Kila kubwa ina kubwa yake?

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,025
Nilikutana na watu wa kabila la wasagara maeneo ya ruaha mbuyuni.Hawa watu shughuli zao kuu ni uvuvi katika mto ruaha.Mto ruaha una mamba wengi hatari.Kitu wanachofanya wasagara ni kula mayai ya mamba na wakimkamata mamba basi wanaufanya mkia wake kitoweo.Kutokana na tabia hii,mamba akikutana na msagara awe mtu mzima au mtoto,huogelea kwa spidi ya bomu la majini(torpedo) kumkimbia msagara kuepuka kugeuzwa msosi.Cha ajabu ukienda mtu wa kabila jingine ambaye si mwenyeji,hawa mamba hawakuachi lazima wakuharibie.
 
Mkuu! Habari yako inanipata utata kidogo....mamba anawezaje kutambua kama mtu huyu ni Msagara au sio? Hebu dadavua wanavyojitofautisha ili habari iwe imetulia.
 
Hapo mkuu mwenyewe sikuwa na jibu sahihi,ila wanavyosema wao kile kitendo cha kula mayai ya mamba ni kinga tosha,kwa hiyo logic ninayopata,hata akihamia mtu wa kabila jingine,akianza hako katabia,atakuwa easily identified na hao mamba.swali ni hao mamba wanajuaje huyu mtu ni mla mayai ya mamba?,hapo jibu sina ila habari ndo hiyo.
 
Inawezekana ni kweli maana nasikia Wamasai wa Ngorongoro hukatisha mbugani giza giza akiwa peke yake amechelewa kwenda ngomani ndani ya mbuga. Huwa wanakuwa na ngoma zao za kimila huko mbugani katikati, sasa anayechelewa anatimka mwenyewe na mkuki wake saa 1 - 2 jioni anawahi wenzake na simba wanawajua hawawafanyi kitu. Hii nayo leo inafanya niamini wanyama wanaelewa mambo japo wanaelewaje hatuwezi kujua.
 
Hapo mkuu mwenyewe sikuwa na jibu sahihi,ila wanavyosema wao kile kitendo cha kula mayai ya mamba ni kinga tosha,kwa hiyo logic ninayopata,hata akihamia mtu wa kabila jingine,akianza hako katabia,atakuwa easily identified na hao mamba.swali ni hao mamba wanajuaje huyu mtu ni mla mayai ya mamba?,hapo jibu sina ila habari ndo hiyo.

Jag, mbona umetoa mwanzo wa jibu mwenyewe? huenda kuna chemicals fulani ziko ndani ya mayai hayo ambazo zinawafanya mamba kuwatofautisha wala mayai na watu wa kawaida?
 
Wanyama wanakawaida ya kutambua, ila mie nitatoa mfano kwa wanyama wa kufugwa hasa ng'ombe ambao kule usukumani tunawatumia kwa ajili ya kilimo, wapo ng'ombe wengine believe me wamezoea kufungwa kwenye nira na kina mama, ukienda mwanaume hata kama ungekuwa na nguvu kiasi gani atakupiga pembe mpaka utajuta kuzaliwa lakini akiona kanga tu mpole sasa sijui kama nao sense organs zinafanya kazi kama wanadamu.
 
Nilikutana na watu wa kabila la wasagara maeneo ya ruaha mbuyuni.Hawa watu shughuli zao kuu ni uvuvi katika mto ruaha.Mto ruaha una mamba wengi hatari.Kitu wanachofanya wasagara ni kula mayai ya mamba na wakimkamata mamba basi wanaufanya mkia wake kitoweo.Kutokana na tabia hii,mamba akikutana na msagara awe mtu mzima au mtoto,huogelea kwa spidi ya bomu la majini(torpedo) kumkimbia msagara kuepuka kugeuzwa msosi.Cha ajabu ukienda mtu wa kabila jingine ambaye si mwenyeji,hawa mamba hawakuachi lazima wakuharibie.
CHAKACHUA NI CHAKACHUE NA KUMWAGA PWAAA!
Mkuu umeniacha na maswali hivi mamba wana akili hizo kweli? Hebu itohoe alafu uidadavue sentensi tuelewe!
 
Kuna jamaa mmoja akipita na gari njia wanayosimama changu doa lazima aitwe we Johniiiiiiiiii weee, akafikiri labda wanalijua gari lake ila cha ajabu hata akiazima gari lingine mambo ni yale yale sijui wanamjuaje?
 
CHAKACHUA NI CHAKACHUE NA KUMWAGA PWAAA!
Mkuu umeniacha na maswali hivi mamba wana akili hizo kweli? Hebu itohoe alafu uidadavue sentensi tuelewe!
kwa kweli siri wanayo mamba wenyewe,kama nimekukera leave me alone!utani tu buddy!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom