Kumbe nilikuwa simjui vizuri sana huyu raia eeh!...Badala ya kujibu hoja unawatisha wananchi waliokuchagua kwa kutumia POLISI?...kWELI mvi SIO BUSARA!Hotuba nimeanza kuisikiliza kati lakini naona topic muhimu anayozungumzia ni mugomo wa Wafanyakazi (watumishi, waajiliwa) kama ulivyotangazwa na TUCTA.
Sijui itaishia wapi lakini naona hapo alipo nimeshangaa. Kwanza ni choice ya audience yake, 'wazee wa Dar es Salaam' Kama ni wazee kwa maana ya siku zote naona kama siyo watumishi wa Serikali. Muenendo naona anatoa hotuba kwa washabiki (nilitegemea hili) maana wanashangilia hata bila sababu.
Baya ambalo sikutegemea, ni jinsi alivyoahidi kwamba wakigoma na kuandamana, watapigwa na polisi. Huyu ni Rais na naamini anafahamu nguvu ya maneno yake, Sijui ni kwa nini anaelekeza tendo kama hilo. Anazidi kusema Polisi watawaumiza. Kakumbusha uwezo wa polisi kuua kama ilivyowahi kutokea huko nyuma.
Ok, vyovyote itakavyokuwa ktk hotuba hii, binafsi sifahamu ni kwa nini hotuba za viongozi wetu hazitofautiani na zile za Mugabe. Tusubiri anakoishia.
Mkwere ni mkwere tu bana...Jasiri haachi asili...Huu ni ushakunaku wa juu kabisa!Anasema kwa kejeli kuwa hana haja na kura za wafanyakazi wanaodai ongezeko la kima cha chini cha 315,000 kwani serikali ya CCm haina uwezo wa kutimiza ahadi hiyo hivyo kura zao ndio amezikosa hivyo wakitaka wawapigie upinzani
Anasema Tanzania ina wafanyakazi takribani laki 3.5 kati ya Watanzania 45m hivyo hawezi kutumia mapato ya Watanzania wote kuwaridhisha wafanyakazi wachache hiyo ni DHULUMA. Wafanyakazi hata wakigoma bado mshahara hautapanda...kwani madai yao hayatekelezeki.