Kikwete akumbana na zomeazomea Mbeya...

Wa mmoja

Member
Aug 4, 2009
99
0
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete jana aliendelea na mikutano yake ya kampeni katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Mbeya ambapo wananchi walimpa matumaini makubwa ya ushindi lakini wagombea ubunge wawili walizomewa.

Kikwete aliwasili mkoani Mbeya jana na kuanzia kampeni zake kwenye mji mdogo wa Tunduma ambao uko mpakani mwa Zambia na ambao una pilikapilika nyingi za wafanyabiashara wa Tanzania na nchi hiyo jirani.

Tofauti na mikutano mingine ya kampeni katika majimbo mbalimbali ambayo ameshatembelea kwenye kampeni zake, Kikwete alikumbana na hali isiyo ya kawaida wakati alipowanadi kwa nyakati tofauti wagombea hao wa majimbo ya Nkasi Kusini, Desderius Nipata na wa Mbozi Kusini, Lucas Siyame.

Tukio la kwanza la kuzomea lilitokea kwenye Uwanja wa Kate, ulio katika Kata ya Kate ambako wananchi walizomea baada ya mgombea wa Jimbo la Nkasi kuwataka wampigie kura Kikwete.

Lakini alipoanza kuomba wananchi hao wampigie kura na yeye ili afanye kazi na Kikwete, wananchi hao walianza kumzomea.


Source: Mwananchi 30/08/2010
 
atajiju...........hiyo ni rasharasha tu mvua yenyewe bado...
 
Vyombo vya habari havitaki kuitangaza hii.
Sio havitaki,vingi vinaogopa!
But naona mwananchi wamekuwa wabishi kidogo,hivi karibuni mwandishi wao alipigwa pini kuufwata msafara wa kikwete kuelekea kwenye kampeni za CCM!
 
Back
Top Bottom