Kilango amwambia waziri kasema uongo!

Mapujds

JF-Expert Member
May 12, 2011
1,286
127
Leo katika kikao cha bunge cha maswali na majibu mbunge Anna Kilango Malechela amemwambia naibu waziri Agrey Mwanri kuwa kalidanganya bunge wakati akijibu swali kuhusu hali ya maji katika jimbo lake.

Waziri alijibu akisema kuwa visima vimejengwa katika vijiji ndani ya jimbo lake lakini mama Kilango alikuja juu na kupingana na majibu ya naibu waziri.

Sasa haya majibu yanayotolewa na mawaziri au manaibu waziri huwa wanayatoa wapi?
 
Nami nimejionea mwenyewe na Waziri kasema, Taarifa hizi ameambiwa na mkurungezi wake muda mfupi kabla ya kuingia mjengoni.

Nashukuru Waziri kakiri kuwa yeye hawezi kupingana na mbunge wa sehemu husika ila baada ya bunge watakwenda wote kujionea uhalisia. Inaonekana MAJIBU YA MJENGONI MENGI NI YA UONGO
 
Walizoea kutembeza bahasha ili kuwaziba wabunge midomo, sasa tumewashtukia hivyo mambo yote ni hadharani.
 
Nami nimejionea mwenyewe na Waziri kasema, Taarifa hizi ameambiwa na mkurungezi wake muda mfupi kabla ya kuingia mjengoni.

Nashukuru Waziri kakiri kuwa yeye hawezi kupingana na mbunge wa sehemu husika ila baada ya bunge watakwenda wote kujionea uhalisia. Inaonekana MAJIBU YA MJENGONI MENGI NI YA UONGO

Huyu Mama angekuwa ni wa kutoka upinzani LAZIMA angetakiwa atoe uthibitisho kwa maandishi haraka vinginevyo angetolewa nje.Swala la waziri kukiri kwamba hana taarifa zaidi ya mbunge husika lisingekuwepo kabisaa.
 
yale maswali ya papo kwa papo bungeni kwa mawaziri majibu yake kwa kiasi kukbwa huwa ni uongo........niliamini juzi wakati wa bajeti ya mambo ya ndani......kila swali jibu ni sungura mdogo.......
 
Hahhaaaaaaaa kumbe bahasha ilikua na nafasi yake eehhh
 
Hilo ndiyo tatizo kuu la bunge letu - spika na wenzake wanaongoza bunge ki chama zaidi na si kama taasisi huru ya kitaifa ya kutunga sheria.
ingekwa Chadema angeambiwa thibitisha!!!
 
Huyu Mama angekuwa ni wa kutoka upinzani LAZIMA angetakiwa atoe uthibitisho kwa maandishi haraka vinginevyo angetolewa nje.Swala la waziri kukiri kwamba hana taarifa zaidi ya mbunge husika lisingekuwepo kabisaa.
Mama kathibitisha kabisa kwamba n/waziri kasema uongo kwa kutoa miradi miwili, mmoja ulifadhiliwa na watu kutoka uarabuni na yeye mwenyewe Kilango akaweka umeme but serikali ikasema maji hayafai kwa matumizi ya binadamu.mimi najiuliza hivi hakuna upembuzi yakinifu unaofanywa ilikujua kama sehem hii maji yake yanafaa na si kungojea mpaka mradi unakamilika then unakataliwa, huu si upotevu wa fedha za wafadhili?
 
Kilaza Lukuvi hakuomba mwongozo wa bibi Kiroboto?

Asinge weza kuomba kwa sababu n/waziri kakiri kuwa taarifa alizopewa na mkurugenzi zinaweza kuwa si za kweli,ila ameomba waongozane na mbunge kwenda kuangalia hiyo miradi.jamaa kaonesha ukomavu kwa kukiri kudanganya na hii inatokana na kupewa taarifa za uongo na watendaji wake.
 
Mama kathibitisha kabisa kwamba n/waziri kasema uongo kwa kutoa miradi miwili, mmoja ulifadhiliwa na watu kutoka uarabuni na yeye mwenyewe Kilango akaweka umeme but serikali ikasema maji hayafai kwa matumizi ya binadamu.mimi najiuliza hivi hakuna upembuzi yakinifu unaofanywa ilikujua kama sehem hii maji yake yanafaa na si kungojea mpaka mradi unakamilika then unakataliwa, huu si upotevu wa fedha za wafadhili?
<br />
<br />hayo maji yana nini?
 
Tangu Bunge hili la 10 lianze chini ya mama kiroboto ni Mawaziri wangapi wamesema uongo ndani ya Bunge. Hii inadhihirisha kabisa hata Waziri mkuu hulidanganya Bunge kwenye maswali ya papo kwa papo. Hakuna haja kabisa ya kuwa na hicho kipindi.

Kimeanzishwa na Wabunge wa magamba ili Waziri Mkuu aonekane yuko bize Bungeni- majibu yake huwa hayana mshiko kabisa. Hutoa majibu mepesi kama mlenda hata diwani makini anaweza kujibu maswali hayo.
 
Asinge weza kuomba kwa sababu n/waziri kakiri kuwa taarifa alizopewa na mkurugenzi zinaweza kuwa si za kweli,ila ameomba waongozane na mbunge kwenda kuangalia hiyo miradi.jamaa kaonesha ukomavu kwa kukiri kudanganya na hii inatokana na kupewa taarifa za uongo na watendaji wake.
Saafi kabisa, mtiririko ulioueleza ni mzuri kabisa kimantiki. tatizo ni kwamba, mtiririko kama huo hauwahusu wabunge wa "upinzani". ajenda ya ccm ni kuwafanya wabunge wa "upinzani" waonekane watu wa vurugu, kuwazima kabisa wasijenge hoja zao, au wasifike mbali.

kimsingi nadhani huu ni mkakati wa ccm kufuatia ukweli kwamba upande wa upinzani bungeni umekuja na bundiki nyingi na hivyo waliona wajipange kuwadhibiti ili ku-mitigate hasara watakayopata. kwa upande mmoja inakilinda chama cha ccm, lakini kwa upande mwingine wanajiweka kwenye mtego.

upinzani wakijizatiti vizuri wanaweza kutumia nafasi hiyo kuwavua nguo ccm mbele ya wananchi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom