Kikwete mnyongeni lakini haki yake mpeni!

nasita kukubaliana na wewe kwa sababu hili wimbi la freedom of expression limeikumba dunia nzima kwa hiyo hata kama ni wewe ungekuwa unaongoza mambo yangekuwa hivi,ni mfumo wa kidunia.
 
..Kwa hiyo tulimchagua akuze demokrasia? Kama tunataka kumpima Rais Kikwete, tumpime kwa kuangalia ahadi zake wakati wa chaguzi zote mbili na tuangalie hali ya nchi wakati anaichukua. Haina maana kuchagua rais kama ataharibu waliyofanya wenzake (kwa mfano uchumi) waliotangulia. Tunataka rais aje na vision yake na aitekeleze bila kuathiri mazuri waliyofanya wengine.
 
Mkuu Mkwakwasu mimi nampongeza Kikwete kwa hii issue ya katiba mpya. Kama ataendelea na msimamo thabiti bila kuwasikiliza wenzake wengi ndani ya CCM ambao hawapendi ushiriki wa wananchi wote basi atadumu ktk historia ya nchi yetu vizazi vingi vitavyofuata ingawa ameshindwa katika Uchumi.
 
Mzee Ruksa alisema ''kila zama na kitabu chake''. Rais Kikwete, pamoja na mapungufu yake yaka kiongozi na binadamu, amefanikiwa sana katika kukuza demokrasia na uhuru wa watu kuto amoni bila wasiwasi. Nchi nyingi barani Afrika uhuru kama huo ni ndoto za mchana. Tumpe pongezi kwa hilo. Suala la uchumi tutanza kulipatia ufumbuzi baada ya katiba mpya kama itategua kitendawili cha mfumo tulionao ambapo maamuzi yote yamehoidhiwa dar na kwa watu wachache.
 
we mwenyewe umemwita baba mwanaisha! Badala ya kumwita mh JAKAYA, ni dalili ya kumdharau. Jk hana lolote kachemka 2.
 
napigana na hoja yako kwa upande wa demokrasia,ni vizuri uwe na uhuru wakuongea na unavyoviongea havifanyiwi kazi? je kipi bora kuwa na demokrasia ya kuongea na kukosoa afu watu wako wanakufa njaa kwa umaskini,uchumi wa nchi yako uko down?NOTE: ni bora uwe Dictator lakini maendeleo ni makubwa na uchumi wako uko juu,na ufisadi hakuna katika serikali yako.Mtu kama Gaddafi ametunza na amepigania rasilimali ya nchi yake kwa muda wa miaka yote.
 
Naunga mkono hoja!!Tatizo siasa za Tanzania zinahitaji uelimishaji sana kwa wananchi!Watu wakishakuwa against na wewe hata ufanye nini wataendelea kukuponda tu!Kwa democracy Jamaa amejitahidi na atabaki kuwa mfano wa kuigwa!!

Nawasilisha!!

Kweli usemayo mtu hata mchukue tembo ambebe mfukoni wataona hajafanya kitu!
 
Ulu ulishamuuliza Jenerali ulimwengu dhama zake wakati wa mzee BWM hali likuwaje,yaliyomtokea usingesema haya,kama ulikuwa mfuatiliaji wa magazeti ya RAI basi usingesema haya ya kuwa hiyo ni haki yako.Unajua haki ipo siku zote lakini haki hiyo inatendeka?
Na hakika JK anagombana sana na wasaidiz wake nikimaanisha watawala wa Serikali na chama chake kwa uhuru huu wa habari ambao wao wnaona kama umekithiri na kuleta changamoto kubwa sana kwenye utawala kwa kuwa Wananchi husika wako well informed na mambo mengi yanayoendelea ndani ya Taifa na ndani ya Serikali.

...Unataka kusema waandishi wa habari wako huru zaidi sasa? Kubenea na Ndimara walimwagiwa tindikali kipindi cha Mkapa au Kikwete? Ni ktk utawala wa nani gazeti la Mwanahalisi lilifungiwa kwa siku 90? Na ya Jerry Muro je? Nini hasa sababu ya Prof. Baregu kutopewa mkataba UDSM?

Kuna demokrasia kweli kama waziri maisha yake yanakuwa hatarini kwa sababu ya mambo aliyoyasema au anayoyajua? Analalamika kwamba kuna watu wana njama za kumuua na hatua hazichukuliwi, huku sio kufungana midomo?

Kwa nini Tirdo Muhando alinyimwa mkataba mpya kimizengwe pamoja na kazi nzuri aliyoifanya TBC? Mhariri na mwandishi wa Tanzania Daima pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Mwananchi wana kesi mahakamani kwa "uchochezi", huu ni utawala wa nani? Demokrasia iko wapi ktk haya?
 
Karibia watu wote niliowahoji wanadai Jk hajafanya lolote la maana kama kiongozi wa nchi.Mimi naona si kweli.Jk amefanikiwa sana kukuza Demokrasia kuliko watangulizi wake japo ameshindwa kukuza uchumi.Watu wana uhuru wa kuongea,Uhuru wa media umeboreka,maoni ya wapinzani yanafanyiwa kazi, unaweza hata kumkosoa rais au kiongozi yeyote hadharani nk.hayo mambo ni ya muhimu sana kwa maendeleo ya nchi.Ndiyo yaliyo mng'oa Gadafi japo alifauru sana katika nyanja ya uchumi.
wadau mnasemaje?
Naomba kutoa hoja.
.

Jk amefanikiwa sana kukuza Demokrasia kuliko watangulizi wake,
 
Hayo ni mapungufu lakini hayaondoi ukweli kwamba Jk kakuza sana demokrasia kupita watangulizi wake. Jf ni matokeo ya kukua kwa demokrasia hiyo.
 
