Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,461
- 39,928
Kitu kingine nimekisoma hapo ni kuwa hao madereva walishakuwepo hapo kwa muda na kupata tayari mafunzo ya magari hayo..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kitu kingine nimekisoma hapo ni kuwa hao madereva walishakuwepo hapo kwa muda na kupata tayari mafunzo ya magari hayo..
Hivi maafisa wote Ikulu hawakugundua tofauti kati ya Longido na Loliondo hadi Rais mwenyewe!? Mnajua huko aliko mwenyewe anajipongeza kuwa amesevu na gazeti la Daily News na mengine ya serikali yatatoa pongezi kubwa kwa Rais huku yakilaumu watendaji wake.
Yah niliona kwenye habari ya jana mkuu,muungwana alionekana kuchukia,lakini mpaka sasa sielewi kuwa mpaka rais anatoka ofisini hakujua anaenda kumpa nani gari?,je huyo mkurugenzi aliyenyimwa hilo gari halihitaji(na maana kwake hakuna uhaba wa magari ya kubeba wagonjwa?).Anyway tuwaachie wenyewe bwana na protocal zao
Nimesikiliza Clouds FM asubuhi hii wakimhoji DED wa Longido. Anyway,kuhojiwa kwake sio hoja ila nilishangazwa na jinsi Clouds walivyoamua kumfagilia JK kwamba ni Rais mwenye kumbukumbu nzuri sana kutokana na utendaji mzuri. Aibu kwa Clouds! wametengeneza mpaka katangazo kwamba Rais si mchezo hadanganyiki.
Upotoshaji na kujikomba tupu.
Kwani hao wasaidizi wake alishushiwa toka Mbinguni? Team ya kutenda nayo kazi kaiandaa mwenyewe, na kubambikizwa mambo hakukuanza leo na bado anao tuu. Kikombe hicho lazima akinywe mwenyewe.Mimi nakubaliana na clouds FM, hao wahusika wa Ikulu wajiuzulu kabisa maana kama dogo hivi hawawezi je kubwa wataliwezea wapi? Inaonekana walikuwa na njama zao za kutaka gari iende sehemu nyingine na ndio maana hawakumwambia JK, mtu ameingia mpaka Ikulu and I am sure alisachiwa pia kama ana chochote cha kudhuru, saa zote hizi hawakuweza kugundua kweli? Si bure walikula njama hawa na Jk akawashtukia...
Hivi hicho kitengo cha habari Ikulu kina tatizo gani? Ni professionalism ndogo au ni mzaha? Kwa nini huyo mkurugenzi wake asijiuzulu tu? Mara nyingi migongano kibao ya habari na bado Mh. Rais anamvumilia tu. Hayo ndiyo matatizo ya kubeba vibaraka wa maswahiba huku uwezo hawana. Itabidi habari maelezo wachukue jukumu la kusemea habari za nchi maana hicho kitengo cha habari Ikulu bomu la nuclear kabisa.
Umesema ukweli kabisa na hii yote ni Kampeni na kuona kuwa jinsi gani wapo makini,. sasa kama umakini kwa mambo madogo kama haya haupo basi mengine ni hatari kabisaTatizo la JK anaaibisha Ikulu yetu. Kutaka publicity sana kuna mgharimu. Tumechoshwa kusikia failures zinazoihusu ikulu hata kwa masuala madodo madogo kama haya.
vitu vingine vidogo vidogo kama hivi angelikuwa anawaachia wasaidizi wake wahusike navyo. Anajaribu kujiaibisha na intelligence yake/yetu bureeee!!. Wakati fulani, hata kama kuna udhaifu kwenye nyumba, mama au baba hujaribu kujistiri kidogo!
JK hajifunzi tu? Juzi juzi tu hapa katuacha hoi na ile hotel ya Arusha, hatujakaa sawa mkenge na CMC.
Uozo wa CMC tunaufahamu. Wahindi hawa, wanadhurumu mali ya wa TZ kwa kukwepa kodi, halafu wanatumia pesa walizokwepa kodi nk, kujifanya wanatoa misaada. Huu ni uhuni!
Kwa JK
Mh Rais unatuaibisha. Kwa nini kujihusisha husisha na uzinduzi wa vitu vidogo vidogo ambavyo hata havijawekwa sawa??. Kama, ndiyo njia ya kutaka mass support, poa! Ngoja nimalizie kajumba kangu, nami nianze kuwasiliana na wakuu wa itofaki; wakulete uje ukazindue. Huku utashangiliwa sana!
Ila ujapo uje na majibu ya swali hili: Wewe hauoni unatuaibisha kwa kujihusisha husisha na uzinduzi wa shughuli ndogo ndogo ambazo zingefanywa na wasaidizi wako wakiwemo wakuu wa wilaya?????