Kikwete mnyongeni lakini haki yake mpeni!

Baba Mwanaasha
1. Aliingia kwa demkrasia ya kutukana watangulizi wake kwa kutumia magazeti leo kanuna mwenyewe. BWM alikuwa mchapa kazi akamwachia hazina ya kutosha lakini huyo mwanademocrasia kazitafuna zote!
2.Kabla ya Democrasia yake hatukuwa tumegawanywa kidini kama sasa leo tanzania yenye udini inawezekana.
3. Chini ya BWM uchumi uliimarika lakini leo mambo shghabaghala
4. Aliahidi kuwavua watu magamba holaaa! HAKUJUA KWAMBA MTI BILA GAMBA UNAKAUKA!
5. Aliingia akiwa HANDSOME sasa uso umezeeka

TANZANIA BILA DEMOCRASIA INAWEZEKANA
 
Karibia watu wote niliowahoji wanadai Jk hajafanya lolote la maana kama kiongozi wa nchi.Mimi naona si kweli.Jk amefanikiwa sana kukuza Demokrasia kuliko watangulizi wake japo ameshindwa kukuza uchumi.Watu wana uhuru wa kuongea,Uhuru wa media umeboreka,maoni ya wapinzani yanafanyiwa kazi, unaweza hata kumkosoa rais au kiongozi yeyote hadharani nk.hayo mambo ni ya muhimu sana kwa maendeleo ya nchi.Ndiyo yaliyo mng'oa Gadafi japo alifauru sana katika nyanja ya uchumi.
wadau mnasemaje?
Naomba kutoa hoja.

kama unazungumzia uhuru wa kujieleza wa DK Benson Bana sawa. Kama unazungumzia uhuru wa kidemokrasia wa Habari leo , Uhuru, Jamba leo na Dira ya Mtanzania sawa. Lakini unajua fika wengine wanavyofuatiliwa kwa uhuru huo huo kama Mwnahalisi, JF, nk. Hao wapo tu kwa roho ngumu ! Hana jinsi, maana mitatndao ya jamii hawezi izuia....technolojia mzee inamlazimisha akubali. JK , ameshindwa demokrasia ndani ya chama chake, na kukiteka kikawa cha familia, leo hii unakuja sema ameruhusu demiokrasia? CCM sasa ni yake, anafanya atakavyo. Kina Warioba, Sumaye, Salim Ahmed Salim, Mkapa, Mangula, Malechela, Butiku , Kitine, to mention a few wnaweza sema neno ndani ya CCM? Na mbaya zaidi sasa hivi wameenguliwa kabisa, watabaki washauri tu...kwishnei! leo hii huyo aliyeshindwa kuheshimu demokrasia ndani ya Chama chake kilichomkuza ataruhusu wapi demokrasia kwenye jamii nje ya cchama hicho? Hilo la kuruhusu mijadala hana budim, hata Irani ambako demokrasia ni zero, bado watu wanauhuru kwa kutumia mitandao ya kijamii.
 
@zero. Mkuu imebidi nichangie kuhusu comment yako kwamba demokrasia ilianza kukua wakati wa Mkapa. Mimi sikubaliani na wewe kwasababu kama kuna mtawala ktk nchi hii ameongoza kibabe na kutumia vyombo vya dola kuhujumu wapinzani wake ni Mkapa. Tusiwe wasahulifu hivi. Hivi unajua ni kwanini watawala mpaka sasa hawaoni aibu kuiba ama kuchakachua kura za wapinzani wao? Hivi kama siyo hizi tabia za kibabe na kinyume na demokrasia zilizoasisiwa na utawala wa Mkapa leo hii tungekua na bunge lililojaa wana CCM wanaosinzia na kugonga meza kupitisha ujinga wowote ilimradi umeletwa na serikali?
 
Pamoja an weaknesses nyingi nyinginezo kama walivyo mapresida wote duniani kwani hakuna aliye perfect,mimi nina mu admire sana JK kwa uvumilivu na subira aliyonayo when it comes to criticism,amekuwa mvumilivu sana na hajawahi kuonyesha jazba wala hasira,hii ni quality ya kipekee ambayo I believe ni inborn,for this nampa 5
 
...Unataka kusema waandishi wa habari wako huru zaidi sasa? Kubenea na Ndimara walimwagiwa tindikali kipindi cha Mkapa au Kikwete? Ni ktk utawala wa nani gazeti la Mwanahalisi lilifungiwa kwa siku 90? Na ya Jerry Muro je? Nini hasa sababu ya Prof. Baregu kutopewa mkataba UDSM?

Kuna demokrasia kweli kama waziri maisha yake yanakuwa hatarini kwa sababu ya mambo aliyoyasema au anayoyajua? Analalamika kwamba kuna watu wana njama za kumuua na hatua hazichukuliwi, huku sio kufungana midomo?

Kwa nini Tirdo Muhando alinyimwa mkataba mpya kimizengwe pamoja na kazi nzuri aliyoifanya TBC? Mhariri na mwandishi wa Tanzania Daima pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Mwananchi wana kesi mahakamani kwa "uchochezi", huu ni utawala wa nani? Demokrasia iko wapi ktk haya?

Nimemkopi timbilimu nikaona nikikujibu mimi niatakupendelea sema na Timbilimu "@zero. Mkuu imebidi nichangie kuhusu comment yako kwamba demokrasia ilianza kukua wakati wa Mkapa. Mimi sikubaliani na wewe kwasababu kama kuna mtawala ktk nchi hii ameongoza kibabe na kutumia vyombo vya dola kuhujumu wapinzani wake ni Mkapa. Tusiwe wasahulifu hivi. Hivi unajua ni kwanini watawala mpaka sasa hawaoni aibu kuiba ama kuchakachua kura za wapinzani wao? Hivi kama siyo hizi tabia za kibabe na kinyume na demokrasia zilizoasisiwa na utawala wa Mkapa leo hii tungekua na bunge lililojaa wana CCM wanaosinzia na kugonga meza kupitisha ujinga wowote ilimradi umeletwa na serikali? "
 
Lakini hili litampeleka peponi jamani Mwanae Mwanaasha kasomea hapa hapa bongoland sio kama watoto wa mawaziri wake ikifika december wanapishana angani wengine wanatoka UK,wengine USA wengine India nk
bwana wee sawa, lakini maubadhirifu anayofanaya hata hayo machache unayoyazungumzia kama mema ameyafanya yanamezwa humo.
 
Haya ni mawazo ya kiendawazimu kutoka kwa mtu aliyefirisika kimawazo. Nani kakwambia kuwa uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kutoa mawazo na demokrasia vinahitaji fadhila toka kwa Baba Mwanaasha?? Hiyo ni haki yetu ya msingi ya kikatiba, tena hatuna uhuru wa kutosha katika nyanja hizo hadi vyombo vya habari vya serikali vinatumika kama propaganda ya chama tawala!!! Mawazo yako ni sawa na mzazi anayedhania kuwanunulia wototo wake chakula ni fadhila na sio wajibu. Soma vizuri katiba kijana, nakushauri usishiriki katika kuunda katiba mpya utapotosha watanzania.
ugonjwa mkubwa unaoumwa ni USHABIKI.
Taifa letu linahitaji watu wenye open mind ambao hawana chembe ya ushabiki.kwa hiyo kuleta Demokrasia ni wajibu ila kuleta maendeleo siyo wajibu wake?
 
kwa kuwa tayari tuna demokrasia,Rais atakaefuata ashughulikie uchumi.JK Uwezo huo hana.hayo aliyo yafanya ndiyo mwenyezi Mungu alimwangazia. kumbuka kila mtu ana strength na weakness.
Hiki ulichoandika ni ugonjwa wa akili; yaani fikra zako zinakutuma kuwa mtu akae madarakani miaka kumi kazi yake iwe kujenga uhuru wa kuongea na demokrasia, uchumi sifuri, halafu aje mwingine ndiyo aanze kujenga uchumi? Wewe umelogwa wewe.
Je, Mungu amekwambia kwamba hayo ndiyo aliyomuangazia kama unavyotaka kutuaminisha hapa?
 
Mkuu tuna mhukumu kiongozi kwa ahadi zake za kampeni. Kwa hiyo swala si JK kuleta demokrasia kwa sababu hiyo ni haki yetu haja tufanyia fadhila yoyote. Swala ni je katoa ahadi ngapi na katimiza ngapi?
 
Karibia watu wote niliowahoji wanadai Jk hajafanya lolote la maana kama kiongozi wa nchi.

