Kikwete hana ubavu wa kuvunja baraza la mawaziri

He jamani,

tuweni na subira kidogo. Ninauhakika Kikwete anajua kinachoendelea na atafanya kazi pale uchunguzi utakapokamilika.

Sio kila jambo linalosemwa lina ukweli. Nchi lazima sheria ifuatwe ili amani iwepo. Kikwete atapanga timu mpya pale tu muda utakapotimia.

Asante

Subira hadi 2010 au 2015?
Kwa kukumbusha tu ni kuwa wakati anaingia madarakani walisema NO business as Usual, Atakayetuhumiwa kwa utendaji mbovu na hasahasa rushwa, hatutasubiri ushahidi kwani, tutampumzisha kwa maslahi ya umma.
Yako wapi sasa?
 
....huyu mkwere is a big dissapointment,i doubt hata kama anajua anachofanya,seems he s a nice guy na hana deal chafu lakini kwa style yake ya uongozi hatutaenda popote yaani ni ushikaji shikaji tuu na maslahi ya chama mbele kuliko nchi....very soft & unambitious guy he needs to go!

Mtendeeni haki Mh.JK anajitahidi kuweka mambo yake vizuri kwa faida ya wote,ktk safari hiyo anakutana na mengi ambayo sisi wananchi wa kawaida na hata wana JF kamwe hatutakutana nayo,ni haki kila mwenye neno juu yake kusema lakini ni wajibu wa kujipima na kumpima yeye kwa kuzingatia upana wa majukumu yake ya kila siku.

He is very ambitious president ever happened to TZ tatizo ni sisi wabongo tulimfahamu mapema kuwa ana hamu ya kufanya wonders na yeye amekuwa akikiri hilo toka rohoni mwake kwa mtizamo wa nchi anayoitamani.The guy anahaha ,halali ,anaweweseka na kuna wakati anafadhaika kwa jinsi anavyoona Kanani anayoitaka haiji kwa kasi aliyoidhamiria but he is doing his best for Tanzanian,time will tell.

Anaiongoza Tanzania na siyo kijiji hivyo si mpaka tumuone analia ndio tujue anakerwa na matatizo yetu.

Mabadiliko ktk safu ya uongozi wake ni utashi na imani ya kuwajibika kati yake na baraza analoliongoza,aliwateua kwa utashi wake,imani yake kwa watangulizi,washauri na wafadhiri vivyo hivyo atafanya marekebisho kwa stahil yake kwa wakati ambao yeye kama President na presidency wanauona kuwa sawia.
Tukumbuke kuwa hata akifanya mabadiliko watakaobahatika ni binadamu ambaye wasifu wake mkuu ni udhaifu.
Let him do his job and for us ' We pray for him and Tanzania.
 
Rostam Aziz ni mbunge aliyechaguliwa na wananchi kama wewe na mimi, mkuu mbona unamuongelea kama a convict, wakati ni kiongozi ambaye hana makosa yaliyothibitishwa kisheria?

I understand kuwa unajaribu kuwa aggressive, lakini tatizo unakosa hoja za kimsingi, aliyoyafanya rais yanatosha for now Ikulu ni mahalai ambapo vichwa vinatulia sio kukurupuka tu kama wenda wazimu, mkuu serikali haiendeshwi na JF au mob justice, ndio maana rais ana washauri wengi ambao mimi na wewe tunawalipa mshahara kwa kodi zetu,

Please jaribu kuheshimu viongozi hata kama huwapendi, ni mbunge aliyechaguliwa na wananchi, sasa usimuongelee kama ni mhuni tu wa mtaaani, ukomavu wa kuelewa siasa ni pamoja na kuheshimu viongozi wako walichaguliwa kihalali mkuu, na hii ni kwa CCM na hata upinzani!

KURA; Fasiri yake ni kubwa sana na moja wa wajibu mkubwa wa mpiga kura ni kuheshimu matokeo ya KURA,then aliyechaguliwa ni muheshimiwa automatically.
Ninawaomba watanzania tusisahau kuwa haki ni pacha wa wajibu.

Haki ya KURA iendane na wajibu wa KUHESHIMU.
 
Hivi kweli ni yeye alikuwa na final mandate ya kuwanyima uongozi au wajumbe

Mkuu wangu hesima mbele, waliochaguliwa majuzi Dodoma ni wale tu aliokuwa anwataka Muungwana, ama sivyo Msekwa asingepata kura hata moja, rest assured brother, kuwa hakuna kiongozi yoyote aliyechaguliwa Dodoma majuzi ambaye hatakiwi na Muungwana!


2.
Thanks Mkuu, Nyani anakomwa hapa hapa JF mchana Kweupeeeeee!

Sawa sawa mkuu, tunamkoma nyani lakini kwa hoja za msingi mkuu, viongozi waliochaguliwa na wananchi pia wanahitaji kuheshimiwa, au kuwahehismu wananchi waliowachagua, iwapo hawafanyi tunayoyataka ambao hatukuwachagua!

Ila haipunguzi lolote wala haiongezi kwenye kumkoma nyani!
 
I think we need pace kwenye mabadiliko ya mawaziri especially Fetha,Biashara na madini.Lakini JK kusafiri nje sana ni muhimu he need to give donor countries confidence and explain his vision thats why we have seen donor disbursement in time this year .KWA HILO TUMPE BIG UP
 
Mimi naamini kuwa jeuri ya kufanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri analo,ila siamini kama ana jeuri ya kumtoa/kumbadilisha Lowasa.
Mabadiliko yanakuja na inasemekana mawaziri wengi sana watatemwa,anaelekea kupona kwenye hili ni Chenge.

Cha ajabu ni hiki,inasemekana kuwa Lowassa alipata kura 600 na Makamba alipata kura 400 kwenye uchaguzi wa NEC,na habari zilipofika kwa JK usiku huo,akawaagiza watangaze matokeo kama yalivyo...ilibidi Mwinyi,Kawawa na Mkapa waingilie kati na kuinusuru hio situation,wote wakaongezewa bukubuku kwenye kura zao.Sasa ukweli wa hili sijui ni % ngapi,lakini ni dhahiri kuwa Lowassa anazidi kuwa unpopular,maana inasemekana kuwa hakupata kura hata moja from Arusha,Dodoma na Mara!
 
asante mkuu ES. Nimeelewa. Tunasubiri kwa hamu the big show atakapounda upya cabinet na kuwatoa wachafu. hapo atajitoa kitanzini.
 
Mkuu wangu hesima mbele, waliochaguliwa majuzi Dodoma ni wale tu aliokuwa anwataka Muungwana, ama sivyo Msekwa asingepata kura hata moja, rest assured brother, kuwa hakuna kiongozi yoyote aliyechaguliwa Dodoma majuzi ambaye hatakiwi na Muungwana!

Hilo nalo ni tatizo, je ni viongozi wanaotakiwa na nchi yao? Kutakiwa na Rais Kikwete ni jambo moja, lakini kutakiwa na nchi yako kunazidi matakwa ya Rais!

Sawa sawa mkuu, tunamkoma nyani lakini kwa hoja za msingi mkuu, viongozi waliochaguliwa na wananchi pia wanahitaji kuheshimiwa, au kuwahehismu wananchi waliowachagua, iwapo hawafanyi tunayoyataka ambao hatukuwachagua

Mzee naona unarudia sana suala hili la heshima kwa viongozi. Ndugu yangu heshima haiombwi na haitolewi kama sadaka. Heshima inastahiliwa.. (it is earned!). Halafu heshima siyo kitu ambacho kuna mtu anaweza kukidai kuwa "nataka kuheshimiwa" kwa sababu kuna bendera inapepea na Polisi wanapiga saluti! Hiyo ni heshima ya kijeshi. Heshima inayotokana na woga au hofu hiyo si heshima ni mwanzo wa kutawaliwa kifikra.

Viongozi wetu wanastahili heshima kama binadamu wengine na chochote cha ziada ya hapo they have to earn it! Huwezi kutia sahihi mikataba mibovu halafu ukataka watu wakuheshimu, na haiwezekani mtu avumilie uzembe, azawadie kutokuwajibika halafu watu waendelee kumheshimu. Heshima inaweza kutolewa na inaweza kuondolewa.

