Kikwete yupo nchini?

Mimi hata sijui niseme nini kuhusu huyu jamaa ambavyo hayuko serious na mambo ya msingi.... yaani utadhani haoni adha ya mafuta wanayopata wananchi wake walompa kura....

Na hafikirii kuwa hii adha inaweza kutikisa uchumi wa nchi kwa kipindi kifupi.... nachelea kusema kuwa yawezekana na yeye ni mmojawapo wa waagizaji wa mafuta hayo ndo maana anakuwa bubu kuhusu hili...
 
yuko njiani, anaelekea Namibia kushughulikia tatizo la mgao wa umeme na ukosefu wa mafuta kwa wana wa nchi yake.. Asipoenda nchi itaingia gizani eti!..
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Last I heard, alikuwa anafuturisha viongozi wa dini na jana nadhani alikuwa na Rais wa Somalia.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Rais wetu yupo nchini au? Mbona sisikii chochote kutoka kwake wananchi tunateseka na mafuta.
Yaani huyu JK kuwepo na kutokuwepo ni sawa tuu.............. Kagame alisema apewe bandari na airpot ili ili ailishe TZ na nchi yake...... Jamaa akachekelea tuuu.....Yaani we acha tuuuuuuuuuuu ..............Hatuna Rais ila tu LAIS
 
I wish tungemchukua Paul Kagame wa Rwanda kama rais wetu Tanzania angalau kwa miaka miwili anakuja kama Consultant na huyu JK anapewa likizo bila malipo akapumzike kwanza aone watu wanavyopiga kazi sio uzururaji tu.
 
Rais wetu yupo nchini au? Mbona sisikii chochote kutoka kwake wananchi tunateseka na mafuta.
Anashughulikia matatizo ya somalia ili meli za mafuta zipite salama kwenye gulf ya Aden . Haya madogo madogo ametuma watendaji wake wayashughulikie taarifa ya utekelezaji atapelekewa
 
Jk
Bilal
Pinda
Makinda

Hawa jamaa wameamua kutia pamba masikioni hasa kiongozi wao hapo juu, em leteni mwongozo wa kuwashugulikia hawa
 
Last I heard, alikuwa anafuturisha viongozi wa dini na jana nadhani alikuwa na Rais wa Somalia.
Leo anafuturu na Sheikh Shariff....

Jamaa naona amekata tamaa kabisa, ameamua kuacha nchi ijiendee yenyewe...

Namshauri atafute remote control itamsaidia kupunguza jazba za wananchi...

Unajua toka amekufa mtabiri wake Sheikh Yahya anapata tabu sana kujua what is next ndo maana ameamua kuuchuna tu
 
Back
Top Bottom