Demokrasia ni dhana pana sana , na huu unaouita uhuru wa kutoa maoni ni sehamu tu ya hiyo unayoiita demokrasia. Demokrasia ya kweli huzalisha uchumi uliobora kwani rushwa na ufisadi vinathibitiwa bila upendeleo na vitu hivi vikifanyika maana yake kuna utawala bora; na utawala bora maana yake watu hawaonewi na polisi wala mahakama na wanapata haki zao na hivi ndio vinakuwa vichocheo vya ukuaji wa uchumi. Je kuna utawala bora katika uongozi wa mkweree; je ameweza kuthibiti ufisadi na rushwa vitu ambavyo vingesaidia ukuaji wa uchumi na maisha bora kwa kila mtanzania?
 
Karibia watu wote niliowahoji wanadai Jk hajafanya lolote la maana kama kiongozi wa nchi.Mimi naona si kweli.Jk amefanikiwa sana kukuza Demokrasia kuliko watangulizi wake japo ameshindwa kukuza uchumi.Watu wana uhuru wa kuongea,Uhuru wa media umeboreka,maoni ya wapinzani yanafanyiwa kazi, unaweza hata kumkosoa rais au kiongozi yeyote hadharani nk.hayo mambo ni ya muhimu sana kwa maendeleo ya nchi.Ndiyo yaliyo mng'oa Gadafi japo alifauru sana katika nyanja ya uchumi.
wadau mnasemaje?
Naomba kutoa hoja.

Kwa wanaoona wanaona na kukubali, lakini wasioone hawaoni na wengi wao ni wale wanaolilia kwenda Magogoni... wanalokundi kubwa la watu wanalijaza fitina na chuki kwa serikali yao kwa malengo ya kushibisha matumbo yao.
 
Neno hajafanya kitu katika hali yoyote haliwezi kuungwa mkono. Limejaa chuki.

Kama lengo ni kuonyesha mapungufu inapendeza kuwa wakweli kwa mabaya na mazuri ya utawala wa awamu ya nne.
 
Karibia watu wote niliowahoji wanadai Jk hajafanya lolote la maana kama kiongozi wa nchi.Mimi naona si kweli.Jk amefanikiwa sana kukuza Demokrasia kuliko watangulizi wake japo ameshindwa kukuza uchumi.Watu wana uhuru wa kuongea,Uhuru wa media umeboreka,maoni ya wapinzani yanafanyiwa kazi, unaweza hata kumkosoa rais au kiongozi yeyote hadharani nk.hayo mambo ni ya muhimu sana kwa maendeleo ya nchi.Ndiyo yaliyo mng'oa Gadafi japo alifauru sana katika nyanja ya uchumi.
wadau mnasemaje?
Naomba kutoa hoja.

Mimi sikubaliani nawe kuhusu swala la demokrasia. Nafikiri Demokrasia iliananza kukua wakati wa Mkapa na Kikwete hakuwa na jinsi ya kuistop kwa mahala ilipokuwa imefikia. Kam ni kusema watu wamesema sana humu na viongozi walichambuliwa sana humu kabla ya uchaguzi wa 2005. Kama unayotaka kusema ni kweli kwa nini kuna magazeti yamefungiwa wakati wake na kuna waandishi wa habari wana kesi mahakamani kwa ajili ya kutoa maoni yao binafsi?? Sikumbuki wakati wa Mkapa kama kuna gazeti lilifungiwa au mwandishi wake kufikishwa mahakani kwa ajili ya habari aliyoandika. JF ilifungwa na tukaambiwa humu kuwa wamiliki wamekamatwa wakati huu huu wa JK.

Kitu ninachokuunga mkono ni tabia yake ya walau kusikiliza watu na wapinzani wakati kuna jambo limetokea. Siyo kama Mkapa.
 
Ukiambiwa chagua
A. maneno mengi, kutukana na ngonjera kibao
B. Gunia la mahindi, paa juu ya kichwa chako, na kaniki ya kukusitiri usikae uchi

utachagua nini? A au B?

Acheni longolongo nyingi,Nani anataka kwenda magogoni bana? Hao wanafikiria kila anaeona mapungufu anataka kwenda magogoni basi akili yake ni ndogo sana!Wengine wala hatuna shida kivile kwenda magogoni maana magogo yetu yanatutosha.
 
Mimi sikubaliani nawe kuhusu swala la demokrasia. Nafikiri Demokrasia iliananza kukua wakati wa Mkapa na Kikwete hakuwa na jinsi ya kuistop kwa mahala ilipokuwa imefikia. Kam ni kusema watu wamesema sana humu na viongozi walichambuliwa sana humu kabla ya uchaguzi wa 2005. Kama unayotaka kusema ni kweli kwa nini kuna magazeti yamefungiwa wakati wake na kuna waandishi wa habari wana kesi mahakamani kwa ajili ya kutoa maoni yao binafsi?? Sikumbuki wakati wa Mkapa kama kuna gazeti lilifungiwa au mwandishi wake kufikishwa mahakani kwa ajili ya habari aliyoandika. JF ilifungwa na tukaambiwa humu kuwa wamiliki wamekamatwa wakati huu huu wa JK.

Kitu ninachokuunga mkono ni tabia yake ya walau kusikiliza watu na wapinzani wakati kuna jambo limetokea. Siyo kama Mkapa.

Kama kikwete aliendeleza kazi ya Mkapa bado ni mafanikio kwani tungeweza pia kushuhudia kazi hiyo ya Mkapa ikirudi nyuma.
 
Back
Top Bottom