Kikwete somo la kwanza, Panapofuka moshi, panaficha moto

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
Nimefuatilia kwa muda sasa na ninaona dhahiri jambo moja, Kikwete umeshindwa kazi, achia ngazi. Kwa maneno mengino ccm ushindi wenu wa kuchakachua umekuwa anguko lenu.

Leo hii peke yake 11.11.2011, kuanzia asubuhi nimekuwa nikifuatilia matokeo manne tofauti.

1. Mwanjelwa Mbeya, polisi wanapigana na wafanyabiashara wamachinga wanaotakiwa wahame kutoka eneo wanalofanyia biashara zao. Tatizo hawakupatiwa sehemu ingine.

2. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mlimani, polisi wanapigana na wanafunzi wanaodai malipo ambayo ni haki yao.

3. Babati, polisi wanapigana na wamasai walionyang'anywa ardhi yao wanayotumia kwa shughuli zao za ufufgaji ili ardhi hiyo apewe mwekezaji.

4. Singida tangu jana ngumi zimekuwa zinarindima kati ya madiwani na maofisa wa Wilaya. Jana ilikuwa diwani wa Unyambwa na ofisa wa Ardhi na leo ni diwani wa Unyamikumbi na Kaimu Mkurugenzi.

Hiyo ni mifano michache tu, iko mingi. Nchi haitawaliki tena jk. ccm imeshashindwa. Acheni unafiki wa kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa kitumwa. Jiuzulu wewe na baraza lako la mawaziri, vunja bunge tufanye uchaguzi upya. Tunaelekea pabaya. Kama unafikiri unaweza kutawala Tanzania kwa mabavu muulize Ghadafi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom