Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Nilikutana na watu wa kabila la wasagara maeneo ya ruaha mbuyuni.Hawa watu shughuli zao kuu ni uvuvi katika mto ruaha.Mto ruaha una mamba wengi hatari.Kitu wanachofanya wasagara ni kula mayai ya mamba na wakimkamata mamba basi wanaufanya mkia wake kitoweo.Kutokana na tabia hii,mamba akikutana na msagara awe mtu mzima au mtoto,huogelea kwa spidi ya bomu la majini(torpedo) kumkimbia msagara kuepuka kugeuzwa msosi.Cha ajabu ukienda mtu wa kabila jingine ambaye si mwenyeji,hawa mamba hawakuachi lazima wakuharibie.