Mimi naona si kweli.Jk amefanikiwa sana kukuza Demokrasia kuliko watangulizi wake japo ameshindwa kukuza uchumi.Watu wana uhuru wa kuongea, Uhuru wa media umeboreka, maoni ya wapinzani yanafanyiwa kazi, unaweza hata kumkosoa rais au kiongozi yeyote hadharani nk. Hayo mambo ni ya muhimu sana kwa maendeleo ya nchi.

Ndiyo yaliyomng'oa Gadafi japo alifaulu sana katika nyanja ya uchumi. wadau mnasemaje?

Naomba kutoa hoja.

Demokrasia ipi aliyokuza? kuiba kura?
 
Baba mwanaasha ndiyo yule ambaye mtoto wake kafeli,ndiyo yule kukicha anasafiri,ndiyo yule mwenye ahadi hewa,ndiyo yule asiyekuwa na maamuzi,ndiyo yule anayetoka Chama legelege na dhaifu,ndiyo yule anayetoka chama cha mafisadi,ndiyo yule ambaye mtoto wake kajilimbikizia mamilioni ya mapesa,kama ndiyo huyo kazi ipo natamani hata kesho ajiuzuri ili atuachie nchi yetu Tanzania! Akili ni nywele kila mtu anazake
 
Kweli kafanya mengi kinadharia! lakini kivitendo kafanya mengi madudu, apunguze safari! Sikumbuki kama ameshawahi kutulia mwezi mzima magogoni. Kwa hiyo Democrasia aliyoijenga inafutwa na safari anazosafiri.
 
Unamaanisha huyu mchakachua kura kupitia usalama wa taifa? Use da last gen. election kumpima. Vipimo vingine havitoshi maana havihatarishi uwepo wake madarakan kivile
 
kwa kuwa tayari tuna demokrasia,Rais atakaefuata ashughulikie uchumi.JK Uwezo huo hana.hayo aliyo yafanya ndiyo mwenyezi Mungu alimwangazia. kumbuka kila mtu ana strength na weakness.

Wewee! Acha kumsingizia mwenyezi MUNGU. Huu ni uzembe na ufisadi! ..Safari za nje ni mzigo!, Wizi wa IPTL, Richmond, Dowans na Symbion nao ni mzigo!, Posho za wakubwa, malipo ya wanasiasa, mafao ya wanasiasa wastaafu na waliojiuzulu, Matanuzi ya serikali kwa magari na samani za kifahari n.k. Je, Haya MWEnyezi MUNGU anaingiaje? ..Ahadi za maisha bora kwa kila mtanzania ilikuwa GHILIBA?
 
FEZA huwezi kuilinganisha na shule za kata. Hii ni miongoni mwa shule zenye ada zaidi ya milioni tatu, waalimu wa kutosha, zana bora za kufundishia na kujifunzia, maabara, maktaba n.k. Na Hiki ni kilio cha watanzania waliowengi wanaoelewa!. Shule za serikali ni dhaifu kwakuwa Kikwete na wenzake hawasomeshi huko. Ukifahamu tofauti hii huwezi kutoa utetezi dhaifu kama huu.

Lakini hili litampeleka peponi jamani Mwanae Mwanaasha kasomea hapa hapa bongoland sio kama watoto wa mawaziri wake ikifika december wanapishana angani wengine wanatoka UK,wengine USA wengine India nk
 
Haya ni mawazo ya kiendawazimu kutoka kwa mtu aliyefirisika kimawazo. Nani kakwambia kuwa uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kutoa mawazo na demokrasia vinahitaji fadhila toka kwa Baba Mwanaasha?? Hiyo ni haki yetu ya msingi ya kikatiba, tena hatuna uhuru wa kutosha katika nyanja hizo hadi vyombo vya habari vya serikali vinatumika kama propaganda ya chama tawala!!! Mawazo yako ni sawa na mzazi anayedhania kuwanunulia wototo wake chakula ni fadhila na sio wajibu. Soma vizuri katiba kijana, nakushauri usishiriki katika kuunda katiba mpya utapotosha watanzania.
ndio tatizo lenu wengi wenu humu mmekalia kubisha tu kila linalofanywa na JK huo sio u graet thinker, wakati wa Ben na awamu ya kwanza hiyo katiba unayosema haikuwepo? acheni ubabaishaji kabla ya kuropoka rejea historia
 
Back
Top Bottom