Na endapo heshima itaondolewa haina maana wale viongozi wamepoteza "kura zao". Wananchi wanayo haki ya kuwa na imani na viongozi wao na kutokuwa na imani na viongozi wao, na wanayo haki ya kuwaheshimu au kutowaheshimu. Lakini Kamwe hawalazimiki kuwa na imani au kuwaheshimu ati kwa vile walishinda kura. Wanayo haki ya kuwakubali kama viongozi halali waliochaguliwa kihalali, nje ya hapo is a just toss up!
 
I think we need pace kwenye mabadiliko ya mawaziri especially Fetha,Biashara na madini.Lakini JK kusafiri nje sana ni muhimu he need to give donor countries confidence and explain his vision thats why we have seen donor disbursement in time this year .KWA HILO TUMPE BIG UP

I am sorry there is no big up for JK from me as I have seen it before. Ufedhuli wake kwa kushirikiana na mafisadi katika kula pesa ya walipa kodi tena bila huruma hauwezi kukubalika katika karne ya 21.

Mwanzo alijifanya kuja na danganya toto yake na kusema mikataba inapitiwa na kila kampuni lakini matokeo yake (zero) siku zinakwenda na ndivyo wanavyozidi kujineemesha, juzi juzi tu amesema tume nyingine yaani sisi ni watoto wadogo tuliozaliwa jana tunadanganywa kwa peremende? Kuongoza nchi sio lelemama, yale yanayotokea Niger delta yanakuja Tanzania, usione watu wanarusha mawe kwa wawekezaji ukafikiri hawana akili. Rasilimali zetu zinachezewa tena na watu wa kuja kwa kushirikiana na mafisadi, its time to say no for all this nonsense.
 
wengi wao wamechaguliwa kwa rushwa na udanganyifu kwa wananchi wakichukua advantage ya umaskini wa watz kwa kuwapa tshits, kanga na vibuku tano, sasa kwa vile wabongo wengi huko rural hawajui haki yao na uvivu wa kufikiri beyond hizo shida zao ndogo wamejikuta wakiwapa madaraka bila kujua athari yake. so hakuna haja ya wao kuheshimiwa kama wao wenyewe wameshavunja heshima walopewa na hao wananchi. kuna heshima ipi wanayodai kama wanajari matumbo yao na kugawa raslimali za nchi wakijinufaisha wenyewe? kamwe sitamheshimu mtu wa aina hiyo kwa sababu hastahili, kama mkjj alivyosema respect is earned.
 
I am sorry there is no big up for JK from me as I have seen it before. Ufedhuli wake kwa kushirikiana na mafisadi katika kula pesa ya walipa kodi tena bila huruma hauwezi kukubalika katika karne ya 21.

Mwanzo alijifanya kuja na danganya toto yake na kusema mikataba inapitiwa na kila kampuni lakini matokeo yake (zero) siku zinakwenda na ndivyo wanavyozidi kujineemesha, juzi juzi tu amesema tume nyingine yaani sisi ni watoto wadogo tuliozaliwa jana tunadanganywa kwa peremende? Kuongoza nchi sio lelemama, yale yanayotokea Niger delta yanakuja Tanzania, usione watu wanarusha mawe kwa wawekezaji ukafikiri hawana akili. Rasilimali zetu zinachezewa tena na watu wa kuja kwa kushirikiana na mafisadi, its time to say no for all this nonsense.

Thanks Dua,

Naona issue kuwa kulikuwa na kamati/tume/whatever the name ya Kikwete ikiendelea kupitia madini na mikataba hata wakati Lowasa na Karamagi wakisaini mkataba wa Buzwagi London ni kitu muhimu sana hapa cha kukumbusha usaniii wa Kikwete!

Kuna watu wanataka Kikwete apewe big up hata kwa mambo ambayo ni wajibu wake kufanya. Kuna mtu hapa alidai kuwa Kikwete atukuzwe kwa kutoa mabilioni kwa kila mkoa- kitu ambacho kwanza ni uongo hizo pesa sio za Kikwete ila ni za watanzania, pili hiyo sera ilikuwa mbovu kabisa na hata watoto wadogo wenye elimu ndogo ya uchumi walijua msanii kachemsha.

Kuna siku watu watadai hapa kuwa Kikwete asifiwe kwa kumsaidia mtoto wake akapata kazi katika kampuni la mawakili wa kifisadi la IMMA - kitu ambacho ni wajibu wa kila mzazi kusaidia mtoto wake pale inapobidi!

