Kikwete: Msamaha wa kodi utolewe; Lengo ni kupunguza makali ya maisha

Hana lolote huyu, hivi tangu lini Mwizi akawa na busara? Cheap popularity danganya toto. Ataifishe mitambo ya Dowans na kwafilisi rafiki zake RA, EL, Chenge na kumshitaki Mkapa kwa kufanya biashara Ikulu na kuhujumu uchumi wa TZ.

Afute na kurekebisha mikataba ya madini kama alivyoahidi alipokuwa London.
 
Nafikiri kwa kuanzia rais yupo kwenye mstari hajakosea. tatizo la kodi kubwa Tanzania ni source ya mfumuko wa bei
.

Corruption, rushwa ni source ya kila kitu maana pamoja na kuumiza wananchi pia ina slow down maendeleo yao kutokana na urasimu wanaoufanya waomba rushwa.
I agree with the rest(kinda).But kodi is not what drives up inflation in tanzania.It's production costs mainly from energy(i.e electricity&oil) and the overall global economy coupled by unrest in the middle east and catastrphies going on in Japan,brazil..(The dow jones is down by almost 600pts the past week).

Corruption has been in our blood and both the giver and receiver are to blame,the past regimes were extremely corrupt and they left this regime with a lot of bad deals in mining,bad proccurement policies etc...in 2005 inflation was 20% (World Bank)compared to 10.14 today(was down to 8.5% in 2008)

I completeley agree theres still corruption in Tanzania and this takes everybody,cops,teachers,nurses,bank clerks,everybody! so wananchi ourselves are to blame too!!
 
Kichuguu,
Mkuu wangu kwanza habari za masiku..
Mimi sii mshabiki wa JK na wala siwezi kutetea uwezo wake ila katika hili mkuu wangu namuunga kabisa mkono kutokana na hali halisi..yaani narudi kule kule kwa Watu na Mazingira

Mkuu wangu ipo haja kubwa ya kupunguza kodi na sii kutoa msamaha wa kodi kama ilivyonukuliwa na baadhi ya watu hapa janvini..
Matatizo ya JK ni mengi sana na kutokuwa na uwezo wa kuchukua maamuzi magumu ndio udhaifu wake mkubwa..

siku zote amekuwa mzito ktk maamuzi kiasi kwamba wananchi wamemwona hana uwezo wa kuongoza. Toka awamu ya kwanza.

Yawezekana hujafika Tz muda na huelewi hali halisi TRA na Bandarini kwani nijuavyo mimi karibu asilimia 80 ya bidhaa zilizopo nchini zinatoka nje, hivyo pato zima la nchi linategemea zaidi kodi.

Na kodi kwa nchi inayotegemea imports, kwa wafanyabiashara wengi wapo radhi kulipia kodi ndogo kupitia mlango wa nyuma kwa sababu ni kubwa sana na hazilipiki...hili ndilo tatizo tulokuwa nalo hivi sasa..

Sasa kama unawajua vizuri Watanzania jinsi wanavyoweza kujenga mazingara ya rushwa, na ukawapa sababu kama hiyo basi kila mtu TRA ataitumia na ndipo urasimu unapoanza..

Lakini kama ushuru ungekuwa mdogo kiasi kwamba mfanyabiashara haoni sababu ya kutoa rushwa,,hii ingesaidia zaidi serikali kukusanya kodi zaidi kuliko mfumo uliopo ambao kwa uchache naweza kusema robo tatu ya fedha zinazolipwa TRA huishia mifukoni mwa watu na sii mfuko wa serikali.

Rushwa imefika pabaya sana na hakika sidhani kama rais yeyote atakayekuja pasipo kufanya maamuzi magumu kama haya ataweza kuiondoa rushwa kwa sababu mizizi yake imefika hadi chini kwa walalahoi.

Hii ni hatua ya mwanzo kinachofuata iwe marekebisho ya ukusanyaji wa kodi hizo wakizingatia kuondoa rushwa,zaidi ya kupunguza kero za mfumko wa bei kwani fedha yetu yenyewe haina tena thamani, hivyo regulations zijikite ktk kufanisi hilo.

Binafsi naamini kabisa hii ni hatua nzuri kabisa na itasaidia sana kupunguza urasimu, rushwa na pengine hata bei ya bidhaa nchini maana tunategemea imports,

Umeme hatuna, maji shida yaani hakuna lenye afadhali hata kidogo na haya yote yametokana na uzembe wa viongozi wa chama tawala kutojali mipango ya maendeleo ya muda mrefu. Ila kuiba zaidi kwa ruksa ya Azimio la Zanzibar.

Ukitazama infrastructure ya nchi yetu ktk sekta zote ni zile aloacha mwalimu wakati population imeongezeka mara mbili na uwekezaji nchini kwa asilimia zaidi ya elfi, .sasa kama sisi ni Taifa la ombaomba sidhani kama kuna haja kubwa ya kulalamika tuu hata kama hatua bora zinachukuliwa kurahisisha maisha ya Watanzania ambao hawana jinsi ila na wamekwisha poteza hata tumaini la maisha acha mbali kiuchumi..
 
sasa anatekeleza sera za CDM.
maana kile CDM wanalalamika ndicho yeye anafanya mfano.

katiba ambayo kwa kiasi kikubwa CDM wamepambana nayo hadi kuamua kutoka bungeni wakati akihubia bunge; na hata maandamana ya amani ya CDM ambayo baadhi agenda ilikuwa maisha magumu na ndio vitu ambavyo yeye anataka vishughulikiwe.

nafurahi amekuwa anakubali ushauri CDM kiujanja ujanja
 
Back
Top Bottom