Kikwete azungumza na wazee wa Dar; ajiandaa kwa mgongano na TUCTA

MIMI NAJUA WAFANYA KAZI WA SERIKALI TAYARI WAMEGOMA, KILA MTU ANAKULA KAMKATE KAKE, hawawezi kuingia barabarani najua lakini tayari zaidi ya mwaka hakuna kazi , nikujilipa kila senti inayoingia kutoka Hazina, nakumbuka nami miaka ya Tisini nikiwa mtumisha wa Umma mshahara wangu ulikua 90800, . oooh bora nilikimbia, poleni waTanzania wenzangu.
 
Nami naisikiliza sasa, mara mahousegirl, mara wazalishaji wa maji ya kilimanjaro, mara quotation za kikwere. Nahisi kichefuchefu
 
Hii inawezekana ikawa point tokea aanze kuongea anasema mshahara anaolipwa mtu msingi wake ni mapato anayoingiza huyo mtu pia anahoji house girl akilipwa 315,000 je bosi waki atalipwa mshahara kiasi gani aweze kumlipa kiachi hico??
 
Kuhusu hela walizokalia mafisadi anasemaje?...
Asikwepe hoja..
Kwanini awaite wazee, ambao hawawezi kuhoji chochote?..kwanini asiitishe pressconference na kuruhusu maswali?..
Jibu ni..TOO MUCH USWAHILI!
 
Kuhusu hela walizokalia mafisadi anasemaje?...
Asikwepe hoja..
Kwanini awaite wazee, ambao hawawezi kuhiji chochote?..kwanini asiitishe pressconference na kuruhusu maswali?..
Jibu ni..TOO MUCH USWAHILI!

Watanzania tuelewe kuwa serikali imejaa dharau kwa wananchi wake lakini Mkwere aelewe kuwa saa imekaribia atakapoonja joto ya jiwe hawezi kutufanya wapumbavu kiasi hiki.
Wao posho za kumwaga kwetu bajeti haitoshi na ndo kundi pekee tunaolipa kodi wao aaaaaa.Mungu hawezi kuruhusu udharimu huu uendelee kwa watanzania
 
Rais wa jamhuri ya mmuungano wa tanzania akiongea na wazee wa dar es salaam
ametangaza yoyote atake goma waajiri fukuzeni mbali..akuna kiwango zaidi ya kilichotolewa mtakachopata so leo hii nawaambien wazi tucta na wenzenu mnaojichekesha kwa watu nawatangazia kama amuj=ijui serikali GOMENI...NA atakaegoma naagiza kila mmoja fukuzia mbali...m ntakuwa nyuma yenu....awa TUCTA awana maana hivi leo hii nikisema na wafanyakazi wa BARwa nyumban nao walipwe 315 000 kwa sh ngapi wanazopaa mabosi wao jamani..imefika wakati inatosha ...so kama mnataka kujaribu jaribuni ...ila si serikali
nimeagiza na muda si mrefu watatuma waraka kwenye maofisi atakaeshindwa kufanya kazi na serikali ya kikwete naomba aondoke kwa amani kabla ajaondolewa kwa aibu..
nitaendelea kuongeza mshahara kadri serikali na hali inavyoruhusu...atakaegoma tarehe tano atachukuliwa atua kama sheria za umma zinavyomruhusu
 
Kuna aina mbili za migomo, wa wazi ambao ndio huo unaofuata sheria na mwingine ambao ni mbaya kuliko wa wazi - ule ambao watumishi wamejikatia zao tamaa na wana go-slow. acha bwana, nchi ina hali mbaya hii, sasa tu hawawajibiki, je mkiacha kuwapa hiyo hela? Shame!

Hii ndo hatari itakayotokea, JK hakupaswa kuwavunja moyo wafanyakazi kwa maneno ya aina hii, maneno kama haya yalitakiwa kutoka kwa watu wa chini yake.
eti sitaki kura zenu, ... mnachozalisha hakikidhi kulipwa 315,000 kweli? hivi ame-value huduma zinazotolewa na kukuta hazifikii kulipwa kiasi hicho? na kuhusu kodi ya mapato? osh!
 
nikiwa graduates school pale UDSM MWAKA 2005, vijana wadogo pale UDSM PLUS WALE WA GRADUATES SCHOOL nililionekana ni kungi la kipekee lililoshabikia Kikwete kumshinda Mark Mwandosya na kisha kutangazwa kuwa mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM, Wasomi wa kada mbalimbali hapa TZ waliwaaminisha wananchi wa TZ kwamba tangu baada ya JK nYERERE nchi imepata mkombozi wa aina yake , mwenye haiba na muonekana sawa wa Julius..
wakulaumiwa ni wasomi na wakazi wa mijini kwa kumshabikia rais legelege, rais asieweza kutembea katika maneno yake, rais mpenda makuu, rais anaeshindwa hata kudhibiti familia yake, maana kila mara Ridhwani huchafua hali ya hewa katka chama chao.

Rais asieweza kusimama mbele ya Wafanyakazi maana anaona aibu. kwa hali ya maisha ya leo unamlipa mtu Tsh100,000, kisha unajisifu umemboreshea maslahi yake.

Umenikumbusha jinsi wanafunzi wa UDSM walivyokuwa wanagombania Tshirt za CCM pale geti maji, hakika safari bado ni ndefu sana.
 
anasema hata mgome miaka nane kima cha chini hicho hakipatikani. In other words tutabakia kuwa masikini na hela haitapikana kamwe. Vision ya kukua uchumi haipo. Kasema kama hamtaki acheni kazi, ondokeni. When I hear this, I shudder!

Rais anatamka maneno haya! naona ameanza kurudisha akili yake kwenye ukanali wake (ujeshi).
 
dr. W. Slaa nakuona uko humu

naomba maoni yako katika hili tafadhali

ni sahihi alivyosema huyu Rais?
 
Hao wazee aliyowakusanya sio wale wazee wa kiswahili wanaoshinda katika vijiwe vya Dar kweli? Alitakiwa apeleke mziki kwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari. Halafu mh. Asichofahamu hao wafanyakazi laki tatu na nusu ndio tegemezi la karibu asilimia 75 ya waTz m45 anazozitaja.
 
Daa kweli watanzania tu wapumbavu,wanavyomshangilia Jk na hotuba yake wala siamni kam kweli wao ndio wazee wa Dar.Yaani wanamshangilia mpaka JK mumkari inampanda na kuzidi kubwabwaja kama yuko jukwaani vile.Lol

Kwani ulitegemea nini hapo?hamna kitu na utashangaa zaidi utakavyoona wafanyakazi wakienda kazini kama kawaida, na wafanyakazi watasema wao wana imani kubwa na serikali ya Kikwete na kuwa mgomo ulipangwa tu na viongozi wao na wao hawakushirikishwa kabisa katika hilo.
 
Naona kina Kibonde na Gadna wanamsifu Kikwete kwa kuwatusi wafanyakazi, anasema anaungana na serikali kuwa 315000 serikali haina hiyo pesa. Gadna asema ni upumbafu akichombeza maneno ya Mpuuzi Kibonde.
 
huyu amejisema tu hayo

hivi tukianza mgomo kama ule wa bankok huyu atarudia kauli zake kweli hizi kweli

shime wafanya kazi wenzangu hapa ndo pa kutokea lazima tugome kabisa
 
Mheshimiwa rahisi ni vyema angejua ni kwa sababu gani kima cha chini kinachodaiwa ni kikubwa mno. Usimamizi wako mbovu wa mifumo ya uzalishaji, usambazaji na ugavi wa kipato ndio umeleta yote haya. Kama leo hii kilo ya Unga wa Sembe isingekuwa TSh. 850, lita ya petroli Tsh 1705, gharama za kujenga barabara za lami bilioni 1 kwa kilometa n.k, watu wasingedai kima cha Tsh 315,000.

Maisha magumu huku mtaani kaka ila sidhani wewe mwenzetu mwenye kasri pasi pango pale Magogoni, magari bwererere ya kukusafirisha, ndege ya bure ya kutumia, nyumba pale Regent Estate na niyngine nyingi kwenye kona mbalimbali za nchi hii walitambua hilo.
 
CHADEMA mmejazana humu kumponda rais wetu? Kwenu nyie rais ni Mbowe tu ambaye hata kwenye chama ili ashinde mpaka abebwe na mkwe.
 
Naona kina Kibonde na Gadna wanamsifu Kikwete kwa kuwatusi wafanyakazi, anasema anaungana na serikali kuwa 315000 serikali haina hiyo pesa. Gadna asema ni upumbafu akichombeza maneno ya Mpuuzi Kibonde.

Waoneeni Huruma Gadna na Kibonde, wakitoka Clouds wataenda wapi? wanawania matangazo ya CCM ya uchaguzi yawatoe na wao! I hate thsi, when a man with balls cannot speak the truth, what is in his mind, and be a puppet. Mi ningekuwa serikalini ningegoma na hiyo ingekuwa legacy nitakayoacha kwa watoto na wajukuu zangu. Tulipigwa virungu vya polisi UD na shule tukamaliza, itakua kazi? Tena mtu umesoma? Mimi singeenda, full stop and shame to you all who will not support this. Am out, nimekasirika sanaaaa
 
Back
Top Bottom