Mpanda Merikebu
Senior Member
- Dec 27, 2007
- 170
- 2
Chifu,
Sinuii kukukatisha tamaa, kamwe hiyo si hulka yangu. Hata kama sintokubaliana nawe, sitaota kukukatisha tamaa. Kitu ninachotaka uelewe ni kwamba, jinsi ulivyoandika inaonyesha inataka mambo yafanywe kienyeji.
Hata kama serikali ya Marekani itataka kumrudisha Ballali, haiwezi ikajiamulia tu kufanya hivyo bila kuombwa rasmi na serikali ya Tanzania. Hata kama wakiombwa, ujue kuwa kwa vile Ballali ni mkazi wa kudumu wa Marekani, serikali ya Marekani inaweza ishindwe kumrudisha kwani huko kutakuwa ni njia panda kati ya kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania na kumlinda mtu mwenye kustahili kuishi na kufanya kazi huku.
Kama nilivyoeleza hapo awali, suala hili ni nyeti na lina mtandao wa watu wengi na kufanya mambo kienyeji kutapelekea kukosa hata hilo suluhisho la kudumu. Cha msingi ni kuendelea kuihoji serikali ni kwanini hawawafungulii mashtaka wahusika wote (japo Ballali ni conduit tuu), kina Patel, Lukaza, Mushis (not sure if you're related), na hata wale walioidhinisha malipo haya na Ballali, watu kama kina Mramba, Mgonja etc. Kuishinikiza serikali kwa kila namna ndio njia pekee ya kutafuta suluhisho lakini sio propaganda na udaku wa kutoa tafsiri isiyo sahihi na yenye kuleta uchochezi.