Kikwete aambulia "C" kwa ubora wa marais AFRICA

KUTOKANA NA SCORES ZA HILO DARASA, NADHANI AMEJITAHIDI KWANI KUNA MAKSI HADI ZA ICU... aisee
 
Mimi siyo mpenzi wa JK lakini hizi data za kipuuzi tu. Waweke namna pia ya kuzipima nchi kama US au Germany, hasa pale nchi kama US zinavyovamia nchi zingine kimabavu na kuuwa watu bila hatia? Hapa kuna ajenda ya siri kama vile The International criminal court ambazo zimeanzishwa kwa ajiri ya nchi masikini, huku nchi zingine zikikosa institutions za kuzichunguza na kuzipima utendaji wao. Moe Ibrahim anachofanya ni kucontain utendaji kazi wa viongozi wa nchi maskini ila kila kiongzi aji-tune kwenye wimbo wa human right and good governance, huku ikifahamika wazi kuwa, agenda hiyo wala haitaweza kuleza maendeleo kwa nchi maskini zaidi ya kuzifanya nchi hizi kubakia ombaomba milele. Ndio maana kiongozi mama Kagame anapata D wakati inaelewaka wazi nini anakifanya kwenye nchi yake
 
mmmh! hiyo tume iliyo fanya hiyo tathmini ingekuwa chini ya Tendwa, nahisi JK angechomoka na A++++, ukikaribisha na kauzurulaji kwa karibu, mmmmh! angeng'oka na terrible kabisa siyo honour
 
Kama matokeo yenye kwa nchi zingine za Africa ndo haya, basi Tanzania imejitahidi sana. Kwa Africa Mashariki imeburuza nchi zote kasoro Kenya ndo wametupita kidogo. Hizo nyingine za Africa ndo hohehahe totally, has huo upande wa kulia....

kwa nini una tu fananisha sisi na walio na grade za chini?
Tanzani ilivyo inatakiwa kuwa A.. lakini sasa tuko C tutarudi vipi juu
kama kuna walioridhika na hii grade...?
 
Yule mpuuzi wa Redet anaitwa Bana wa ChuoKikuu cha Dar akiona haya matokeo lazima apande hewani na redet kumsafishajamaa hatakubali dokta mwenzake aonge Nchi asemwe vibaya
 
Anyway ndio maksi zetu watanzania, tena ingekuwa mitihani ya ndani mtaani wangekoma.
 
Kufuatia tafiti iliyofanywa na gazeti lisilo fungamana na upande wowote la East African 06/02/2012 kuhusu ubora wa marais wa Africa,Kikwete ameambulia grade C.Utafiti huo ulizingatia vigezo vifuatavyo;
http://www.theeastafrican.co.ke/pag...434746/-/view/asSearch/-/10p3vw1/-/index.html
Ndugu yangu Gold Addict mtu mwenye akili timamu haitaji Takwimu kujua kuwa Kikwete Ameshindwa Kutawala Nchi hii, Kuna watu wanafikira kama Masaburi alivyosema kwa wabunge wa Dar--Ati juzi Kikwete kazoa wanachama zaidi ya 1800 Mwanza?? What the Hell is Wrong with Tanzanians Thinking Capacity???
 
Ndugu yangu Gold Addict mtu mwenye akili timamu haitaji Takwimu kujua kuwa Kikwete Ameshindwa Kutawala Nchi hii, Kuna watu wanafikira kama Masaburi alivyosema kwa wabunge wa Dar--Ati juzi Kikwete kazoa wanachama zaidi ya 1800 Mwanza?? What the Hell is Wrong with Tanzanians Thinking Capacity???

wanachama 1800?
Halafu anajipa air time kweli JK mufilisi..
Hata Dovutwa hawezi akajisifu amepata wanachama idadi kama hiyo!
 
Kufuatia tafiti iliyofanywa na gazeti lisilo fungamana na upande wowote la East African 06/02/2012 kuhusu ubora wa marais wa Africa,Kikwete ameambulia grade C.Utafiti huo ulizingatia vigezo vifuatavyo;
Mo Ibrahim- 15%
Democracy Index-15%
Corruption Index-15%
human development Index-5%
NMG political Index-15%

Kwa vigezo hivyo hapo,grade zilikuwa kama ifuatavyo:
100-70:A
70-60:B
60-50:C
50-45:D
45-40:F
40-30:Intensive Care Unit(ICU)
30-0:morgue

attachment.php




Kwa habari zaidi ingia humu
The East African: Understanding The Region*- Magazine

huko botswana,capeverde,mauritius kuna nini vya ajabu?
 
huko botswana,capeverde,mauritius kuna nini vya ajabu?

Mkuu hizo ni nchi zinazofuata sharia kali. Ukituhumiwa uzinifu unapigwa mawe hadharani, mwizi anakatwa mikono hapo hapo, halafu elimu ya kimagharibi ni marufuku! Dini ni moja tu, marufuku dini zingine; wana misimamo mikali ajabu, midevu hadi magotini! Hii kitu imewasaidia sana kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.
 
Back
Top Bottom