Kila Mtu Ana Time Zone Yake

Mtayarishaji

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
291
199
New York iko masaa 3 mbele ya Calfornia lakini hii haimaanishi Calfornia inaenda taratibu au labda New York iko mbio sana. Zote ziko sawa isipokuwa kila moja ina TIME ZONE yake.

Kuna mtu yuko single sasa hivi. Kuna mtu ameolewa na kusubiri miaka 10 kabla ya kupata mtoto wakati kuna mtu amepata mtoto ndani ya mwaka wa kwanza wa ndoa.

Au, kuna mtu amemaliza degree akiwa na miaka 22, lakini akasubiri miaka 5 kabla ya kupata kazi, wakati kuna mwingine amemaliza degree akiwa na miaka 27 na akapata kazi mwaka huo huo.

Kuna mtu kawa mkurugenzi akiwa na miaka 25 na kufariki akiwa na umri wa miaka 50, wakati mwingine amepata ukurugenzi akiwa na miaka 50 na kuishi mpaka miaka 90.

Kila mmoja anaishi kulinga na TIME ZONE yake.

RAFIKI ZAKO, NDUGU ZAKO AU WADOGO ZAKO WANAWEZA KUONEKANA MBELE YAKO, AU WENGINE NYUMA YAKO.

KILA MMOJA HAPA DUNIANI ANATEMBEA/KUISHI KWENYE BARABARA YAKE PEKE YAKE YA MUDA. MUNGU ANA MPANGO TOFAUTI KWA KILA BINADAMU. TOFAUTI NI MUDA TU.

Tazama, Obama anastaafu akiwa na miaka 55, Trump anaanza akiwa na 70.

USIMWONEE WIVU, WALA KUMLAUMU MTU, KILA MMOJA NA TIMEZONE YAKE. ENDELEA KUJIAMINI, KILA KITU KITAKUWA SAWA. HAUJAWAHI WALA HAUJACHELEWA. ISSUE NI TIME ZONE YAKO TU.

USIUMIZWE SANA KICHWA KWAMBA. MBONA MWENZANGU KAJENGA MIMI BADO, ANA GARI MIMI SINA, KAOLEWA/KAOA MIMI BADO....N.K.

CHAPA KAZI KWA BIDII, HUKU UKISUBIRIA MUDA WAKO..MCHE MUNGU UMTEGEMEE...KILA UFANYALO FANYA KWA IMANI.

Time will tell.



NB: Nimepata mahali ni share na wewe hapa jukwaani.
 
5b6c3979fb66f95bc860dc977e8ccb50.jpg e7e20e79d5d055f8fe458a7b0ef0fba6.jpg abf891b4d4ce79de702b40d856357182.jpg 0243895807e05a5b81fe3c91341cb0fc.jpg 655e997b19dba7ab98bae48042a57ded.jpg b8a17a053ffecaaa0138ad2851397108.jpg 912138af2ab37aa9917a7c0f5288d356.jpg
5b6c3979fb66f95bc860dc977e8ccb50.jpg
e7e20e79d5d055f8fe458a7b0ef0fba6.jpg
abf891b4d4ce79de702b40d856357182.jpg
0243895807e05a5b81fe3c91341cb0fc.jpg
655e997b19dba7ab98bae48042a57ded.jpg
b8a17a053ffecaaa0138ad2851397108.jpg
912138af2ab37aa9917a7c0f5288d356.jpg
 
Umeandika vizuri sana hasa sentensi ya mwisho make uzi kama huu nimeshawahi kuusoma hapahapa JF.
 
Back
Top Bottom