Kila basi kuwa na mkanda leo

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
Kila basi kuwa na mkanda leo

Friday, 27 November 2009 07:13
Na Hilary Komba

UKAGUZI na kamatakamata ya mabasi ambayo hayajafungwa mikanda katika viti vya abiria ilianza jana kwa mabasi yaendayo mikoani.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Bw. James Kombe amesema shughuli hiyo imeanza baada ya kazi ya ufungaji mikanda kumalizika Novemba 26, mwezi huu.

Alisema serikali ilitoa agizo hilo kwa wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani na daladala kufunga mikanda hiyo katika viti kwa hiari lakini kwa sasa wakati huo umeisha na jeshi la kikosi cha usalama barabarani limesha sambazwa kuyakamata.

"Kwa sasa tumejipanga vizuri na tutahikisha tunakamata mabasi yote ambayo hayajafunga mikanda na kuyafikisha kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) ili yatozwe faini kwa kukaidi kufunga mikanda hiyo kwa hiari," alisema Bw. Kombe.

Alisema SUMATRA itakuwa inatoza faini kwa mabasi yasiyofunga mikanda kuanzia sh.200,000 na kuendelea ambapo shughuli hiyo inatarajiwa kuwa endelevu na baada ya kumaliza mabasi yaendayo mikoani watahamia kwa daladala.
 
Nafikiri wange waangalia zaidi Madereva. Uzembe mwingi unaanzia kwao, na sio abiria.
 
Ina maana ndio itakua mwisho wa mabasi kusimamisha abiria? Je wamiliki wa mabasi watapokeaje kupungukiwa kwa mapato waliyokua wakipata kwa kusimamisha abiria?
Abiria waliozoea kusimama ili wawahi sehemu (makazini) watafanyaje?
Sitetei daladala na mabasi kusimamisha abiria ila nataka tuzungumzie upande wa pili wa shillingi wa hiyo operesheni ya mikanda ya mabasi
 
sipingani nao ila kwa matatizo ya ajali tanzania, kufunga mkanda ndio priority katika rank ya sababu zinazosababisha ajali? mimi niko concern zaidi kuhusu ubora wa magari na uelewa wa maderewa wetu kuliko hata hayo ma mikanda, anyway who cares
 
Back
Top Bottom