! Hii tabia mbaya aliyokuja nayo huyu Makinda ya kutaka uthibitisho wa maandishi mimi inanikera sana ana anaifanya makusudi ili kukikingia kifua chama chake cha magamba.

Jana Mh. Anne Kilango alimshambulia Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu TAMISEMI Aggrey mwanry kwa madai kuwa amelidanganya bunge juu ya maji. Hata hivyo Spika/Naibu spika hakumtaka kutoa uthibitisho. Kwanini?

Tafakari, Chukua hatua

Quality

Back
Top Bottom