Kikwete kwenda Hija?

JK hembu tumia muda wako kidogo uende kukamilisha nguzo ya 5 ya uislam huko Makka/Madina. Sio kila uchao we kiguu na njia tu Ulaya hata unachokifanya kuhusu njii hii hakionekani, nenda kajisafishe huenda ikakusaidia sana kuliongoza taifa hili kwa kipindi kilichobakia.

Ningependa kuona unakuwa mmoja wa mahujaji katika kipindi hiki, hasa ukiangalia tayari kuna matishio ya Al-shabab na misukosuko ya nchi za kiarabu, huenda kwa hija hii mambo mengi yakakaa sawa. Usisahau kuwaambia kwamba serikali yako haitambui mashoga pia.

Nakubaliana nawe, aende Hijja kidogo, labda atatuombea DAWASCO na TANESCO waache rushwa, uvivu na ufisadi, tena anaweza kuongeza kwenye sala zake maswala ya afya, ustawi wa jamii, elimu na miundo mbinu! Sala zake lazima zitakua na nguvu, maana kwa shida tulizonazo, hawezi kuhamisisha wananchi wayatatue, atatuombea wananchi tuache kuabudu ufisadi, tufungue macho yetu na kuchagua viongozi wenye sifa.
Ni sala tu kwa mbele. Mvua hamna sala, barabara mbovu sala, ufisadi sala, yaani ni sala kwa matatizo yetu yote mkuu, mpaka tutasikilizwa na mwenyezi mungu!
 
H.E. President, Alhaji Lt. Col. (Rtd) Dr. Dr. Dr. Dr. Dr. Chairman (CCM) Jakaya Kikwete
 
Hii itakuwa hatua mojawapo muhimu ya kujivua gamba!!
 
kama alivyoenda kumwona ngassa kule seattle akitokea south africa akicheza na man united waqt nchi inamsubiri kutoa maamuzi ya jairo...

angekuwa ngasa kaenda kucheza madina angeenda kumuona.kikwete hata umwambie nakulipia gharama zote hatii mguu madina piga ua.
 
watu walishamezeshwa sumu na hizi imani za kuja na majahazi,na utashangaa anarudi swaafi!!
 
naona kama amewai labda kama kuna remix.
ana vimeo vingi vya kusawazisha labda kama anajuana na karan wa ahera!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom