Kikwete agoma kutoa misaada ya Ambulances; Ikulu yaboronga!

Kwa kweli tukio la mkulu kung'aka ni kusikitisha na hii inaonyesha ni jinsi gani asivyopenda kudelegate minor issues kama hii. Aidha ilipaswa awe well informed na wasaiduzi wake kabla ya kwenye hiyo hafla. It is ridiculous..!
Mnakumbuka kung'aka ndo zake?
Alipotembelea Richmond wakati ule,
alikuta hata mitambo haijafungwa...
akasema huu ndo Us***e nisioutaka!!!
 
halafu kwanini anafikiri hii ni 'kashfa'

Unajua mkubwa hakosei atakuwa alipitiwa na akaona hii ndo kashfa kubwa ya kumwalika mtu ambae hakustahili kupokea huo msaada wa Ambulance by the way nani katoa hayo magari amenunua mwenyewe Rais au ndo msaa wa hiyo kampuni?
 
halafu kwanini anafikiri hii ni 'kashfa' sidhani kama ni kashfa tu the extent ya majumba ya Benki Kuu, Meremeta, n.k hayo yote hajawahi kuita ni kashfa! mweh.. Inawezekana kweli kuwa kulitokea mchanganyo kidogo lakini siyo kashfa kubwa hivyo kiasi cha kufukuzisha watu kazi..

Katika orodha ya kashfa zinazokabili taifa letu hii wala siyo kashfa! Tukikubali tutashangilia akiwafukuza watu au kuwawajibisha hawa watu huku zile kashfa zenyewe watu wake wakiendelea kupeta
mkurugenzi aliyekuja alimweleza ametumwa na mkuu wa mkoa ambaye naamini ni mwakilishi wa raisi mkoani arusha. Iweje asimkambidhi na kummwelekeza mkuu wa mkoa akabidhi longido kwa niaba yake!!!!

halikuwa jambo la kuita kashfa!!!!
 
Aisee jana ilikuwa aibu sana,yaani rais ametoka mpaka anakaribia kugawa gari kumbe ameletwa mtu mwingine? Kwanini watu wa Longido hawakuja?

Yaani ilikuwa kama mchezo wa kuigiza ina maana watu hajui wajibu wao hadi mkuu wao wa kazi anatambua kabisa mlengwa alikuwa nani na wao wameleta mtu mwingine
 
Kwanza kabisa nampa pole mheshimiwa rais kwa jinsi ambavyo wasaidizi wake wanavyoendelea kumuaibisha kila kukicha.

Mtizamo wangu ni huu:

1. Ajira ndani ya ikulu na za wasaidizi wa Rais ziangaliwe upya
2. Waliohusika na matukio yote ya kumuaibisha rais wafukuzwe kazi
3. Idara ya itifaki ikulu ifanyiwe marekebisho makubwa, Sikuwahi kuona wakati wa Sisco kukiwa na mauza uza ya kumuabisha rais
4. Ikulu ni mahali patakatifu patumike kwa shuguli zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na si kila shughuli ifanyike pale
5. Mheshimiwa Rais kuna kila dalili za kukuhujumu angalia tena team ya wasaidizi wako

MATUKIO YALIYOMUABISHA RAISI

1. Ufunguzi wa Arusha Hotel
2. Kugawa gari state house
3. Itifaki kuvunjwa na mke wa mgeni wa Rais kuingia katika gari la Rais mwenyeji na mgeni wake
3. Walinzi wa Rais kupigana na waandishi wa habari mbele ya Rais
4. Ujio wa kombe la dunia

TAFAKARI MHESHIMIWA RAIS NA CHUKUA HATUA...
 
Nadhani JK angeweza kushughulikia suala la kutumwa/uwakilishi wa mtu mwingine kwa style tofauti na ikaonyesha ustaarabu zaidi. Sasa kumshushua Mkurugenzi ambae ametumwa na Mkuu wake wa Mkoa kumuwakilisha mwenzie imekuwa kashfa?

Mimi nilidhani angeendelea na jukumu lake la kukabidhi gari, halafu angewasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, na kumuambia kuwa hilo gari ni ahadi aliyoitoa kwa wilaya ya Loliondo na angetaka liwafikie. Nadhani hiyo ingetosha kuhakikisha kuwa ahadi yake inafika.

Vinginevyo, nadhania anataka watakaosikia kuwa amekataa kukabidhi gari kwa wilaya tofauti, wajue kuwa hata ahadi alizotoa kwao atahakikisha haziendi kwingine. Ni trick ya kisiasa ila isiyofaa.

Madhara kwa serikali yake ni makubwa mno.
 
Unajua mkubwa hakosei atakuwa alipitiwa na akaona hii ndo kashfa kubwa ya kumwalika mtu ambae hakustahili kupokea huo msaada wa Ambulance by the way nani katoa hayo magari amenunua mwenyewe Rais au ndo msaa wa hiyo kampuni?
kama kuna jambo najua JK analijuutia ni kuwa na Wateule wake wasio faa hata kuonngoza mitaa, kwangu mimi naamini JK alitaka kutoa ujumbe kua amezungukwa na watendaji wa hovyo, akisahau kua ni yeye alie wateua.
 
Kwa mara nyingine tena inathibitisha yale tunayoyasema muda mrefu hapa kwamba Ikulu kuna watu wengi hawastahili kuwa pale. Hawana umakini wala ujuvi wa kujua utakatifu unaoendana na Ikulu.
Endeleeni tu kujaza watu sehemu nyeti kwa kujuana na urafiki. Ipo siku itatokea aibu kubwa kuliko hii ya kugawa magari. Lakini hakuna mwingine wa kumlaumu isipokuwa ni wao wenyewe watawala kwa kutofuata maadili ya uongozi na kuendeleza urafiki na kubebana.
 
naamini JK SASA analielewa somo kuwa wasaidizi aliowateua ni vimeo, uteuzi wake unamgharimu, wanashidwa kumsaidia na kumuokoa kutoka kwenye aibu kama hizo, walitakiwa wao kugundua makosa kabla ya JK.

kUMBUKENI MKASA WA JK kwenda kuzzindua kivuko daraja hewa kule mto Ruvuma miaka miwili nyuma, kumbuka mkasa wa JK kuzindua Hotel yenye matatizo ya kujengwa kwenye hifadhi ya barabara kule Arusha, ni milolongo hadi kufikia JK kupigwa mawe MBEYA, hana wasaidizi makini kwa sababu hakuwa na uteuzi makini.
Unategemea nini kama process of raising the ranks of your team is merited by friendship? Watu wababaishaji, wenye kujiweka kimbelembel ndio wanachukuliwa kama hardworkers wenye kustahili kukaa hata hizi sehemu nyeti. Kwangu mimi Ikulu inaakiwa watu waliotulia kiakili na wenye kutumia akili hizo ili image yetu kama nchi isiharibiwe.Ikulu sio kijiwe cha saigoni!
Tuache kuajiri watu kwa style ya 19th century na kuwajaza kwenye kazi nyeti ilhali tunajua hawana uwezo. 19th century watu walikuwa wanaajiriwa kwa kigezo kimoja tu, kwamba wana mikono ya kufanyia kazi.Hawakuwa na elimu na kazi zao nyingi zilikuwa ni za kutumia nguvu tu. Leo hii kama tunataka kufanikiwa lazima tuajiri kufuatana na hali halisi ilivyo, kwamba skills based on knowledge must be the priority wakati tunaajiri, especially hizi ofisi nyeti.
 
Nadhani JK angeweza kushughulikia suala la kutumwa/uwakilishi wa mtu mwingine kwa style tofauti na ikaonyesha ustaarabu zaidi. Sasa kumshushua Mkurugenzi ambae ametumwa na Mkuu wake wa Mkoa kumuwakilisha mwenzie imekuwa kashfa?

Mimi nilidhani angeendelea na jukumu lake la kukabidhi gari, halafu angewasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, na kumuambia kuwa hilo gari ni ahadi aliyoitoa kwa wilaya ya Loliondo na angetaka liwafikie. Nadhani hiyo ingetosha kuhakikisha kuwa ahadi yake inafika.

Vinginevyo, nadhania anataka watakaosikia kuwa amekataa kukabidhi gari kwa wilaya tofauti, wajue kuwa hata ahadi alizotoa kwao atahakikisha haziendi kwingine. Ni trick ya kisiasa ila isiyofaa.

Madhara kwa serikali yake ni makubwa mno.

Safari hii haina mwisho
 
mi nazani kuna tatizo kubwa katika haya yote....huenda raisi n mbishi na anataka kufanya anavyotaka yeye au wasaidizi wke wanamfanyia kitu kibaya au ni uozo uliopo kwa hiyo kila mtu anaona bora liende, hakuna wakumshika mwingine,hivi mbona ile aibu ya hotel ya arusha ilikuwa mbaya sana,ni wakati raisi afanye ya muhimu...naaza kuhisi hawa wasaidizi wakati mwininge wana ajenda ya siri,kumharibia JK
 
RAIS Jakaya Kikwete jana aligoma kukabidhi gari la msaada wa kubeba wagonjwa, tukio hilo lililotokea katika viwanja vya Ikulu mbele ya maofisa wa Ikulu wakati Rais Kikwete alipoonesha kusita kulikabidhi baada ya utambulisho uliomfanya agundue kuwa aliyefika kukabidhiwa gari ni wa Ngorongoro badala ya Longido.

Gari hilo lililotolewa msaada na Kampuni ya CMC Automobiles Limited, lilipaswa kupewa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Arusha, lakini kwa mshangao wake, jana alifika mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Kayange Jacob.

“Wewe ni nani... ahaa, umetokea Loliondo, ahaa hii gari si ya kwako bwana, sikupi….si yako…hii ni ya watu wa Longido si Loliondo,” wewe ni nani kakutuma?” Kayange alimueleza Rais Kikwete kuwa ametumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isdori Shirima. Rais Kikwete aliwageukia maofisa wa Ikulu, “Hii ni nini? Hii ni kashfa, waombeni radhi hawa mliowaalika bwana.”

“Mimi mwenyewe nilifika katika kijiji hicho nikiwa katika ziara na moja ya ahadi zangu kwao baada ya kukuta hali walionayo katika kubeba wagonjwa kijijini hapo, niliwaahidi nikipata msaada wa gari, nitawapelekea na si hawa wa Loliondo, hii ni nini, hii ni kashfa,” alirudia kusema Rais Kikwete.

Hata hivyo, juhudi za Maofisa wa Ikulu, kumfafanulia rais Kikwete aligoma na kuondoka kurudi ofisini (ndani) na kuendelea na kikao kingine kilichokuwa kikimsubiri. Kayange hakuamini macho yake alipoachwa peke yake baada ya rais kutokomea ofisini huku akilalamika what is this....bwana.

WanaJF mnatoa maoni gani kuhusu hili sakata kwa rais wetu............

Mmh kazi ipo.Yaani hawa jamaa wanmdanganya mpaka Rais?au walimuelewa vibaya Rais?
 
Tatizo ni kuwa Rais huyu Kikwete anateua watu kwa urafiki/ushkaji bila kuangalia uwezo, utendaji na umakini wa mhusika. haya yamesemwa kwa muda mrefu tu, blunders za aina hii zinaendelea tu kutokea sana kwenye Serikali yake.

Tatizo jingine ni kuwa anapenda sana publicity hata kwa mambo yasiyomlazimu yeye kuwepo, kwa mfano za juzijuzi tu kama:
-Kufungua hoteli Arusha iliyo kwenye hifadhi ya barabara,
-Kupokea ambulance mbili toka kwa muhindi, na sasa hili hapa.

Alichofanya hakistahili kusifiwa (There was a better way to react than that), bali ni kielelezo cha kutokuwa na watu makini Ofisini kwake hapo Ikulu.

Mambo ya uteuzi wa kishkaji hayo...
 
Tugari tuwili ndo unakuja kugawa+waandishi wa habari..
Mkulu please be serious...
Kuna mengi ya kufanya sio hilo..
 
JK ameonyesha kuwa ahadi zake anazozitoa anazikumbuka kuliko hata hao wasaidizi wake na hao anaoambatana nao kwenye misafara mirefu ya gharama kubwa kumbe hata hawatilii maanani anachokiongea huko. Hongera JK, la MAISHA BORA kwa kila MTZ limekaaje? 2010 hii!
 
halafu kwanini anafikiri hii ni 'kashfa' sidhani kama ni kashfa tu the extent ya majumba ya Benki Kuu, Meremeta, n.k hayo yote hajawahi kuita ni kashfa! mweh.. Inawezekana kweli kuwa kulitokea mchanganyo kidogo lakini siyo kashfa kubwa hivyo kiasi cha kufukuzisha watu kazi..

Katika orodha ya kashfa zinazokabili taifa letu hii wala siyo kashfa! Tukikubali tutashangilia akiwafukuza watu au kuwawajibisha hawa watu huku zile kashfa zenyewe watu wake wakiendelea kupeta

Kwa mwendo huu huenda hata hizo za BOT na meremeta anapelekewa mezani taarifa potofu hivyo anaona hakuna tatizo.
 
Ikulu imeoza. Tunahitaji mtu wa kutusitiri kwa haya maozo yanayotokea kila siku. Najiuliza kwa nini alaumiwe Dobi kwa kushindwa kutakatisha kaniki wakati rangi ya nguo yenyewe ni bayana?
 
MATUKIO YALIYOMUABISHA RAISI

1. Ufunguzi wa Arusha Hotel
2. Kugawa gari state house
3. Itifaki kuvunjwa na mke wa mgeni wa Rais kuingia katika gari la Rais mwenyeji na mgeni wake
3. Walinzi wa Rais kupigana na waandishi wa habari mbele ya Rais
4. Ujio wa kombe la dunia

TAFAKARI MHESHIMIWA RAIS NA CHUKUA HATUA...

Wadanganyika tunauwezo mkubwa sana wa kusahau haraka.... Tumeshasahau kwamba muungwana alishawahi kupewa cheque ambayo tarakimu zake zinatofautiana sana na fedha halisi zilizotakiwa kuandikwa kwenye cheque!!
 
Tugari tuwili ndo unakuja kugawa+waandishi wa habari..
Mkulu please be serious...
Kuna mengi ya kufanya sio hilo..

Jamani inatakiwa muelewe rais naye huwa anaomba kwa rafiki zake na haya magari aliyaomba kutoka CMC kwani ni rafiki zake/wanategemea msamaha wa kodi. Kwa hiyo wanapomwambia kuwa alicho waomba kipo tayari ni lazima wamkabidhi yeye na yeye anatekeleza ahadi zake kwa njia hii.
 
Wadanganyika tunauwezo mkubwa sana wa kusahau haraka.... Tumeshasahau kwamba muungwana alishawahi kupewa cheque ambayo tarakimu zake zinatofautiana sana na fedha halisi zilizotakiwa kuandikwa kwenye cheque!!
Aliyakataa mapanki ya Mwanza, akaambiwa pia kuwa ile kampuni, BAE, iliyotuuzia rada ni mali ya serikali ya Uingereza, Rais wetu wasaidizi anao!
 
Back
Top Bottom