Au kuna wengine watataka Kikwete asifiwe kwa kunawa uso asubuhi!
 
Hilo nalo ni tatizo, je ni viongozi wanaotakiwa na nchi yao? Kutakiwa na Rais Kikwete ni jambo moja, lakini kutakiwa na nchi yako kunazidi matakwa ya Rais!

Mkuu Mwenzangu MMJ,

Heshima mbele mkuu, huu uchaguzi ulikuwa ni wa CCM, sio taifa kwa hiyo ni ridhaa za mwenyekiti na anaotaka kufanya nao kazi, ili kutekeleza sera za CCM,

Kuhusu heshima mkuu, mimi ni mu-Afrika na mbongo pia, kwa hiyo nitaendeleza utamaduni na jadi zetu, za kutokubaliana ki-hoja na viongozi wetu wa pande zote mbili yaani CCM na Upinzani, huku nikiendelea kuwaheshimu, hasa wale waliochaguliwa kwa kura za wanachi,

Kama wamevunja sheria, basi ni lazima niwakemee kwa lugha kali, iwapo itathibitishwa na vyombo vyetu vya sheria kuwa ni wahalifu, kiongozi kama Ditopile, kwa kweli mwananchi akikosa heshima naye nitaelewa, lakini heshima ni kitu cha bure, JF tunheshimika kwa hoja, na sio viroja mkuu!

Otherwise, you have a point kwenye mengine!
 
kwenye hilo mzee mwenzangu tukubaliane kutokubaliana, binafsi naona huu Uafrika wa kuchagua miye simo tena... tumeamua kuvulia nguo demokrasia, we better live up to it~~
 
Kama wamevunja sheria, basi ni lazima niwakemee kwa lugha kali, iwapo itathibitishwa na vyombo vyetu vya sheria kuwa ni wahalifu, kiongozi kama Ditopile, kwa kweli mwananchi akikosa heshima naye nitaelewa, lakini heshima ni kitu cha bure, JF tunheshimika kwa hoja, na sio viroja mkuu!

Otherwise, you have a point kwenye mengine!

Mkulu,

Ndani ya bongo utasubiri miaka kibao sana watu kuthibitishwa na vyombo vya sheria kuwa ni wahalifu! Hiyo ya Dito mbona ni moja ya nyingi kibao tu zinaisha kimya kimya
 
Ah wapi,

Vasco da gama aache safari aje kushughulikia mambo ya ndani ya nchi? miezi sita iliyopita nilidhani kuwa angeweza kufanya hivyo. Baada ya hii trip yake ya mwisho ya US na yote niliyosikia na kuona yakifanyika, Kikwete hana ubavu kabisaaaa wa kuvunja baraza la mawaziri.

Hii ni kutokana na sababu mbili:

1. Kikwete na CCM wamesema kuwa issue ya ufisadi, richmonduli, kiwira, rada, BOT, ndege za rais, Buzwagi, nk ni uzushi tu toka kwa wapinzani ambao nia yao ni kuchukua madaraka tu.

Kama Kikwete akiact na kufanyia kazi hizi tuhuma basi atakuwa amesalenda kwa upinzani na kuthibitisha madai yao.

2. Serikali ya Kikwete inaongozwa kwa ushirikiano wa watu watatu ambao nao pia wana makundi yao. Kikwete ni rais ila yeye anaendeleza kazi yake ya uwaziri wa mambo ya nje, Lowasa ndiye anadeal na mambo ya ndani, wakati Rostam Aziz anashughulikia biashara zao na vyombo vya habari. Wote hawa wana watu wao katika baraza la mawaziri na wanasaidiana katika kufanya ufisadi na wizi wao.

Kuvunja baraza la mawaziri itamaanisha kuvunja nguvu na style ya kikwete ya kuongoza kitu ambacho hana bollz za kufanya!

Kikwete,

I dare you kuvunja baraza la mawaziri ili unipe sababu ya kusherekea ushindi mwingine dhidi yako baada ya ule wa wewe kunikimbia hapa USA kukwepa maswali yangu na watanzania!
Mbona mlimwandama sana
 
Back
Top Bottom