Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Kitu kingine nimekisoma hapo ni kuwa hao madereva walishakuwepo hapo kwa muda na kupata tayari mafunzo ya magari hayo..
Kitu kingine nimekisoma hapo ni kuwa hao madereva walishakuwepo hapo kwa muda na kupata tayari mafunzo ya magari hayo..
Hivi maafisa wote Ikulu hawakugundua tofauti kati ya Longido na Loliondo hadi Rais mwenyewe!? Mnajua huko aliko mwenyewe anajipongeza kuwa amesevu na gazeti la Daily News na mengine ya serikali yatatoa pongezi kubwa kwa Rais huku yakilaumu watendaji wake.
Yah niliona kwenye habari ya jana mkuu,muungwana alionekana kuchukia,lakini mpaka sasa sielewi kuwa mpaka rais anatoka ofisini hakujua anaenda kumpa nani gari?,je huyo mkurugenzi aliyenyimwa hilo gari halihitaji(na maana kwake hakuna uhaba wa magari ya kubeba wagonjwa?).Anyway tuwaachie wenyewe bwana na protocal zao
Nimesikiliza Clouds FM asubuhi hii wakimhoji DED wa Longido. Anyway,kuhojiwa kwake sio hoja ila nilishangazwa na jinsi Clouds walivyoamua kumfagilia JK kwamba ni Rais mwenye kumbukumbu nzuri sana kutokana na utendaji mzuri. Aibu kwa Clouds! wametengeneza mpaka katangazo kwamba Rais si mchezo hadanganyiki.
Upotoshaji na kujikomba tupu.
Kwani hao wasaidizi wake alishushiwa toka Mbinguni? Team ya kutenda nayo kazi kaiandaa mwenyewe, na kubambikizwa mambo hakukuanza leo na bado anao tuu. Kikombe hicho lazima akinywe mwenyewe.Mimi nakubaliana na clouds FM, hao wahusika wa Ikulu wajiuzulu kabisa maana kama dogo hivi hawawezi je kubwa wataliwezea wapi? Inaonekana walikuwa na njama zao za kutaka gari iende sehemu nyingine na ndio maana hawakumwambia JK, mtu ameingia mpaka Ikulu and I am sure alisachiwa pia kama ana chochote cha kudhuru, saa zote hizi hawakuweza kugundua kweli? Si bure walikula njama hawa na Jk akawashtukia...
Hivi hicho kitengo cha habari Ikulu kina tatizo gani? Ni professionalism ndogo au ni mzaha? Kwa nini huyo mkurugenzi wake asijiuzulu tu? Mara nyingi migongano kibao ya habari na bado Mh. Rais anamvumilia tu. Hayo ndiyo matatizo ya kubeba vibaraka wa maswahiba huku uwezo hawana. Itabidi habari maelezo wachukue jukumu la kusemea habari za nchi maana hicho kitengo cha habari Ikulu bomu la nuclear kabisa.
Umesema ukweli kabisa na hii yote ni Kampeni na kuona kuwa jinsi gani wapo makini,. sasa kama umakini kwa mambo madogo kama haya haupo basi mengine ni hatari kabisaTatizo la JK anaaibisha Ikulu yetu. Kutaka publicity sana kuna mgharimu. Tumechoshwa kusikia failures zinazoihusu ikulu hata kwa masuala madodo madogo kama haya.
vitu vingine vidogo vidogo kama hivi angelikuwa anawaachia wasaidizi wake wahusike navyo. Anajaribu kujiaibisha na intelligence yake/yetu bureeee!!. Wakati fulani, hata kama kuna udhaifu kwenye nyumba, mama au baba hujaribu kujistiri kidogo!
JK hajifunzi tu? Juzi juzi tu hapa katuacha hoi na ile hotel ya Arusha, hatujakaa sawa mkenge na CMC.
Uozo wa CMC tunaufahamu. Wahindi hawa, wanadhurumu mali ya wa TZ kwa kukwepa kodi, halafu wanatumia pesa walizokwepa kodi nk, kujifanya wanatoa misaada. Huu ni uhuni!
Kwa JK
Mh Rais unatuaibisha. Kwa nini kujihusisha husisha na uzinduzi wa vitu vidogo vidogo ambavyo hata havijawekwa sawa??. Kama, ndiyo njia ya kutaka mass support, poa! Ngoja nimalizie kajumba kangu, nami nianze kuwasiliana na wakuu wa itofaki; wakulete uje ukazindue. Huku utashangiliwa sana!
Ila ujapo uje na majibu ya swali hili: Wewe hauoni unatuaibisha kwa kujihusisha husisha na uzinduzi wa shughuli ndogo ndogo ambazo zingefanywa na wasaidizi wako wakiwemo wakuu wa wilaya?????
Duuh hatariRAIS Jakaya Kikwete jana aligoma kukabidhi gari la msaada wa kubeba wagonjwa, tukio hilo lililotokea katika viwanja vya Ikulu mbele ya maofisa wa Ikulu wakati Rais Kikwete alipoonesha kusita kulikabidhi baada ya utambulisho uliomfanya agundue kuwa aliyefika kukabidhiwa gari ni wa Ngorongoro badala ya Longido.
Gari hilo lililotolewa msaada na Kampuni ya CMC Automobiles Limited, lilipaswa kupewa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Arusha, lakini kwa mshangao wake, jana alifika mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Kayange Jacob.
Wewe ni nani... ahaa, umetokea Loliondo, ahaa hii gari si ya kwako bwana, sikupi.si yakohii ni ya watu wa Longido si Loliondo, wewe ni nani kakutuma? Kayange alimueleza Rais Kikwete kuwa ametumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isdori Shirima. Rais Kikwete aliwageukia maofisa wa Ikulu, Hii ni nini? Hii ni kashfa, waombeni radhi hawa mliowaalika bwana.
Mimi mwenyewe nilifika katika kijiji hicho nikiwa katika ziara na moja ya ahadi zangu kwao baada ya kukuta hali walionayo katika kubeba wagonjwa kijijini hapo, niliwaahidi nikipata msaada wa gari, nitawapelekea na si hawa wa Loliondo, hii ni nini, hii ni kashfa, alirudia kusema Rais Kikwete.
Hata hivyo, juhudi za Maofisa wa Ikulu, kumfafanulia rais Kikwete aligoma na kuondoka kurudi ofisini (ndani) na kuendelea na kikao kingine kilichokuwa kikimsubiri. Kayange hakuamini macho yake alipoachwa peke yake baada ya rais kutokomea ofisini huku akilalamika what is this....bwana.
WanaJF mnatoa maoni gani kuhusu hili sakata kwa rais wetu............